Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 904
- 3,352
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imepanga kusitisha matumizi ya namba za vitambulisho vya taifa kuanzia tarehe 1 Mei mwaka huu kwa wananchi waliotumiwa ujumbe wa kuchukua vitambulisho vyao lakini hawakufanya hivyo.
Akizungumza leo kutoka ofisini kwake, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema kuwa hali ya wananchi kujitokeza kuchukua vitambulisho ni ya kusikitisha licha ya juhudi kubwa za kuwatumia ujumbe mfupi kuwafahamisha mahali pa kuchukua vitambulisho hivyo.
"Inasikitisha sana, tumekuwa tukituma ujumbe mfupi kwa wananchi kuwaelekeza ni mahali gani waende kuchukua vitambulisho vyao lakini idadi ni ndogo sana.
"NIDA tumeamua kuwa tutasitisha matumizi ya namba za vitambulisho, kwa wale wote ambao wameshatukiwa vitambulisho lakini hawajachukua," amesema Kaji.
Katika maelezo yake, Kaji pia aligusia kuwa NIDA ipo karibu kukamilisha mfumo mpya wa usajili ambao utawezesha kusajili watu kuanzia utotoni, hatua inayolenga kuboresha zaidi utambuzi wa wananchi tangu awali.