MENEMENE TEKERI NA PERESI
JF-Expert Member
- Mar 11, 2022
- 5,012
- 13,613
Mh labda miaka hiyo ,Tanzania ya leo na machawa wa leo uwe na pesa uandae sherehe eti watu wagome kuja hata kinafiki lengo wapate cha kusimulia ?Ila ujue maisha ni kama meza inayozunguka!! Ni vizuri ukalijua hilo. Na watu hutawahitaji kwenye harusi tu, maisha yana mambo mengi yatakayokutaka watu wakusaidie na si lazima iwe fedha!! Hata kama una pesa nyingi, kuna wakati hizo pesa haziwezi kuwa ,mbadala wa watu!!
Kuna jamaa alikuwa ana pesa nyingi tu kwa hiyo yeye akasema mimi sitachangia shughuli za watu. Ikifika zamu yangu sitachangisha pia pesa kwa watu lakini NITAWAALIKA WOTE bila kuhitaji wanichanmgie kwanza!! Kilichotokea jamaa akaandaa shughuli yake vizuri, akaalika watu, lakini utafikirio watu wameambiana!! hawakuhudhuria!! hata ndugu zake pia walimtosa maana yeye alikuwa hawachangii pia!! Sherehe ikadoda!! machokoraa wakaingia kula msosi, picha za sherehe ya harusi zikaharibika!! ukumbi mweupeee!!!!
Badala ya kuwa ni siku ya furaha ikawa ni siku ya huzuni kwake!! Pesa zake hazikuweza kumshangilia!! Laiti angejua mwanzoni labda angekodi watu wa kumshangilia!!
Nop haitokei kwasasa , kikubwa tutafute hela na harusi na masherehe wakati wa kuoana ni mwanzo wa kukaribisha wachawi kwenye ndoa ndiyo maana hazidumu .
Mimi na wangu tumepanga kubebana kama gunia la mkaa , tukishindwana ni kimya kimya kila mtu aone ustaarabu wake hatuwaambii watu siri zetu