Kwa kweli imefika Mahali hizi timu zetu ziwe na vyanzo vyao binafsi vya kudumu vya mapato,haiwezekani timu zinazjiita wa Kimataifa halafu mchezaji anagoma eti Timu imeshindwa kumlipa mshahara wake.
Hizi timu zetu zimekua kama za mtu mmoja sio ajabu kusikia Baada ya mtu flani kujitoa Kwenye timu,timu inakosa pesa za mshahara kwa Wachezaji.
Ukiangalia wenzetu wa Ulaya Timu zinaendeshwa na wanachama wao na wafadhili mbalimbali ila huku kwetu ni Kinyume kabisa,vyanzo vya Mapato vya timu haviko wazi,utasikia kiongozi huyu ametoa millioni 100 za kusaidia timu,mara kiongozi ametoa ametoa pesa yake mfukoni kumsajili mchezaji flani hii iko Kwetu tu,sijawahi kusikia Mtendaji mkuu wa Manchester/Arsenal ametoa pesa zake mfukoni kusajili mchezaji au kusaidia timu timu zinajiendesha kutokana na vyanzo vyao vya wazi kabisa vya mapato kama vile,mauzo ya jezi,vifaa mbalimbali vya michezo,pesa za makampuni mbalimbali,etc
Ifike mahali na hizi timu zetu ziwe wabunifu kwa kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato ni aibu sana Mchezaji Kugoma kucheza kisa timu imeshindwa kumlipa mshahara wake,Viongozi wa timu zetu na wanachama tubadilike kwa maendeleo ya vilabu vyetu.
Ni hayo tuu.