Chakorii
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 18,733
- 51,278
Habari jamani, mnaendeleaje? Hebu acha niende moja kwa moja kwenye hoja.
Iko hivi, miezi kama miwili au mitatu katika kupiga stori za hapa na pale one of my colleagues (KE) akaniambia unajua fulani anaolewa na fulani (wote wanafanya kazi pamoja)? Nilifurahi kwa mshangao maana sikuwahi kujua kama walikuwa wako na mahusian, so stori ikaishia hapo tukaendelea na habari za maisha mengine.
Sıjakaa sawa ilibaki kama wiki mbili au tatu akafunge ndoa ndio akaja kuniambia Chakorii nafunga ndoa na fulani, naomba support yako. Nikamjibu kwakuwa muda uliobaki ni mfupi na hili swala lako limekuja kwa haraka, sina uhakika asılımia mia kama nitaweza kuku support, akasema sawa.
Kiukweli majukumu yalinizidi nikamsahau kabisa! Yooo, nakuja kuonana nae tena ni baada ya likizo, sasa sijui ndio alitoka kufunga ndoa ama alikuwa likizo kawaida maana sikuona kiashiria chochote cha kuwa huyu mtu alikuwa kwenye hekaheka.
Kilichonifanya nikaleta uzi sasa, heee si kaninunia huyo mwanadada, hata nikimsaliamia haitiki! Nikasema labda pengine amevurugwa akili. Siku nyingine tena nikamsalimia kaitika kama kalazimishwa, mind u mimi ndie huwa namuanzaga.
Sasa juzi kaja sehemu ambapo mimi ndie muhusika, hakunisalimia tena nikamuuliza “My love mimi na wewe tuna matatizo?” Akanijibu hapana mambo ni mengi tu, nikajisemea ahhaa mambo mengi ee, nikamtukana kimoyo moyo, wewe siku ukiisikia salam yangu uniite dog ingawa mimi sio dog!
Sasa kila nikimuona yulee nainyanyua simu najifanya naongea na mtu kwa simu. Akili imemkaa sawa anataka kunisalimia lakini ninaongea na simu, nimeshamfungia vioo na si mfungulii tena.
Ni lazima kuchanga kwenye vitu vya umuhimu ambavyo vinakuja bila taarifa. Harusi ama send-off ni swala la kuvuta pumzi na kujipanga, sio lazima kusumbua watu wakuchangie.
Hallelujah 🤸♀️