Ni mambo gani mazuri ya Kikwete tunayoweza kumshauri Magufuli kuyafuata na kuyaendeleza?

Watu wanalalamika kwa sababu walizoea mteremko. We fikiria serikalini na mashirika ya umma wamejaa vihiyo (watu wenye vyeti feki na hawajuwi nini wakifanyacho). Kila kukicha ukienda serikalini kutafuta huduma unakutana na hawa watu, a simple thing, wao wanashindwa kukusaidia wakati wameajiriwa kuhudumia wananchi (wewe na mimi). Kikwete alikuwa anawalimbikiza wakati people have been saying it for a long time kuwa tuna wafanyakazi wasio na taaluma, leo JPM anawatimua unafikiri watampenda JPM? Angalia walimu walio na vyeti feki na elimu wanaotoa kwa watoto wetu. Kikwete aliharibu sana Tanzania na inabidi ashitakiwe tu, hafai kabisa yule mtu.
 
Magufuli si mjinga kihivyo na ndiyo maana anapangua mambo yote katika utawala wa Kikwete kwani hayastahili kuigwa. Kikwete will go down as the most useless president Tanzania has ever had. Jiulize wewe mwenyewe: kipi kizuri alikifanya Kikwete katika utawala wake? Au hata kina Mkapa na Mwinyi, walifanya nini cha maana zaidi ya kuididimiza hii nchi? Nawaunga mkono wasomi wote wanaoshauri katiba ipitiwe upya ili viongozi walioboronga wafunguliwe mashitaka na kuhukumiwa kama nchi za wenzetu walioendelea ili iwe fundisho kwa viongozi wengine wakaokuja.
Naunga mkono, mimi huwa najiuliza hivi ugonjwa wa amnesia (kusahau) umewapata watu au nini?
 
Watu wanalalamika kwa sababu walizoea mteremko. We fikiria serikalini na mashirika ya umma wamejaa vihiyo (watu wenye vyeti feki na hawajuwi nini wakifanyacho). Kila kukicha ukienda serikalini kutafuta huduma unakutana na hawa watu, a simple thing, wao wanashindwa kukusaidia wakati wameajiriwa kuhudumia wananchi (wewe na mimi). Kikwete alikuwa anawalimbikiza wakati people have been saying it for a long time kuwa tuna wafanyakazi wasio na taaluma, leo JPM anawatimua unafikiri watampenda JPM? Angalia walimu walio na vyeti feki na elimu wanaotoa kwa watoto wetu. Kikwete aliharibu sana Tanzania na inabidi ashitakiwe tu, hafai kabisa yule mtu.
Well said. ..AMEN
 
Naunga mkono, mimi huwa najiuliza hivi ugonjwa wa amnesia (kusahau) umewapata watu au nini?

Siyo tu amnesia, watu wanahaha kwa sababu walizoeleshwa mteremko na JK, kwenda kunywa chai na kula maandazi ya nazi Magogoni kwao ilikuwa ishu. Hivi kweli mtu unauza utu wako kwa ajili ya maandazi ya bure na kucheza mchiriku viwanja vya Ikulu? Sawa utalishwa maandazi na uji wa ulezi bure, je huko kijijini kwenu nduguzo wamekula? Watanzania tubadilike jamani. Nyerere alionya Ikulu si pa kucheza, ni sehemu tukufu pale.....ndiyo maana majirani wanatucheka kwa ujinga.
 
Usiwe mpu.mbavu kihivyo. Jiulize tu kwa kina, as a president for 10 years ni nini cha maana alichofanya Kikwete? Nchi haiendelezwi kwa kuchekea wananchi na kuwadanganya kuwa nchi yao ni masikini wakati kila kukicha vitu vinagunduliwa hapa nchini ambavyo ni hadimu kupatikana duniani lakini bado anatafuta kisingizo tu ili aendelee kuiba na kunufaisha genge lake la majambazi. Hivi hata wewe mwenyewe huoni haibu kutetea uozo wa Kikwete kweli? Au mwenzetu unaandika umejificha chooni huku ukicheka kuona nitakujibuje? Kikwete was a useless president, mbona hata wenzake wanajuwa hivyo?
Huna haja ya kutukana kama unataka tujibizane kwa hoja.

Wewe tafuta Rais yeyote unaedhani unaweza kumlinganisha na Jakaya kwenye Nyanja ya

Shule
Miundombinu ya barabara na Umeme
Utawala wa Kidemokrasia
Mahusiano ya.kimataifa n.k
Mlete Rais unaedhani kafanya Mambo kumzidi Kikwete tujadili kwa ushahidi thabiti ila sipo tayari kwa kutukanana kama upo tayari kwa mjadala usio na matusi nakusubiri.
 
Utawala bora na wa kufuata sheria
JK ana mshinda Magufuli tena kwa mbali sana

Kuchagua cha kusema chenye hadhi ya kauli ya Rais
International relationship

Uvumilivu wa kisiasa!JK hakuruhusu polisi watishie watu kama tunavyo ona Dodoma now
 
  • Thanks
Reactions: mpk
Mwl Nyerere aliwahi kusema kwa miaka 26 madarakani alifanya mambo mengi mazuri na mengine ya kijinga na akaendelea kusema "Shida ninayoiona wanaacha mazuri na kuendeleza ya kijinga" Nadhani ni kauli ya mtu aliyejaa busara na ni msingi kwa viongozi waliofuata kama Mungu akiwajalia busara.

Kama watanzania bila kujali itikadi zetu tunajua Kikwete kuna vitu alifanya vizuri na kuna alivyofanya vibaya. Ni mazuri yapi tunamshauri Magufuli ayaendeleze? Nimeamua kuleta uzi huu baada ya rais wetu kusema jana anapata muda kupitia maoni yetu mitandaoni.

Mnajua msimamo na itikadi yangu lakini thread hii ni kwa faida ya taifa letu pendwa la Tanzania. Ningeomba tumshauri rais kufuata na kuendeleza mambo mazuri ya JK bila kufuata misimamo yetu kisiasa. KARIBU!
Unahoji kama nani? Kila zama na kitabu chake bwana, asome atakachona chamfaa aige kisichomfaa aache, full stop.
 
Siyo tu amnesia, watu wanahaha kwa sababu walizoeleshwa mteremko na JK, kwenda kunywa chai na kula maandazi ya nazi Magogoni kwao ilikuwa ishu. Hivi kweli mtu unauza utu wako kwa ajili ya maandazi ya bure na kucheza mchiriku viwanja vya Ikulu? Sawa utalishwa maandazi na uji wa ulezi bure, je huko kijijini kwenu nduguzo wamekula? Watanzania tubadilike jamani. Nyerere alionya Ikulu si pa kucheza, ni sehemu tukufu pale.....ndiyo maana majirani wanatucheka kwa ujinga.
well said ndugu yangu, heshima, hekima na busara lazima irudi katika nchi yetu TANZANIA....asante JPM, hakika umetoka kwa MOLA!
 
aache kubania ajira mpya. atuajiri tu maana metunyoosha vya kutosha kabisa. Mkuu Magu tafafhali tutazame na sie tuliosomeshwa kwa mbinde kwa pesa za kuuza mihogo na kunde. leo hii hadi tuliowaacha vyuo wanatukuta mtaani tunapigwa jua tu. Mkuu wetu tafadhali zingatia hili.

Hilo ndilo la maana sana. Naamini TRA watahitaji vijana zaidi ya 2,000 katika kuhakikisha kodi inakusanywa!
 
Utawala bora na wa kufuata sheria
JK ana mshinda Magufuli tena kwa mbali sana

Kuchagua cha kusema chenye hadhi ya kauli ya Rais
International relationship

Uvumilivu wa kisiasa!JK hakuruhusu polisi watishie watu kama tunavyo ona Dodoma now
Tunahitaji maoni ya kumshauri rais na siyo kumlinganisha
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema kwa miaka 26 madarakani alifanya mambo mengi mazuri na mengine ya kijinga na akaendelea kusema "Shida ninayoiona wanaacha mazuri na kuendeleza ya kijinga" Nadhani ni kauli ya mtu aliyejaa busara na ni msingi kwa viongozi waliofuata kama Mungu akiwajalia busara.

Kama watanzania bila kujali itikadi zetu tunajua Kikwete kuna vitu alifanya vizuri na kuna alivyofanya vibaya. Ni mazuri yapi tunamshauri Magufuli ayaendeleze? Nimeamua kuleta uzi huu baada ya rais wetu kusema jana anapata muda kupitia maoni yetu mitandaoni.

Mnajua msimamo na itikadi yangu lakini thread hii ni kwa faida ya taifa letu pendwa la Tanzania. Ningeomba tumshauri rais kufuata na kuendeleza mambo mazuri ya JK bila kufuata misimamo yetu kisiasa. KARIBU!
Asiwe anajibu kila kitu. kikwete alikuwa kimya kama hayupo. Watu watasema, wataponda, hadi kutukana wakati mwingine . Lakini hakuwa anawajibu yaani kama hajasikia. Hili litaepusha tofauti wa kauli kati ya raisi na watendaji wengine kama mawaziri n.k
 
Sina haja ya kuuliza watu kwani hata wasaidizi wake walimdharau, niulize ili iweje wakati ukweli uko hadharani? Kuuliza anauliza mtu asiyejuwa.
 
Huna haja ya kutukana kama unataka tujibizane kwa hoja.

Wewe tafuta Rais yeyote unaedhani unaweza kumlinganisha na Jakaya kwenye Nyanja ya

Shule
Miundombinu ya barabara na Umeme
Utawala wa Kidemokrasia
Mahusiano ya.kimataifa n.k
Mlete Rais unaedhani kafanya Mambo kumzidi Kikwete tujadili kwa ushahidi thabiti ila sipo tayari kwa kutukanana kama upo tayari kwa mjadala usio na matusi nakusubiri.

Rudi shule, eti utawala wa kidemokrasia.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwa miaka 26 madarakani alifanya mambo mengi mazuri na mengine ya kijinga na akaendelea kusema "Shida ninayoiona wanaacha mazuri na kuendeleza ya kijinga" Nadhani ni kauli ya mtu aliyejaa busara na ni msingi kwa viongozi waliofuata kama Mungu akiwajalia busara.

Kama watanzania bila kujali itikadi zetu tunajua Kikwete kuna vitu alifanya vizuri na kuna alivyofanya vibaya. Ni mazuri yapi tunamshauri Magufuli ayaendeleze? Nimeamua kuleta uzi huu baada ya rais wetu kusema jana anapata muda kupitia maoni yetu mitandaoni.

Mnajua msimamo na itikadi yangu lakini thread hii ni kwa faida ya taifa letu pendwa la Tanzania. Ningeomba tumshauri rais kufuata na kuendeleza mambo mazuri ya JK bila kufuata misimamo yetu kisiasa. KARIBU!

Yangu ni haya hapa:
1. Awe Raisi wa wote-tajiri, kundi la kati na masikini
2. Awe anawapongeza watumishi wa umaa -wengi wanafanya kazi nzuri mno
3. Awe na mtazamo wa kitaifa kwa ujumla wake-kidini, kikanda,kidemografia nk
4. Aimarishe ubia wenye manufaa na sekta binafsi-nchi zote zilizoendelea zimefanikiwa kwa msingi huu
5. Aweze kukasimu(delegate) hana sababu ya kujaribu kufanya kila kitu yeye mwenyewe
6. Awajengee imani wateule wake-wengi wanaonekana kujaa uoga na kutojiamini -tatizo ambalo linasababisha kukurupuka.
7. Akae mbali kidogo na wanaojiita 'manabii'- baadhi wanaweza kuwa 'manabii' wa uongo .Taifa linahitaji kuongozwa na katiba na sheria siyo utabiri wa 'manabii'.
8. Apunguze jazba-atabasamu zaidi kuepuka msongo
 
Uhuru wa habari na kujieleza, kukubali kukosolewa na asiwe mdini maana teuzi zinaonekana zinafanyika kwa jina la bwana tu!

Enzi za JK,haya yalitokea now tumeshasahau
1.Mwangosi aliuliwa na Polisi
2.Kubenea alimwagiwa tindikali
3.Dr Mvungi aliuliwa,Kubanda akavamiwa
4.Magazeti ya Mwanahalisi,East Africa yalifungiwa
5.Dr Ulimboka alikamatwa na kuteswa

6.Chadema walipigwa Arusha
7.Mtikila alikamatwa mara nyingi
 
mkuu habari ya huko karatu?

Tuko poa ila tumemiss Dr Slaa. Tumemkubali rais JPM na tunaomba amwite Dr wetu na kumpa kazi kama alivyompa mzee Mrema. Atamsaidia sana katika vita dhidi ya mafisadi na wafujaji wa mali za umma.
 
Teuzi zake hazina sura ya Kitaifa, Waislamu ni wachache sana katika teuzi zake, hii inaleta taswira mbaya na kujikuta anaangaliwa kwa jicho baya.
Ajitahidi kuweka balance kwa kuchukua watu wenye sifa kutoka makundi yote ya kijamii
 
Back
Top Bottom