Ni Tanzania pekee Jaji Mkuu ameandikwa kwa Penseli

Hizi ni hisia
Rais anapendekezewa orodha kutoka katika tume ya uteuzi wa majaji.
Nadhani ungefanya utafiti wako huko kwenye hiyo tume kumetokea nini badala ya kuja na assumption za dunia nzima.
Hata hivyo kuwa kaimu Jaji,hakumpunguzii hata chembe ya madaraka katika kutimiza majukumu yake kama kaimu jaji mkuu
 
Kifungu namba 118 cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kinaruhusu kwa mazingira matatu: 1. post ya CJ ipo wazi, 2. CJ yuko nje ya nchi, 3. CJ anaumwa.
Kwenye ipo wazi labda walifikiria CJ kafa au kupoteza sifa. Lakini normal succession ni maajabu kabisa.
Kenya Wamefanya kwao juzi na lazima Bunge kupitia kamati husika wapitishe
 
Mahakama ni moja kati ya muhimili wa nchi yetu. Unatakiwa kuwa huru na usitomaswe tomaswe katika namna yeyote na mda wote.

Vilevile moja kati ya tuezi ambazo rais anaweza kuteua tu na hawezi kwa mujibu wa katiba kutengua ni Jaji Mkuu na Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Hata kama utamuundia fitna vipi utaishia kumtazama tu.......

Baada ya Jaji Mkuu wa Tanzania Athumani Chande kumstaafu. Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Prof.Ibrahim Juma kuwa Jaji Mkuu lakini akiwa Kaimu Jaji Mkuu yaani Acting Chief Justice. Kwa tafsiri ya kimtaa-mtaa Jaji huyu kwenye Ujaji Mkuu kaandikiwa kwa penseli na kwamba anaweza kufutwa mda wowote na akaandikwa mtu mwingine....nadhani mnanielewa....

Nimefanya utafiti nchi mbalimbali sijapata kuona Jaji Mkuu anakaimishwa. Hii ni kutokana na unyeti wa nafasi yake na kumuongezea mamlaka na nguvu. Lakini hapa kwetu ni kinyume.

Je,
1.Mamlaka ya uteuzi haioni kama kukaimisha nafasi kubwa kama hii kunamuondolea Jaji power ya kufanya maamuzi.

2.Kwa nini mamlaka haikuona haja ya kumteua bwana huyu kuwa Chief kamili

3.Nini madhara ya uteuzi kama huu kisheria?Hatuoni kama muhimili huu umewekwa rehani?

Naomba majibu na sio kashfa
Mwache Rais afanye kazi yake kwa kadri aonavyo inafaa hakuna mhimili ambao hauwezi kuingiliwa pale inapolazimika.
 
Ilikuwa na haja gani kumteua nusu? Haya mambo ya ushabiki hayapendezi wakati wa mambo ya msingi, nchi ni yetu sote na ina katiba na sheria watu wanauliza swali la msingi wewe unajibu aliyemteua inahusu nini?

Tujaribu kuwa huru wa fikra na sio ushabiki ambao hata roho yako ipo kinyume na unachokiandika.

Kwa tafsiri ya wengi kusema mahakama haiko huru baadhi ya indication zake moja wapo ni hiyo ya mtoa hoja.
Hujanielewa atashauriwa na nani na yeye kila kitu anajua na wanamuogopa?
 
Ukipata madaraka cheza Na Wa kwenu!_jamaa zangu Wa namtumbo mlie Tu! Sugueni bech!watoka povu nawaonea huruma kaomben buku7lumumba getini!
 
Toka aingie madarakani alijua wazi ni lini CJ anastaafu. Ni ajabu mchakato wa kumpata mwingine haukufanyika.

Au hawakujua kama ilivyokuwa kwa kamishna wa tume ya madawa ya kulevya?

Only in Tanzania.

Kaimu CJ ipo kikatiba? Katika hali ya kawaida kama CJ amesafiri nani hukaimu nafasi yake? Kwa nini huyo asikaimu hadi apatikane CJ mwingine?
Mambo yakizidi tutamuomba ajiuzulu kama alivyotolewa kafara Posi .
 
Kwenye ipo wazi labda walifikiria CJ kafa au kupoteza sifa. Lakini normal succession ni maajabu kabisa.
Kenya Wamefanya kwao juzi na lazima Bunge kupitia kamati husika wapitishe

Katiba inasema post ya CJ inakuwa wazi endapo: 1. amefikisha umri wa kustaafu, 2. amejiuzulu, 3. ofisi ipo wazi kwa kuumwa au kifo, 4. anaondolewa kwenye post ya CJ na Rais
 
Jamani si kaimu CJ tu, hata CJ mwenyewe hana sucurity of tunure kwa mujibu wa katiba yenu. Anaweza kuondolewa na rais muda wowote abakie na ujaji wa kawaida. Ujaji ndio rais amewekewa utaratibu mgumu kuwaondoa. Ngoja niwaletee kifungu husika cha katiba
 
Hii ndo style ya M7 wakuu kwa miaka 10 ata Uganda haina CJ kuna mtu anakaimu yaani...KAGAME MUNGU ANAKUONA
 
Kwa ukweli katiba yetu ina contradictions nyingi sana. Haya mambo yalitakiwa yawe professional zaidi ya kuwa ya kisiasa.

Rais ana madaraka ya ki mungumtu sana. Wenzetu Kenya wana mfano mzuri wa kumweka CJ ofisini na hata uongozi wa IEBC kwa wenye taaluma hiyo kuomba
Ndiyo maana kutokana na Kenya kuwa na mfumo wa mahakama iliyo huru tumeshuhudia Mahakama ya Rufaa ikiwaachia huru wale viongozi wa vyama vya wafanyakazi waliokuwa wamefungwa jela kwa ajili ya kuongoza mgomo wa madaktari.

Hebu tufanye comparison na TZ.

Mbunge wa Arusha mjini yupo Rumande kwa zaidi ya miezi 3 kwa makosa anayotuhumiwa ambayo yana dhamana!

Mbunge LijiaLikali amefungwa jela miezi 6 bila kupewa option ya faini kwa 'kubambikiwa' kupiga maaskari!

Naye Suleiman Mathew, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi naye amehukumiwa kwenda jela miezi 8 eti kwa kosa la kufanya mkutano wa kisiasa ambao haukuwa umepewa kibali na Polisi!

Kwa TZ tunayokwenda nayo ni kama vile 'indirect' tunalazimishwa watanzania wote tuwe wanaccm!
 
Ibara ya 118 (2)(c) ya Katiba, Rais anaweza kumuondoa CJ kwenye post hiyo muda wowote. Kifungu hicho hakiweki ule utaratibu mugumu wa kumuondoa jaji wa mahakama kuu au ile ya Rufaa. Utata from that framing of the provision. Anaondolewa u CJ anabaki Jaji wa kawaida
 
Katiba inasema post ya CJ inakuwa wazi endapo: 1. amefikisha umri wa kustaafu, 2. amejiuzulu, 3. ofisi ipo wazi kwa kuumwa au kifo, 4. anaondolewa kwenye post ya CJ na Rais
Labda hakuna kifungu kinawafunga kuhakikisha ili mmoja akistaafu mwingine apatikane ndani ya muda fulani.
Kenya waliona hilo. Katiba ya sasa hairuhusu ombwe hata kidogo. Mchakato unaanza mapema na tume yao ya mahakama kupendekeza majina kadhaa ya watu kuomba. Wana muda maalum wa kufanya hivyo. Baada ya vetting wanapeleka majina matatu kwa Rais. Yeye amepewa week mbili kupendekeza jina moja kwenye kamati husika ya Bunge ambao humuhoji na kupitisha au kukataa.
Wakikubali jina harudi kwa Rais ili amteue rasmi!
 
Ndiyo maana kutokana na Kenya kuwa na mfumo wa mahakama iliyo huru tumeshuhudia Mahakama ya Rufaa ikiwaachia huru wale viongozi wa vyama vya wafanyakazi waliokuwa wamefungwa jela kwa ajili ya kuongoza mgomo wa madaktari.

Hebu tufanye comparison na TZ.

Mbunge wa Arusha mjini yupo Rumande kwa zaidi ya miezi 3 kwa makosa anayotuhumiwa ambayo yana dhamana!

Mbunge LijiaLikali amefungwa jela miezi 6 bila kupewa option ya faini kwa 'kubambikiwa' kupiga maaskari!

Naye Suleiman Mathew, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi naye amehukumiwa kwenda jela miezi 8 eti kwa kosa la kufanya mkutano wa kisiasa ambao haukuwa umepewa kibali na Polisi!

Kwa TZ tunayokwenda nayo ni kama vile 'indirect' tinalazimishwa watanzania wote tuwe wanaccm!
Haya yote yanatukuta kwa sababu ya uoga wetu waTz kutokubali kufia unachokiamini . Africa kusini, Ghana, Nigeria, Kenya etc mpaka kwanza watu walifia nchi ndiyo mkae kwa heshima kuiweka taratibu za kuongoza nchi, otherwise tukubali kufuata matakwa ya ccm daima
 
Hoja yako ingekuwa na mshiko kama ungekuja na kifungu cha katiba kinachozuia uteuzi wa Kaimu Jaji Mkuu.

Kinyume na hapo ni yaleyale na kupinga kila kitu.
Nafikiri na wewe post yako ingekuwa na mashiko kama ungeleta ibara ya katiba inayotambua uwepo wa kaimu jaji mkuu!
 
Back
Top Bottom