Ofisi ya Nida ubungo wameanzisha biashara nyuma ya zoezi la ugawaji wa vitambulisho linaloendelea.
-
Wafanyakazi wa getini wamekuwa wakitoza elfu moja moja ya kanga kwa wanawake ambao wamekuja wakiwa wamevaa suruali za jeans au nguo ya kata mikono.
Unapofika tu getini kuuliza, kama umevaa suruali au nguo ya kata mikono wanakwambia rudi hauruhusiwi kuingia, tafuta kanga au toa elfu moja wakuazime kanga yao ujifunike na ukitoka unairudisha mwingine tena anakodishwa.
Zoezi hili ni kama limewalenga wanawake pekee na kwa makusudi, kwanini? Kwasababu mwanaume hata aje amevaa kaptura ataingia hakuna wa kumrudisha wala wa kumkodisha suruali ya kitambaa.
Sawa inaeleweka kuwa kuna utaratibu wa mavazi kuingia katika ofisi za serikali, na kanuni hii inafanya kazi kwa wote wanaume na wanawake lakini kwa zoezi linaloendelea Nida Ubungo naona inafanya kazi kwa wanawake tu, wanaume wanaokuja na jeans tena zile za kubana au zile skin Jeans za kiume na kaptura wanaingia kama kawaida.
Licha ya hilo sioni haja ya kuzuia mavazi kwa sababu hizi
Na kama mmeamua kufuata utaratibu huu wa mavazi, fanyeni kwa woteee si tu wanawake, wekeni suruali hapo za kukodisha.
Achanane na hili suala la mavazi. Labda kama mtu amevaa nguo isiyo na staha au amevaa nusu uchi hiyo itaeleweka

- Kwanza zoezi hili linafanyika nje wameweka Tent, hakuna mtu anayeingia ofisini ndani sasa kwanini mnazuia watu wasiingie na suruali ilimradi mtu hajavaa uchi.
- Kurudisha huku watu kwanza kunarudisha nyuma zoezi hili ambalo limewekwa mwisho Februari 28, Baadhi ya watu wanarudi kweli kama hawana elfu moja tu ya kukodosha kanga na hawana taarifa hiyo.