Ni lazima kumchangia mtu send-off ama harusi?

Sio lazima na sio muhimu.

Kuna CHUDDA mmoja nilimuomba~ga maQu pale Muleba akaninyima nikapozi ,siku kadhaa mbele akanikuta na rafiki yake wa karibu tumekaa sehemu tunapata menu. Huku na kule akagundua nimetoka kumto****ba rafiki yake ...... Alinuna hatari.

Miaka mitatu mbeleni ananipigia simu ananiomba nimchangie sendoff yake anaolewa.

Sikumchangia chochote, akakasirika sana. Ndoa yake ilidumu mwaka mmoja ikafa. Eti anakuja kuanza kujirahisi rahisi anataka tufufue mtongozo aliokuwa ameugomea kipindi kileeee yupo Tyr kunivulia chuppi, nikamwambia hapana hapana hapana.

Anayeoa na anayeolewa wagharamie sherehe yao vinginevyo wakimalizana kwenye nyumba ya ibada kila mmoja ashike njia yake mambo yaishie pale, sio kutaka sherehe kubwa ya gharama kwa kutegemea michango toka kwa watu wengine.
 
Kwani wanakulazimisha kuchanga? Ukipenda toa, la huna nafasi waambie wazi kuwa kwa sasa huna nafasi hiyo.
Nyie si ndo mnalazimisha watu wawatoleee michango na mnashindwa kujipanga Kwa mambo yenu. Mwisho mnaanza kusema watu hawawasaidii. Huenda hata hivo watu wanakusaidia kwenye michango hii sababu ya kukuonea huruma tuu.
 
Na mara nyingi harusi zisizo gharama kubwa zinadumu kuliko za gharama kubwa
 
Mie sichangii harusi au sherehe yoyote full stop!
Ila ujue maisha ni kama meza inayozunguka!! Ni vizuri ukalijua hilo. Na watu hutawahitaji kwenye harusi tu, maisha yana mambo mengi yatakayokutaka watu wakusaidie na si lazima iwe fedha!! Hata kama una pesa nyingi, kuna wakati hizo pesa haziwezi kuwa ,mbadala wa watu!!

Kuna jamaa alikuwa ana pesa nyingi tu kwa hiyo yeye akasema mimi sitachangia shughuli za watu. Ikifika zamu yangu sitachangisha pia pesa kwa watu lakini NITAWAALIKA WOTE bila kuhitaji wanichanmgie kwanza!! Kilichotokea jamaa akaandaa shughuli yake vizuri, akaalika watu, lakini utafikirio watu wameambiana!! hawakuhudhuria!! hata ndugu zake pia walimtosa maana yeye alikuwa hawachangii pia!! Sherehe ikadoda!! machokoraa wakaingia kula msosi, picha za sherehe ya harusi zikaharibika!! ukumbi mweupeee!!!!

Badala ya kuwa ni siku ya furaha ikawa ni siku ya huzuni kwake!! Pesa zake hazikuweza kumshangilia!! Laiti angejua mwanzoni labda angekodi watu wa kumshangilia!!
 
Nyie si ndo mnalazimisha watu wawatoleee michango na mnashindwa kujipanga Kwa mambo yenu. Mwisho mnaanza kusema watu hawawasaidii. Huenda hata hivo watu wanakusaidia kwenye michango hii sababu ya kukuonea huruma tuu.
Hayo ni mawazo dhaifu!! Mchango haujawahi kuwa wa lazima, na mtu hapaswi kujihisi vibaya kama ameshindwa kuchangia na pia mtu hapaswi kukasirika usipomchangia!! Kwa wengi tatizo siyo roho mbaya bali tatizo ni ukata!! mtu analaumu kuombwa mchango wa harusi kwa ajili ya ukata!! huo ndio ukweli!!
 
Siyo lazima lakini mpaka mtu amekuomba umuunge mkono kwenye jambo lake tafsiri yake ni kuwa amekutambua na amekupa heshima, najua wengi mtapuuza lakini kimsingi tunawiwa kushiriki katika furaha na huzuni za watu wetu wa karibu kwa namna moja ama nyingine. Tusijitenge hata kamawewe hutohitaji support yao hapo baadae kwani maisha ni hayahaya
 
Unateseka sana.
Kanuni yangu nakusalimia mara 3 kuhakiki kama kweli umeamua...baada ya hapo usubirie tukasuhuhishwe na Musa huko alikotangulia...akinisalimia nitamwangalia...natabasamu napita.

Acha kushika simu kiungo...wewe tabasamu tu unapita au anapita.

Nitakutesa kwa furahq na raha zangu😂😂😂
 
Jitahidi kama wewe ni Mkristo uwe unahudhuria kwenye ibada ya Misa ya ndoa kanisani na kama ni muislamu jitahidi kufika msikitini au Nyumbani kwa bibi harusi inapofungwa ndoa, mambo ya sherehe waachie wengine.

Hii itakuondolea lawama kwamba aushiriki matukio ya kijamii, lakini ukiwa shuhuda kanisani au msikitini wewe ni zaidi ya hao waliochanga pesa ili wakalewe pombe na viongozi wa Kamati kujipigia pesa za michango kupitia kandarasi za mapambo, chakula na vinywaji.
 
maQu🤣🤣😂
 
“Binadamu”

Nilikuwa mtoaji mzuri sana, utoaji wangu ulikuwa laki 1 haipungui wala sichangi zaidi ya hiyo. Lakini wale watu unaowachangia wakishamaliza jambo lao wala hawana habari na wewe. Nikaona isiwe shida.

Kwa sasa nachanga kwa ndugu zangu tu, tena wale wa karibu sana. Naunganishwa kwenye groups napledge nakaa kimya mpaka group linavunjwa.
 
Kuhudhuria ndoa ya mtu tena mchana kwangu hapana, ni rahisi kuchanga kuliko kwenda kuhudhuria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…