Ni sahihi Mh. Rais kuzungumza lugha ya kabila lake katika mkutano wa hadhara?

Nimeona leo kule shinyanga, anachomekea kuzungumza kwa kisukuma.

je haiwezi kuwa ni kuonesha kuwa "mimi ni wenu?" kuna ulazima gani wa kuzungumza kisukuma ktk mkutano unaotazamwa na watanzania wa makabila 120 nchi nzima?

nawasilisha!
Kisukuma na kichaga ni lugha za kikanda siyo kikabila hata kimaasai pia!Sasa ni kawaida huko duniani mtawala kuongea lugha ya kanda husika anapoizuru kama anaifahamu wala siyo dhambi!
 
Kuongea kilugha ni namna tu ya kuelewana na audience yako. Kikwete alimfanyia kampeini mwanaye Chalinze kwa kilugha. Lowassa alisema kapewa "mahaba" alipokuwa Zanzibar wakamshangaa. Mke wake akihutubia Machame akawaomba waambie Wachagga kokote waliko wamchague Lowassa "kwa sababu najua Wachagga ndugu zenu wako wengi huko Bara". Baadaye James Mbatiya akaimba Tenzi za Rohoni kwenye uzidunzi Jangwani, na Lowassa akaenda Tabora Kanisa la Walutheri (wengi wao si watu wa Tabora). Hapo ndo jiulize mwenyewe ukabila ni upi na maongezi tu ni yapi.
 
Nimeona leo kule shinyanga, anachomekea kuzungumza kwa kisukuma.

je haiwezi kuwa ni kuonesha kuwa "mimi ni wenu?" kuna ulazima gani wa kuzungumza kisukuma ktk mkutano unaotazamwa na watanzania wa makabila 120 nchi nzima?

nawasilisha!
Huyu jamaa ni mkabila sana,hata sisi wasukuma tusiotoka chato hatupendi
 
Kama kiongozi wa kitaifa kuwafanya hivyo ni kosa kubwa maana hata hapo anapohutubia kuna watu wa makabila mengine wasiojua kisukuma...uvccm watatetea na hilo maana hawaoni kosa kwa mkuu
Mkuu ni Malaika hakosei.Ila ingekuwa pande ya kule kwetu ingekuwa ni maIngaombwe tyngesemwa mpaka chooni
 
Wafuasi wa mamvi bhana (sio chadema!), yaani mmekosa contents za maana kwenye hotuba hadi mjadili kisukuma??

Katika Makabila JKN aliyokataa yasipewe nafasi ya kuwa Rais ni Wasukuma,Wa haya,wanyakyusa,wachagga na wanyamwezi.Yaani makabila makubwa adhari yake ndiyo tunayoiona,Ukabika at first class
 
Mbona alianza long time back... toka kampeni zake alikuwa anatupia kisukuma tu..!!
 
Back
Top Bottom