Nico bambaga hatunaye

RIP Bambaga.

Kwenye picha nayefahamu ni Homeboy Said Mwamba Kizota.

Alifia Dar baada ya kugongwa na gari akitoka Uwanja wa Taifa kuangalia mechi...............
Dah.....RIP Nico

Hivi katika hiyo picha........ni akina nani ambao hatunao tena
 
mpira anachukua hussein masha kwake george masatu kwake khalfan ngassa ngassa anakwenda anapiga majaro pale kwake hamza mponda, hamza mponda na mpira anamtangulizia pale nico bambaga, nicodemus bambaga anakwenda, anakwenda sasa nico bambaga hatari hatari goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
RIP NICO Bambaga
 


93861977.jpg

Kutoka kushoto ni:
Joshua Kilale, Ally Yusuph 'Tigana', Willy Mtendawema, Fomu Felician, Keneth Mkapa, James Tungaraza, Suleiman Mkati, Said Mwamba 'Kizota' na Steven Nemes.

Waliochuchumaa kutoka kushoto ni:
Willy Martin, Mohammed Hussein, Nico Bambaga, Jose Ayoub, Sanifu Lazaro, Edibily Lunyamila na Sekilojo Chambua.[/QUOTE]
RIP Niko
 
RIP Nico Bambaga... Hivi Club zetu/TFF huwa zinawakumbuka hawa Veterans??? Au kesho ndio utawaona wakijazana na makamera ya video/TV msibani na salamu nyingi za pole ... "NG'INDE" waliwahi kuimba wimbo uitwao "Ni majaliwa yake Mungu kuuona mwaka"
 
ALIYEPATA kuwa kiungo wa timu ya soka ya Simba, Nico Bambamba, amefariki usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya jeshi Lugalo alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na homa ya mapafu.
Kwa mujibu wa jirani yake na mchezaji mwenzake wa zamani wa Simba, Dua Saidi, kabla ya kukumbwa na umauti marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa karibu wiki tatu.

Alisema mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa leo nyumbani kwake Kigogo kuanzia saa nne asubuhi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Musoma kwa mazishi yatakayofanyika kesho.

Enzi za uhai wake, marehemu aliwahi pia kuzichezea timu za Yanga, Pan African, Malindi ya Zanzibar pamoja na timu ya Kilimanjaro Stars kwa mafanikio huku akiwa ni mmoja wa wachezaji waliokuwemo katika kikosi kilichotwaa ubingwa wa Chalenji mwaka 1994 huko Uganda.

Marehemu aliyestaafu soka mwaka 2000 ameacha mke Consolata na mtoto mmoja Andy Cole.

Naye Mwandishi Wetu Makuburi Ally anaripoti kuwa aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya wanawake Tanzania (Twiga Stars), Suleiman Gwaje, amefariki dunia jana alfajiri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Ofisa Utawala wa Chama cha Soka Wilaya ya Kinondoni (KIFA), Abbas Ngau, alisema, Gwaje ambaye pia alikuwa mkufunzi wa makocha wa soka wilayani humo alisema, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kifua.

Ngau alisema tatizo hilo lilimchukua muda mrefu kabla ya kuanza kusumbuliwa na tatizo la moyo ambapo jana ilikuwa afanyiwe uchunguzi wa tatizo la moyo na wakati wakisubiri taratibu za uchunguzi, mauti yakamkuta.

Alisema taratibu za msiba zinafanyika nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar es Salam ambako mazishi yatafanyika leo saa saba mchana katika makaburi ya Manjunju Mwananyamala.
 
Pumzika kwa amani Nicodemus Bambaga
Kila nikisikia hli jina naikumbuka klabu ya malindi ya zanzibar ikiwa katika ubora wake na ukwasi wa hali ya juu waliweza kuwatoa Yanga na kuwapeleka zanzibar
Leo masikini ya Mungu timu za zanzibar zimejichokea balaa
 
Pumzika kwa amani Nicodemus Bambaga
Kila nikisikia hli jina naikumbuka klabu ya malindi ya zanzibar ikiwa katika ubora wake na ukwasi wa hali ya juu waliweza kuwatoa Yanga na kuwapeleka zanzibar
Leo masikini ya Mungu timu za zanzibar zimejichokea balaa
Mkuu hili jina lako ndio wewe mwenyewe au ni fake ID?
 
Back
Top Bottom