Ni ujinga kuwalaumu ACACIA kwa makosa ya serikali ya CCM

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,282
38,359
Sidhani kama bila tamaa na ufisadi wa viongozi wetu ACACIA wangefanya utapeli wowote ule, kila walichokitaka ACACIA walipewa baraka na mwongozo wa kutosha kutoka kwa viongozi wetu.

Hizi sheria tunazosema mbovu ACACIA hawakutokanazo kwao, zilitungwa na viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kulinda rasilimali za nchi yetu chini ya serikali ya CCM.


Ni utani..lile lile bunge lililopitisha sheria mbovu ndio hilo hilo likarekebishe...utani huu....yule yule anaelipa bunge mwongozo wa kupitisha sheria ndio huyo huyo analipa bunge mwongozo wa kurekebisha sheria.?

Kuna haja ya kuanzisha mjadala wa kitaifa kikatiba kuhusu umuhimu wa bunge letu kwa mustakabali wa Taifa letu.....

ikiwezekana hili livunjwe liundwe lingine lenye weledi.....ama tuanzishe lingine lisilo na itikadi ya vyama ili kusahihisha makosa ya bunge lililopo sasa.... maana hili linaburuzwa tu na serikali.

Bila katiba mpya mihimili yote inayojiita iko huru itaendelea kuwa kwapani mwa mhimili uliojikita chini.... rejea agizo la Rais leo kwa spika kuhusu wabunge wanaoitwa wakorofi.


Mungu ibariki Tanzania.!
 
Basi tuwasifue ACACIA ili uendelee kupata ujira wako mkuu
 
Nimekuelewa Mkuu idawa .

Huu Mzigo wa MAVI ingebidi waubebe CCM, lakini nashangaa wanabebeshwa ACACIA MINING na akina LISSU na Wapinzani wengine.

Mpaka inafikia hatua MAGUFULI anamuagiza Spika awafukuze wanaokuwa na mawazo mbadala bungeni, ili wakija huku uraiani yeye awashughulikie kupitia vyombo vya Dola!

Hii sio sawa kabisa! Na ni kinyume kabisa na Katiba yetu!
 


Hii ni hatari sana kwa huyu mchawi anayeitwa CCM, tangia uhuru hadi leo nchi hii haijawahi kutawaliwa na chama kingine isipokuwa ccm.

Mikataba yote ya kuibia wananchi imesainiwa na CCM. Ufisaidi wote ambao umefanyika nchini umefanyika china ya serikali ya chama cha mapinduzi.

Watu ambao wameibia nchi hii hadi kugeuka shamba la bibi wote ni makada wa CCM. Leo tunaambiwa Acacia haikuwa imesajiliwa, inashangaza nchi yenye usalama wa taifa, vyombo mbalimbali vya dola, yenye intelejensia ya kugundua mikutano ya vyama vya upinzani kuna watu waliopanga kufanya funjo au walikusudia kufanya uovu mbaya, leo tunaambiwa kampuni iliyokuwa inasafirisha makontena hadi 270 kwa wakati mmoja haijasajiliwa ni kituko.

CCM ndio waliofanya yote haya, badala ya kutuomba radhi watanzania leo wanaibuka na mbwembwe za uongo kwamba wao wanatetea wananchi ila wapinzani ndio wanatetea wezi. this is not serious. siku zote mchawi ujibaraguza harakaharaka ili aonekane ana huruma kumbe ni yeye aliyeuwa

CCM ndio waliologa nchi wasijifanye waganga wa kutibu nchi. Ni wao waliopiga meza ndioooooooooo akiwemo naniiiiiiiiiiiiiiiii
 
Ni actually upumbavu kushabikia mwizi anapokuibia, halafu mtu unahangilia kama zuzu vile.
 
Sitaki tuendelee kuibiwa ila sipendi unafiki wa ccm na serikali yao!!! Kabla acacia hawajaondoka tuanze na hawa ccm waliosema ndiioooooo (akiwemo magufuli )ili mikataba mibovu kama hii ipite!! Hawa wote ina bidi wawajibishwe!!
Hadi lowasa na sumaye alisema ndiooo lakin kwa sasa ndo mnawalamba
 
Mkuu idawa sio kwamba ccm hawajui kwamba wao ndio wameingiza nchi hii kwenye hiyo mikataba, ila wanachofanya ni propaganda ili kukwepa aibu hiyo. Na kwa bahati mbaya wananchi wa nchi hii hawana uwezo wa kuhoji mambo makubwa kama haya. Uthibitisho wa hilo ni kuona watu wenye kashfa za wazi kwenye nchi hii wanajitokeza kugombea uongozi na wanapata kura tena nyingi.

Usishangae leo rais anafanya hayo anaungwa mkono na watu wengi huku wakitokwa na mishipa ya shingo. Lakini akija rais mwingine akaunga mkono huo wizi utashangaa watu wanamuunga mkono na kusema rais wa sasa alikimbiza wawekezaji.
 


CCM ilikuwa mbioni kuiba kura na kufirigisa uchaguzi kule Zanzibar huku watu wakifanya vitu vyao.

By the way hawa waliojiuzia migodi akina Mkapa and Co. mbona hatusikii kutajwa ???
 
I support My Presdent on this.Haijalishi waliotufikisha hapa ni kina nani maadamu Raisi ameonyesha nia ya dhati kwa vitendo kurudisha kilicho chetu.IM WITH HIM
 
Mkuu mantiki ya hoja yangu ni kwamba viongozi wetu waliokuwepo wakati huo ndio chanzo cha kila kitu.

Kwani hizi tunazosema sheri mbovu walipitisha ACACIA.?

ACACIA kazi yao ilikuwa ni kurubuni tu.
Mkuu CCM walituingiza cka kwa kauli zao za NDIYOO ila hii haiwezi kutuzuia sisi kudai haki yetu au kurekebisha pale tunapoona kuna wizi.
CCM walihusika kutuingiza kwenye mikataba mibovu na sheria za ajabu na ACACIA nao ni WAHUNI

KATIKA HILI TAIFA KWANZA VYAMA BADAE!

uCCM & uCDM sijui kijani na blue hizi ni fursa za watu kupiga hela tu.
 
Mwenyekiti Mao anashamgaa tumelogwa na nani wakati waliosaini mikataba wapo,waliokuwa wanawasimamia hao waliosaini mikataba wapo,hao ndio waliotuloga tukashidwa kuwauliza mapaka sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…