KERO Ni lini Daraja la Milala Shongo lililopo Manispaa ya Mpanda litajengwa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,870
6,807
photo_2025-04-22_11-24-31.jpg

Daraja la Milala Shongo lililopo Kijiji cha Milala, Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi ni tatizo sana kwetu Wananchi wa Milala.

Sisi wakazi wa Milala tatizo hili limetuchosha kwa sababu limedumu kwa muda muda mrefu sana na kuwa kikwazo cha mawasiliano na kufanya shughuli zetu za kiuchumi.

Wanawake ni Wahanga wa kushindwa kuvuka hususani wanapokwenda kutafuta huduma za afya na kujifungua katika Zahanati yetu ya Milala hasa pale mvua ikiwa imenyesha hujaa maji mengi na kukata mawasiliano.

Nikiwa Mkazi wa Kijiji cha Milala, kwa kipindi fulani niliwahi kuona daraja hilo ujenzi wake ukifanyika lakini ghafla hatukuona ujenzi ukiendelea.

Nawaomba wahusika jengeni daraja kuondoa hali hii mbaya.
 
Hiyo njia inahitaji hela ndefu kujenga Madaja hayo matatu japo nina muda sijaitumia ila ni ya muhimu,kwanza kwa mtemi beda hapo panahitaji dalaja ,kuna kamto kutoka shule ya msingi hadi parokiani na baada ya hapo ndo hilo dalaja kuvuka kwenda mabanini na kwenda kasokola hivyo wanaona ni gharama kubwa sana
 
Mama anaupiga mwingi! Msituchoshe na nyimbo za madaraja miaka yote 60 na kitu ya uhuru, Kwa sasa ni NO REFORMS, NO ELECTION!
 
Mama anaupiga mwingi! Msituchoshe na nyimbo za madaraja miaka yote 60 na kitu ya uhuru, Kwa sasa ni NO REFORMS, NO ELECTION!
Bora umewapasha. Madaraja madaraja na magari ya kupita hata hawana.
Mbona mababu zenu walipita daraja hilo hilo miaka hiyo na hawakulalamika?
Mkiona vipi, tengenezeni wenyewe. Hatuna pesa ya mchezo.
 
Back
Top Bottom