Ni vema polisi wakalipa gharama za matibabu za shujaa huyu

Hii itamsaidia kuacha kiherehere, hana akili hata kidogo, wenzio wana mashine wewe unachomekea bodaboda chako??? Wangemmiminia za kutosha ili na wengine wajifunze.

unatetea majambazi au ulipenda huyo shujaa afe !?

pengne hayo majambazi yasingekamatwa... yangeweza kuua watu wengne ktk matukio ya uhalifu.
 
Hii habari haina maslahi kwa Clouds wangeshampigia chapuo kama yule dada wa juzi Chuo cha Mzumbe.
Kuna vitu ukivitizama kwa makini utaona itakua aibu kwa serikali kwa jambo ambalo wao wameweka idara kusimamia(polisi) lakini akatokea mtu akaonesha uzalendo na kuhatarisha maisha yake lakini serikali isubiri jambo hili lifanywe na clouds!hapana hii si sawa na naamini hata wao hawawezi kubali.
 
Mkuu siwatetei majambazi, ila unaootaka kufanya jambo ni lazima kuangalia both sides ,
unatetea majambazi au ulipenda huyo shujaa afe !?

pengne hayo majambazi yasingekamatwa... yangeweza kuua watu wengne ktk matukio ya uhalifu.
 
Kwanza nianze kwakusema mpaka hapa silaumu kitengo cha polisi kwani huenda hakijafanya hili kwakukosa taarifa.

Leo kupitia taarifa ya habari ya clouds TV ameoneshwa kijana dereva wa bodaboda ambaye kwa ushujaa mkubwa alifanikisha kukamatwa kwa jambazi Dar es Salaam.

Shujaa huyu ambaye aliwachomekea majambazi akiwa kwenye pikipiki na kupelekea yeye pamoja na pikipiki ya majambazi kuanguka jambo ambalo lilifanikisha kukamatwa kwa majambazi hao kwa urahisi na askari.

Shujaa huyu licha ya kupata majeraha kwakuanguka na pikipiki lakini pia alipigwa risasi na jambazi iliopelekea kukimbizwa Muhimbili.

Amepata tiba lakini tatizo ni gharama za matibabu inahitajika 500,000 ili aruhusiwe pesa ambayo yeye hana.

Naamini kama polisi hua mnatangaza mpaka dau la 1,000,000 ili kufanikisha kukamatwa kwa majambazi naamini hamshindwi kulipa 500,000 ya matibabu na hata pesa ya ziada kama motisha kwa ujasiri aliounesha.
 
kwa nini hao boda boda wasipitishe daftari la mchango mitaani watu tuchangie kidogo kidogo?
 
Kwanza nianze kwakusema mpaka hapa silaumu kitengo cha polisi kwani huenda hakijafanya hili kwakukosa taarifa.

Leo kupitia taarifa ya habari ya clouds TV ameoneshwa kijana dereva wa bodaboda ambaye kwa ushujaa mkubwa alifanikisha kukamatwa kwa jambazi Dar es Salaam.

Shujaa huyu ambaye aliwachomekea majambazi akiwa kwenye pikipiki na kupelekea yeye pamoja na pikipiki ya majambazi kuanguka jambo ambalo lilifanikisha kukamatwa kwa majambazi hao kwa urahisi na askari.

Shujaa huyu licha ya kupata majeraha kwakuanguka na pikipiki lakini pia alipigwa risasi na jambazi iliopelekea kukimbizwa Muhimbili.

Amepata tiba lakini tatizo ni gharama za matibabu inahitajika 500,000 ili aruhusiwe pesa ambayo yeye hana.

Naamini kama polisi hua mnatangaza mpaka dau la 1,000,000 ili kufanikisha kukamatwa kwa majambazi naamini hamshindwi kulipa 500,000 ya matibabu na hata pesa ya ziada kama motisha kwa ujasiri aliounesha.
Nani alilijua hili? Kwanini si angelitaarifu katika mamlaka ili kuona kama polisi ilishindwa kumhudumia? Ni nani aliyejua kama alidhibiti kukimbia kwa majambazi au ilitokea bahati mbaya? Je, ilifahamika kiofisi kuwa alifanya hivyo kwa kusaidia majambazi wakamatwe? Nani aliyempeleka hospitali? Je, aliyempeleka alifahamu kuwa alitenda tendo la kuwadhibiti majambazi na alihitaji msaada? Polisi walijua? Je, alipopelekwa mhimbili polisi walilifahamu hilo? Na walijua kuwa alijitolea kuwasaidia na sasa anahitaji msaada wao? Je, ni mmoja katika mashahidi wa mahakamani dhidi ya kesi ya hao majambazi?

Ifike hatua tusilaumu bila kuwa na habari muhimu.
 
Ndio maana tumetoa taarifa na hakuna sehemu nimeilaumu polisi@spade
 
Hii itamsaidia kuacha kiherehere, hana akili hata kidogo, wenzio wana mashine wewe unachomekea bodaboda chako??? Wangemmiminia za kutosha ili na wengine wajifunze.
Mtoto wa Kuku maneno makali hayo umetumia,tunahitaji wazarendo kama hawa
 
SIDHANI KAMA ILIKUA SAHIHI KUMUONYESHA SURA YAKE...COZ ITAMUARIBIA MAISHA YAKE YALOBAKI
 
Jana niliandika thread ili kwapamoja tupaze sauti kwa serikali imsaidie yule shujaa dereva bodaboda alieshindwa kuruhusiwa hospitali Muhimbili akidaiwa gharama za matibabu 500,000.
Dereva huyu alipigwa risasi na majambazi baada ya kuwafukuza na kuwachomekea majambazi hao jambo ambalo lilipelekea yeye pamoja na majambazi kuanguka chini na pikipiki zao.
Hatimaye Mh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amemtoa hospitali na kumzawadia pikipiki.
Hongera paul Makonda wewe ni mfano wakuigwa.

Copy and paste
 
Back
Top Bottom