Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
25,044
35,924
Hakuna kinachozuia IGP kujiuzulu kwa haya yanayoendelea. Mauaji ya watu wasio na hatia tena mchana kweupe wanakwapuliwa kwenda kuuawa ni dhahiri polisi na usalama wanashirikiana kutekeleza hayo.

TISS ipo chini ya ofisi ya Rais na aliitaka ikae chini yake kupitia mabadiliko ya sheria ya TISS inayowapa mamlaka ya kukamata bila kuzingatia uhuru wa raia na kuwapatia kinga wanapoua.

IGP Wambura ajjuzulu, Rais Samia awajibike.

Uhai na usalama wa watanzania upo katika mashaka makubwa.

Soma Pia: Rais Samia aagiza uchunguzi wa Kifo cha Ali Mohamed Kibao
 
Hii nchi hakuna mwenye uchungu nayo kila mtu anatizama maslahi yake hao TISS vimeo tu hakuna kitu.
 
Hii nchi hakuna mwenye uchungu nayo kila mtu anatizama maslahi yake hao TISS vimeo tu hakuna kitu.
Kuna dogo nilimuona ni TISS tulisoma nae secondary afu alikua kilaza nilishangaa kusikia TISS sema baba yake ni kanali nkasema kazi ipo
 
Ile Sheria Ile!soon itaanza kuwageuka kama kweli Sheria inahalalisha utekaji na uuaji!

Naamini TISS wataanza pande zao ndipo na wao watapaza sauti saw na watz wengine!
 
Kwa hshima na taadhima, Mh. Rais Samia kujivua uhusika a serikali yako na kifo hiki na utekaji unaoendelea wafute kazi/watimue DGIS na IGP na Awadhi! Utakuwa umejivua uhusika wa hili na yote ya utekaji!

Utakuwa umebadili dhana iliyokwisha jengeka kuwa haya yana baraka zako!

Soma Pia: Rais Samia aagiza uchunguzi wa Kifo cha Ali Mohamed Kibao
Haya yatafanyika tu siku moja mtoto wa kiongozi yeyoye akikumbwa na kadhia hii....
 
Rais Samia masikitiko yako juu ya kifo cha Ally Kibao yalipaswa kuambatana na kuwatimua kazi haraka CDF na IGP kisha baadaye ungewatimua waziri wa ulinzi, waziri wa mambo ya ndani na kumaliza na RPC wa Dar na Pwani.
Maana yake Tanzania iko katika uvamizi wa kivita au ujambazi mkubwa unaofanywa na watu wenye uwezo wa kivita (kijeshi).
Kama hutawatimua kazi hao niliowataja maana yake unaafiki kuwa watekaji na wauaji wako ndani ya serikali yako.
Swali jingine: Je, wanafanya kwa baraka zako au wako na mission yao nyingine ambayo wewe huijui?
 
Wote wapo ndani ya kikapu kimoja. Mpaka watakapokamatwa wahusika na kuchukuliwa hatua, masikitiko hayo ni ya kinafiki
 
Back
Top Bottom