Ni ujinga kuwalaumu ACACIA kwa makosa ya serikali ya CCM

Sidhani kama bila tamaa na ufisadi wa viongozi wetu ACACIA wangefanya utapeli wowote ule, kila walichokitaka ACACIA walipewa baraka na mwongozo wa kutosha kutoka kwa viongozi wetu.

Hizi sheria tunazosema mbovu ACACIA hawakutokanazo kwao, zilitungwa na viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kulinda rasilimali za nchi yetu chini ya serikali ya CCM.


Ni utani..lile lile bunge lililopitisha sheria mbovu ndio hilo hilo likarekebishe...utani huu....yule yule anaelipa bunge mwongozo wa kupitisha sheria ndio huyo huyo analipa bunge mwongozo wa kurekebisha sheria.?

Kuna haja ya kuanzisha mjadala wa kitaifa kikatiba kuhusu umuhimu wa bunge letu kwa mustakabali wa Taifa letu.....

ikiwezekana hili livunjwe liundwe lingine lenye weledi.....ama tuanzishe lingine lisilo na itikadi ya vyama ili kusahihisha makosa ya bunge lililopo sasa.... maana hili linaburuzwa tu na serikali.

Bila katiba mpya mihimili yote inayojiita iko huru itaendelea kuwa kwapani mwa mhimili uliojikita chini.... rejea agizo la Rais leo kwa spika kuhusu wabunge wanaoitwa wakorofi.


Mungu ibariki Tanzania.!
Nikweli kabisa , mie binafsi nashangaa kuona watanzania tunaelekeza shutuma kwa hawa wawekezaji badala ya kuzielekeza kwa viongozi wetu
 
Namshukuru rais Kwa kuthubutu kuwa muwazi Kwa hili na imani yangu kwamba rais alipokuwa mbunge angekuwa shujaa Wa nchi hii kama angeungana na kambi ya upinzani kupinga vikari kutaka mikataba yote ya madini ambayo imehubiliwa sana bungeni

Lakini vikao vya wabunge wa CCM Kupanga mikakati ndo kilipelekea mikataba ya hivyo kabisa na itakuwa vizuri awaambie wabunge wake waache kuitana pembeni kupeana mikakati iliyopangwa na utawala na hill ni tatizo kubwa mfano mikataba Wa gesi ulivyofanyika ni aibu Kwa taifa na kibaya kabisa hats hawa maspika wetu wao wanatakiwa waongoze bunge wasiegemee upande wa chama chao na hill limepelekea wabunge kufanya ovyo kutokana na spika!
 
Nimekuelewa Mkuu idawa .

Huu Mzigo wa MAVI ingebidi waubebe CCM, lakini nashangaa wanabebeshwa ACACIA MINING na akina LISSU na Wapinzani wengine.

Mpaka inafikia hatua MAGUFULI anamuagiza Spika awafukuze wanaokuwa na mawazo mbadala bungeni, ili wakija huku uraiani yeye awashughulikie kupitia vyombo vya Dola!

Hii sio sawa kabisa! Na ni kinyume kabisa na Katiba yetu!
Tatizo la CCM ni kutuona watanzania wote wajinga hatuwezi kufikiri ila wao tu.

Hii yote sababu ya kuwa na Katiba ya chama kimoja ndani ya vyama vingi.. .ndio maana bunge linakuwa kama tawi la ccm.
 
Hii ni hatari sana kwa huyu mchawi anayeitwa ccm, tangia uhuru hadi leo nchi hii haijawahi kutawaliwa na chama kingine isipokuwa ccm.

Mikataba yote ya kuibia wananchi imesainiwa na ccm. Ufisaidi wote ambao umefanyika nchini umefanyika china ya serikali ya chama cha mapinduzi.

Watu ambao wameibia nchi hii hadi kugeuka shamba la bibi wote ni makada wa ccm. Leo tunaambiwa Acacia haikuwa imesajiliwa, inashangaza nchi yenye usalama wa taifa, vyombo mbalimbali vya dola, yenye intelejensia ya kugundua mikutano ya vyama vya upinzani kuna watu waliopanga kufanya funjo au walikusudia kufanya uovu mbaya, leo tunaambiwa kampuni iliyokuwa inasafirisha makontena hadi 270 kwa wakati mmoja haijasajiliwa ni kituko.

CCM ndio waliofanya yote haya, badala ya kutuomba radhi watanzania leo wanaibuka na mbwembwe za uongo kwamba wao wanatetea wananchi ila wapinzani ndio wanatetea wezi. this is not serious. siku zote mchawi ujibaraguza harakaharaka ili aonekane ana huruma kumbe ni yeye aliyeuwa

CCM ndio waliologa nchi wasijifanye waganga wa kutibu nchi. Ni wao waliopiga meza ndioooooooooo akiwemo naniiiiiiiiiiiiiiiii
Mkuu mambo mengine ukihoji sana unaweza kuugua kichaa.

Ila kwa sababu tupo dunia ya tatu acha twende nayo hivyo hivyo japo tunaumia.
 
Nimekuelewa Mkuu idawa .

Huu Mzigo wa MAVI ingebidi waubebe CCM, lakini nashangaa wanabebeshwa ACACIA MINING na akina LISSU na Wapinzani wengine.

Mpaka inafikia hatua MAGUFULI anamuagiza Spika awafukuze wanaokuwa na mawazo mbadala bungeni, ili wakija huku uraiani yeye awashughulikie kupitia vyombo vya Dola!

Hii sio sawa kabisa! Na ni kinyume kabisa na Katiba yetu!
Mbona kwenye lawama hizi huwa hamumkumbuki lowasa na sumaye????huwa mkoje nyie?
 
CCM ni matakataka wote hamna cha nani wala nani,mtu unajifanya unauchungu ila kipindi unanyanyua makwapa na kushangilia kwa kusema NDIYO ipite uliona sawa tu..Viwavi jeshi kama kina polepole wanajifanya kusema wamethubutu...umethubutu/mmethubutu nini?
Kifupi tunahitaji bunge lingine zaidi ya hili linalomilikiwa na akina Lusinde...kama tutaendelea kutegemea bunge hili basi tutakuwa tunapiga hatua kumi mbele na kurudi hatua ishirini nyuma halafu tunajipongeza.
 
Zimamoto akitaka kuzima moto baada ya yeye mwenyewe ndiye kuwa kaanzisha moto huo utampongeza kwa kutaka kuzima moto au utamlaumu kwa kuanzisha moto awali kabisa?
Kwa akili yetu tutampongeza kwa kuzima moto, ila kwa sababu hatutaki kuumiza vichwa vyetu kuuliza nini chanzo cha moto....basi jamaa atakuwa shujaa wa kwa kuzima moto uliouanzisha yeye mwenyewe.
 
Mkuu CCM walituingiza cka kwa kauli zao za NDIYOO ila hii haiwezi kutuzuia sisi kudai haki yetu au kurekebisha pale tunapoona kuna wizi.
CCM walihusika kutuingiza kwenye mikataba mibovu na sheria za ajabu na ACACIA nao ni WAHUNI
Sasa ndo watukanwe wapinzani?
KATIKA HILI TAIFA KWANZA VYAMA BADAE!

uCCM & uCDM sijui kijani na blue hizi ni fursa za watu kupiga hela tu.
 
Mkuu idawa sio kwamba ccm hawajui kwamba wao ndio wameingiza nchi hii kwenye hiyo mikataba, ila wanachofanya ni propaganda ili kukwepa aibu hiyo. Na kwa bahati mbaya wananchi wa nchi hii hawana uwezo wa kuhoji mambo makubwa kama haya. Uthibitisho wa hilo ni kuona watu wenye kashfa za wazi kwenye nchi hii wanajitokeza kugombea uongozi na wanapata kura tena nyingi.

Usishangae leo rais anafanya hayo anaungwa mkono na watu wengi huku wakitokwa na mishipa ya shingo. Lakini akija rais mwingine akaunga mkono huo wizi utashangaa watu wanamuunga mkono na kusema rais wa sasa alikimbiza wawekezaji.
Mkuu ndio maana wengine tunaona ni ujinga kupongeza serikali ileile iliyoingia mikataba ya hovyo.

ccm ni ndio kansa ya nchi yetu.
 
Ccm hata wamuweke malaika atakimbia sembuse huyu mwanadamu

Ngoja tuendelee kulala usingizi huyu atapita atakuja mwingine vilevile mpaka tutakapokuwa na akili
Tunahitaji katiba itakayo ifanya mihimili huru iwe huru kweli, sio mbunge anaogopa kukosoa chama chake kisa atavuliwa uanachama.

Hapo hatuwezi kufika.
 
CCM ilikuwa mbioni kuiba kura na kufirigisa uchaguzi kule Zanzibar huku watu wakifanya vitu vyao.

By the way hawa waliojiuzia migodi akina Mkapa and Co. mbona hatusikii kutajwa ???
Katiba yetu ndio tatizo.
 
I support My Presdent on this.Haijalishi waliotufikisha hapa ni kina nani maadamu Raisi ameonyesha nia ya dhati kwa vitendo kurudisha kilicho chetu.IM WITH HIM
Hicho chenu kilichorudishwa kilitolewa na nani.?
 
Mkuu CCM walituingiza cka kwa kauli zao za NDIYOO ila hii haiwezi kutuzuia sisi kudai haki yetu au kurekebisha pale tunapoona kuna wizi.
CCM walihusika kutuingiza kwenye mikataba mibovu na sheria za ajabu na ACACIA nao ni WAHUNI

KATIKA HILI TAIFA KWANZA VYAMA BADAE!

uCCM & uCDM sijui kijani na blue hizi ni fursa za watu kupiga hela tu.
Unachoongea ni kweli lakini huo uhuni ACACIA walipewa na serikali ya ccm.
 
Back
Top Bottom