Ni wapi Kariakoo Wanahifadhi/laza Mizigo uichukue siku nyingine?

JourneyMan

Member
Apr 1, 2020
42
50
Nimezoea kununua bidhaa, baada ya hapo nakusanya shop flani hivi then nikimaliza nachukua Usafiri napeleka dukani.

Sasa kuanzi J3 mpk J5 kuna manunuzi nitafanya, Mzigo utakua mkubwa kdg siwezi kujaza pale ofisini ni kero lakini pia huu unatakiwa uende Mkoani sio hapa Dar,
Hivyo nilikua nataka sehemu ambayo ipo kitaratibu nikishanunua mzigo napeleka nikahifadhi, naendelea tena kwa siku 2 then naipack naituma Huko Bariadi/Maswa/Busega kwa Wasukuma(Hapa pia naomba Msaada Malori ya kwenda huko ya uhakika napata wapi?, Je kuna private pia za kwenda maeneo hayo? Nazipata wapi?)

Niliwaza hotelini ila imani yangu inaniambia ile ni kwa watu wanaolala pale pale hotelini,

Sasa mimi nataka sehemu ya kuhifadhi, nasepa baadae naleta mwingine nafunga, kesho tena naleta naunganisha..

Nina imani wenye hio huduma kiutaratibu wapo, Unaacha mzigo, unapewa risit/namba ya utambulisho unasepa, Basi naomba msaada wa kuelekezwa ni Wapi,
Bila kusahau Wenye uaminifu.
 
Nenda Kidongo Chekundu jirani na JK Sports kuna cargo zipo pale ongea nao wanakupa space
 
nadhani Geita cargo inakufaa

Mizigo yako utalaza hapo

Wapo mtaa wa Amani kama sijasahau
 
Kuna sehemu walikua wanatoa hio huduma ila kwa Ukubwa ila kwa sasa naona wameweka biashara nyingine, ngoja nijarb kuulizia nakuchek.

Mara Paaa unalaza mizigo ya watu kama hio,
Wazee wa kutindua Nguzo wanashusha Ghorofa tena..

Asubuhi unaona watu wanokoa maiti unataka ujifanye eti jana ulilaza viroba vyako hapo, kwanza hamna anayekufahamu, uliemkabizi yupo shimoni, lazima uonekane tapeli,
Hahaaa Sijui utatumia kiswahili gani kwa Wahusika...

Pia nahisi ukipata Cargo husika uatakua Umepiga 2 in 1.
 
Back
Top Bottom