JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,868
- 6,807
Daraja la Milala Shongo lililopo Kijiji cha Milala, Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi ni tatizo sana kwetu Wananchi wa Milala.
Sisi wakazi wa Milala tatizo hili limetuchosha kwa sababu limedumu kwa muda muda mrefu sana na kuwa kikwazo cha mawasiliano na kufanya shughuli zetu za kiuchumi.
Wanawake ni Wahanga wa kushindwa kuvuka hususani wanapokwenda kutafuta huduma za afya na kujifungua katika Zahanati yetu ya Milala hasa pale mvua ikiwa imenyesha hujaa maji mengi na kukata mawasiliano.
Nikiwa Mkazi wa Kijiji cha Milala, kwa kipindi fulani niliwahi kuona daraja hilo ujenzi wake ukifanyika lakini ghafla hatukuona ujenzi ukiendelea.
Nawaomba wahusika jengeni daraja kuondoa hali hii mbaya.