MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
- Thread starter
-
- #161
Ni kweli, Lowassa angekuwa type yangu lazima ningekuwa fisadi papa!Mleta mada umevimbiwa mihogo, lowassa siyo type yako kaa mbali kabisa,
Acha kudanganya watu wewe,Ukweli ni kwamba endapo Lowassa angekuwa hana busara wala hekima, na kuamua kuwashawishi watanzania zaidi ya MIL 6 waingie barabarani, leo hii nchi nzima ingekuwa eneo la makaburi.
Dunia nzima inahubiri amani na kwa watu wenye uelewa wanatambua kuwa kwa "hekima & busara za Edward Lowassa" leo Tanzania ina utulivu.
Amefisadi nini? Mahakama gani ya Tanzania ili mkuta Na hatia???Ni kweli, Lowassa angekuwa type yangu lazima ningekuwa fisadi papa!
duh, hebu rudi ukajifunze kuchangia maana naona unatokwa na povu bila sababu za msingi.Acha kudanganya watu wewe,
Lowasa na chadema wenzako waliitisha maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima,
Ila wananchi tu ndio walipuuza hilo agizo .
Hekima hekima wapi ,kenge Wa njano kabisa
Ndio zenu mkiambiwa ukweliduh, hebu rudi ukajifunze kuchangia maana naona unatokwa na povu bila sababu za msingi.
Hakuna ukweli uliouleta ukapingwa, cha kufanya lete vitu vya uhakika na siyo kuleta mipasho isiyo na kichwa wala miguu.Ndio zenu mkiambiwa ukweli
Kwa hiyo unakili kuwa kwa miaka kumi ,mbowe ,lisu, msigwa walikuwa wanaongea mipashoHakuna ukweli uliouleta ukapingwa, cha kufanya lete vitu vya uhakika na siyo kuleta mipasho isiyo na kichwa wala miguu.
Mimi ninaongelea Watanzania, wewe unaanza kuleta mifano ya mataifa mengine.
Hizi ndizo fikra kama za Lowassa kudhani amani ya Tanzania ilikuwa ndani ya mdomo wake. Nani amekuambia Watanzania ni kama Wasomalia, Wanaijeria, Wakenya au Wamisri?
Yeah, Siyo kosa kuota ndoto za alinacha.
Zanzibar kuna amani kwa sababu wananchi wengi wameamua kuishi kwa amani. Hakuna kiongozi yoyote aliyeshikilia amani ya Zanzibar.
Mambo ya busara unayafahamu wewe lakini ninachosema, Lowassa kusema amani ya Tanzania alikuwa ameitunza kwenye mdomo wake ni kuwafanya watanzania wengi kama nyumbu.
Amani ya Tanzania iko mikononi mwa Watanzania wengi. Ni lini amani ya Tanzania ilimilikiswa kwa Lowassa?
haya bwana naona ujinga wangu, ulipoishi ndipo akili zako zilipoanzia..Kwa hiyo unakili kuwa kwa miaka kumi ,mbowe ,lisu, msigwa walikuwa wanaongea mipasho
Amefisadi mali za Watanzania.Amefisadi nini? Mahakama gani ya Tanzania ili mkuta Na hatia???
Mkuu wewe hapa ndo umesema fisadi hebu defend hoja yakoAmefisadi mali za Watanzania.
Viongozi wakuu wa CHADEMA wanafahamu vizuri kuhusu ufisadi wake.
Mchango wako umeutoa vyema ... nawachukia wanaokurupuka na kuwatusi members wengine mara ..... hooo vile. Kama mtu anawaza tofauti na wewe hakuna haja ya kumtukana badala yake ni kumwelewesha ili aelewewe.Hata shetani anasikilizwa na watu zaidi ya Mungu!
Yes, Lowassa ni nabii kwa kutumia fikra za wapambe wake kama Gwajima na William Mwamalanga!
Nadhani huu ushauri ungeanzia kwanza kwa Edward Lowassa ambaye kwa sasa kila anapokutana na kundi la Watu anaanza kudai amani iliyokuwepo baada ya uchaguzi mkuu imetokana na yeye kukaa kimya baada ya uchaguzi.
vuvuzela wewe endelea kupulizaAmefisadi mali za Watanzania.
Viongozi wakuu wa CHADEMA wanafahamu vizuri kuhusu ufisadi wake.
Dah! Kiongozi, Yaani unavunja amri ya tisa hivi hivi bila ya chembe ya aibu!!mpuuzi wewe kama sio hekima za lowasa sasa hivi ungekuwa kweye kambi za wakimbizi kenya. Pangewaka moto hapa nchni
i
Bado unapambana naye tu.Dunia inatambua Lowassa ana utajiri wa kifikra kuhusu njia ya kuwa fisadi nchini Tanzania. Kinachoendelea kwa sasa kinadhihirisha Lowassa anahitaji huruma za kisiasa kutokana na mwenendo wake kisiasa. Anahitaji sana ushauri usio wa kinafiki kuhusu hatima yake kisiasa nchini.
Nilivyomsikia kwa mara ya kwanza akitoa madai kuwa ukimya wake baada ya Uchaguzi Mkuu umesababisha kuwepo amani nchini, nilidhani kinachomsumbua ni mihemko ya kisiasa.
Nilipomsikia pia kwa mara ya pili akitamka maneno hayo Mkoani Arusha wakati akishiriki katika kampeni za Uchaguzi wa Jimbo la Arusha ambao uliahirishwa katika siku ya Uchaguzi Mkuu baada ya kifo cha mgombea wa ACT-wazalendo Estomih Mallah sikushangaa sana.
Kilichonishangaza zaidi ni pale nilipomuona tena kwa mara ya tatu ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Usharika wa Monduli akisema kunyamaza kwake baada ya wananchi kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kumewafanya wananchi wasiuane. Eti anadai wananchi walikuwa wanasubiri neno lake ili waingie barabarani na kuanza kuuana.
Lowassa anataka kutuambia watanzania wengi ni kama nyumbu kwamba kila atakalolisema watalifuata au kulitenda. Anataka kutuambia watanzania wengi wanafanya mambo yao kwa kutegemea kauli zake. Anadhani yale aliyokuwa anayaita mahaba kwenye mikutano yake ni unyumbu.
Hawa watu wanaomshauri Lowassa waache kumdanganya. Kuna baadhi ya watu wanamjaza ujinga ili adhani ana hekima na busara zaidi ya Watanzania wengi.
Lowassa na wapambe wake hawafahamu kama watanzania wengi wana haiba ya kutopenda vurugu. Hafahamu kama kuna chaguzi kuu nne zimefanyika na Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani na kuheshimiana. Hafahamu utawala wa machifu uliokuwa na nguvu kubwa (powerful influence)katika jamii nchini ulipigwa marufuku na Tanzania ikaendelea kuwa na amani na kuheshimiana. Hafahamu tuna makabila zaidi ya 120 yenye imani za kidini tofauti lakini yanaishi katika msingi wa kuheshimiana na undugu.
Lowassa anataka kutufanya wajinga kama hatufahamu kuwa kitendo cha kuita waandishi wa habari na kujitangaza mshindi wa Urais halafu akaitaka NEC imtangaze ilikuwa ni dhamira ya ku-instigate violent lakini wananchi wengi walimpuuza.
Lowassa na wapambe wake wangetafuta kwanza uzoefu kuhusu haiba ya Watanzania kutoka wapinzani ambao wamekuwa katika uwanja wa upinzani kabla yeye hajawaza/kufikiria kama kuna siku atakuja kuwa mpinzani wa serikali ya CCM.
Kinachoonekana kwa sasa Lowassa yuko katika safari ya kisiasa ambayo Augustino Mrema amepitia! Lowassa has gone from hero to zero! As a politician, he is finished. There is no way back for him.
Ni nani anamshauri Edward Lowassa? Mwacheni akachunge ng'ombe wake Monduli!