Ni nani anayemdanganya Edward Lowassa?

Dunia inatambua Lowassa ana utajiri wa kifikra kuhusu njia ya kuwa fisadi nchini Tanzania. Kinachoendelea kwa sasa kinadhihirisha Lowassa anahitaji huruma za kisiasa kutokana na mwenendo wake kisiasa. Anahitaji sana ushauri usio wa kinafiki kuhusu hatima yake kisiasa nchini.

Nilivyomsikia kwa mara ya kwanza akitoa madai kuwa ukimya wake baada ya Uchaguzi Mkuu umesababisha kuwepo amani nchini, nilidhani kinachomsumbua ni mihemko ya kisiasa.

Nilipomsikia pia kwa mara ya pili akitamka maneno hayo Mkoani Arusha wakati akishiriki katika kampeni za Uchaguzi wa Jimbo la Arusha ambao uliahirishwa katika siku ya Uchaguzi Mkuu baada ya kifo cha mgombea wa ACT-wazalendo Estomih Mallah sikushangaa sana.

Kilichonishangaza zaidi ni pale nilipomuona tena kwa mara ya tatu ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Usharika wa Monduli akisema kunyamaza kwake baada ya wananchi kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kumewafanya wananchi wasiuane. Eti anadai wananchi walikuwa wanasubiri neno lake ili waingie barabarani na kuanza kuuana.

Lowassa anataka kutuambia watanzania wengi ni kama nyumbu kwamba kila atakalolisema watalifuata au kulitenda. Anataka kutuambia watanzania wengi wanafanya mambo yao kwa kutegemea kauli zake. Anadhani yale aliyokuwa anayaita mahaba kwenye mikutano yake ni unyumbu.

Hawa watu wanaomshauri Lowassa waache kumdanganya. Kuna baadhi ya watu wanamjaza ujinga ili adhani ana hekima na busara zaidi ya Watanzania wengi.

Lowassa na wapambe wake hawafahamu kama watanzania wengi wana haiba ya kutopenda vurugu. Hafahamu kama kuna chaguzi kuu nne zimefanyika na Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani na kuheshimiana. Hafahamu utawala wa machifu uliokuwa na nguvu kubwa (powerful influence)katika jamii nchini ulipigwa marufuku na Tanzania ikaendelea kuwa na amani na kuheshimiana. Hafahamu tuna makabila zaidi ya 120 yenye imani za kidini tofauti lakini yanaishi katika msingi wa kuheshimiana na undugu.

Lowassa anataka kutufanya wajinga kama hatufahamu kuwa kitendo cha kuita waandishi wa habari na kujitangaza mshindi wa Urais halafu akaitaka NEC imtangaze ilikuwa ni dhamira ya ku-instigate violent lakini wananchi wengi walimpuuza.

Lowassa na wapambe wake wangetafuta kwanza uzoefu kuhusu haiba ya Watanzania kutoka wapinzani ambao wamekuwa katika uwanja wa upinzani kabla yeye hajawaza/kufikiria kama kuna siku atakuja kuwa mpinzani wa serikali ya CCM.

Kinachoonekana kwa sasa Lowassa yuko katika safari ya kisiasa ambayo Augustino Mrema amepitia! Lowassa has gone from hero to zero! As a politician, he is finished. There is no way back for him.

Ni nani anamshauri Edward Lowassa? Mwacheni akachunge ng'ombe wake Monduli!
Unapambana na jitu lenye miraba minne na utaishia kuandika makala ndeeeeefu na kujibu kila comment hapa,mtu mzima anaendelea na mambo yake huku wewe ukionekana hamnazo kwa kupambana na wanao kuzidi kwa kila kitu.
 
Kama angekuwa ni jitu la miraba minne nadhani kwa sasa angekuwa Ikulu hasa ikichukuliwa amekuwa akifanya kila linalowezekana kuanzia mwaka 1992.

Politically, Lowassa is finished!
 
mpuuzi wewe kama sio hekima za lowasa sasa hivi ungekuwa kweye kambi za wakimbizi kenya. Pangewaka moto hapa nchni
i

huwezi kuwa mzima ww lazima uwe mwe*hu. Lowasa aliyetaka kuivuruga tanzania leo hii ajidai ndio kaleta amani na ww unashabikia??
 
Ukimsikiliza Lowassa kwa makini utagundua ni mtu ambaye kwa sasa anaishi kwenye fool's paradise!

Mzee mwanakijiji umesema ukweli kabisa lakini nadhani kishapata Ikulu katika mioyo ya baadhi ya wana JF ndiyo maana wanamtukana aliyeleta mada hapa wao wanatumia matusi kujibu hoja badala ya kutumia hoja kujibu hoja. Sijui hawa watu wamenyweshwa nini na huyu Lowasa ambaye mpaka April ama May mwaka jana walikua wanamtukana pia humu JF hao hao leo wanasema ni rais wa mioyo (Watanzania) sijui watanzania gani maana baadhi yetu tulimkataa kabla hajahama CCM sijui na sisi tunalazimishwa awe rais wa mioyo yetu??
 
Ameandika liwaya ina mwanzo mwisho aina, basi angetuwekea na ref tujue. Eti msema kweli sijui labda kwa watoto wako. Mbona ya Zanzibar hujaongea?
 
Ameandika liwaya ina mwanzo mwisho aina, basi angetuwekea na ref tujue. Eti msema kweli sijui labda kwa watoto wako. Mbona ya Zanzibar hujaongea?
Mbona wewe hujayaongea ya Zanzibar?

Zanzibar ni nchi yenye mipaka yake, Rais wake, Bunge lake, Mahakama zake na Jeshi lake!
 
Mzee mwanakijiji umesema ukweli kabisa lakini nadhani kishapata Ikulu katika mioyo ya baadhi ya wana JF ndiyo maana wanamtukana aliyeleta mada hapa wao wanatumia matusi kujibu hoja badala ya kutumia hoja kujibu hoja. Sijui hawa watu wamenyweshwa nini na huyu Lowasa ambaye mpaka April ama May mwaka jana walikua wanamtukana pia humu JF hao hao leo wanasema ni rais wa mioyo (Watanzania) sijui watanzania gani maana baadhi yetu tulimkataa kabla hajahama CCM sijui na sisi tunalazimishwa awe rais wa mioyo yetu??
Nadhani ume quote comment ambayo hukutarajia!

Mimi siyo Mzee mwanakijiji!

Hata hivyo hoja zako ni muhimu na valid.

Unapoona vijana wanadeki barabara lazima utajiuliza maswali mengi kama wana upeo mkubwa kifikra.
 
Uongo mwingine bwana uachefua huyo bwana msemajikweli inaonekana ana kituo chake binafsi cha habari anitajie tu kama jina lake alipojitangazia na kuamuru tume imtangaze ili nami na wengine wajiridhishe
 
Nadhani ume quote comment ambayo hukutarajia!

Mimi siyo Mzee mwanakijiji!

Hata hivyo hoja zako ni muhimu na valid.

Unapoona vijana wanadeki barabara lazima utajiuliza maswali mengi kama wana upeo mkubwa kifikra.

nliligundua hilo maana comment yangu ilikua inahusu majibu ya mzee mwanakijiji kaitka comment yako lakini nilipopost ilitokea ya kwako tu.
 
Back
Top Bottom