NIffer anachangisha pesa za kuagiza mizigo china, Niffer anachangisha pesa za kuwapa mitaji vijana, leo kachangisha za kuwapa wahanga kelele nyingi

MELEKAHE

JF-Expert Member
Nov 19, 2023
1,003
4,266
Habari wadau.

Binafsi nimeshangaa sana leo hii watu walovyomjia juuu Niffer kuchangisha pesa.

Miaka yote niffer anachangisha pesa na hakuna kesi ya kuvunja sheria yoyote kwake.

Niffer toka nimeanza kumsikia ni anafanya biashara inayohusisha kuchangisha watu pesa.

Biashara yake kuu iliyomtoa ni kuchangisha watu wengi pesa akuagizie mizigo china

Watu wanachangishwa pesa kupitia mitandao hasa instagram kisha niffer kwa kutumia hizo pesa za watu anaenda china kuwanunulia mizigo.

Baada ya hapo watu hao wanachangishwa pesa tena za kutoa mizigo bandarini na Niffer.

Pia niffer ana utaratibu wa kushawishi watu kupitia instagram wachange pesa kwa ajili ya kumuinua kijana mwengine. Mfano anaenda kwa Dobi anaefua nguo kwa mkono.. anarekodi nae video kisha anampost mtandaoni kwamba followera wake wachange pesa kwa kutuma kwenye namba ya niffer ili dobi huyo anunuliwe mashine ya kufulia.

Watu wanachanga pesa zikitimia niffer anaenda kununua mashine na kumpa huyo dobi.

Hivyo suala la niffer kuchangisha pesa sio la ajabu. Kama ni anavunja sheria.. siku zote serikali ilikuwa wapi?
 
Kikubwa asitoke nje ya muongozo
IMG-20241118-WA0054.jpg
 
Habari wadau.

Binafsi nimeshangaa sana leo hii watu walovyomjia juuu Niffer kuchangisha pesa.

Miaka yote niffer anachangisha pesa na hakuna kesi ya kuvunja sheria yoyote kwake.

Niffer toka nimeanza kumsikia ni anafanya biashara inayohusisha kuchangisha watu pesa.

Biashara yake kuu iliyomtoa ni kuchangisha watu wengi pesa akuagizie mizigo china

Watu wanachangishwa pesa kupitia mitandao hasa instagram kisha niffer kwa kutumia hizo pesa za watu anaenda china kuwanunulia mizigo.

Baada ya hapo watu hao wanachangishwa pesa tena za kutoa mizigo bandarini na Niffer.

Pia niffer ana utaratibu wa kushawishi watu kupitia instagram wachange pesa kwa ajili ya kumuinua kijana mwengine. Mfano anaenda kwa Dobi anaefua nguo kwa mkono.. anarekodi nae video kisha anampost mtandaoni kwamba followera wake wachange pesa kwa kutuma kwenye namba ya niffer ili dobi huyo anunuliwe mashine ya kufulia.

Watu wanachanga pesa zikitimia niffer anaenda kununua mashine na kumpa huyo dobi.

Hivyo swala la niffer kuchangisha pesa sio la ajabu. Kama ni anavunja sheria.. siku zote serikali ilikuwa wapi ?
Wanawake mnajuana wenyewe. Huyo miffer si tutamjulia wapi? Utadhani wote tunashinda huko mliko.
 
Niliona nika baki kushika kichwa watanzania wengi ni mbumbu sio critical thinkers bado, unawezaje kuchamga changa tu . Kwa akili ndogo tu unaona uyu dada lazima apige apa
 
Kwani serikali ilisema ina uhaba wa pesa kusaidia wahangwa? Ni kweli alikuwa ana nia njema, ila sio kwa njia hii anayotumia. Ni kama vile ana aibisha serikali (kwamba kwenye maafa serikali inachanga pesa ila kwenye mambo mengine inagawa pesa ovyo). That's the point!
 
Back
Top Bottom