Katika mamia ya sheria nilizowahi kuzisoma hapa nchini Tanzania sijwahi kukutana na sheria inayomtaka Rais kuendeleza kile alichokianzisha mtangulizi wake, na badala yake nchi huwa ikiendeshwa kwa maono ya Rais aliyeoko madarakani.Tuna ushaidi kwa namna gani nchi imekuwa ikipoteza mamia ya pesa kutokana na kutokuwa na sheria kama hii.
Mfano wakati wa uongozi wa awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kuliibuliwa mamia ya miradi mikubwa na midogo na kabla ya kumaliza ukamilishaji wa miradi hiyo tarehe 17/03/2021 tukatangaziwa kuwa nchi imepoteza Rais kwa ugonjwa wa umeme wa moyo, watu wengi wakaingiwa na hofu ya kuwa je Rais anayekuwa anaweza kweli kumalizia ile miradi? na hii inakuja kutokana na kutokuwa na sheria, palekuwa miradi mikubwa kama Mwalimu Nyerere kule Rufiji, ufufuaji wa shirika la ndege kwa kununua ndege, mradi wa ujenzi wa reli ya treni ya kisasa n.k.
Nipende kumpongeza Raisi wa sasa kwa maono yake binafsi ya kuendeleza hii miradi ambayo ilitumia mamilioni ya pesa za ndani na mikopo kwani maono yake na uzalendo wake ndivyo vimemshinikiza kuendeleza kwani hakuna sheria inayomshikiza kuiendeleza.Imagine asingeendeleza tungekuwa tumepoteza mapesa mangapi?. Ni muda sasa kuletwa kwa sheria inayomtaka Raisi kuendeleza na kutekeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake.
''Sheria bora ndizo zinazo determine mustakabali wa nchi husika''
Pia soma
Hivi kuna Sheria inayolinda miradi iliyoanzishwa na Rais John Magufuli?