The Philadelphia finest
JF-Expert Member
- Sep 19, 2023
- 453
- 1,123
Naandika andiko hili nikiwa na uchungu sana na hili jambo.Awali hili kundi lilianza kimasihara tu kama vijana wanaojihusisha na uchezaji wa kamari wao kwa wao.Pengine baada ya kuona malengo yao hayafanikiwa wakabadili mtindo wa utafutaji wakaingia kwenye biashara ya kuuza dhahabu feki.Hili liliambatana na uharibifu wa mifumo/miundombinu ya maji kwa kuiba koki za mabomba ya maji kwa ajili ya kuziyeyusha na kutengeneza hizo product za dhahabu feki.
Hili la uuzaji dhahabu feki japo wanaendelea nalo ila sasa kero iliyo kubwa ni kuanzia kukaba na kumyang'anya mpita njia mali zake zikiwemo fedha,simu na vitu vya thamani anapoonyesha kutoafikiana nao dili ya kuuziana.Pili kama ni Binti huanza kwa kumzunguka na kumnyang'anya pesa zake au simu waziwazi kisha huishia kukimbia na kujificha kwa masaa kadhaa kabla ya kurudi tena baadae hali ikitulia.Mambo haya hufanyika kuanzia asubuhi,mchana na usiku.Baadhi Polisi wanalifahamu hili kundi kwa 100% ila ndio hivyo penye uzia penyeza rupia!
Viongozi wa serikali za mtaa hasa posta na Nyerere maeneo ambayo ni makao makuu ya hao wahalifu wanahangaika usiku na mchana kupambana na hili genge ila mwisho wamekata tamaa.Sababu wahalifu hao wamekuwa wakitamba kuwa na budget ya kuwapa askari na mgambo wasio waaminifu rushwa ili wasipate vikwazo kwenye uhalifu wao.Na hili la baadhi askari kupewa rushwa lipo!
Wito kwa viongozi wa ngazi za juu kuanzia RC Mara, DC Bunda,RPC MARA,OCD Bunda
Msikubali mchafuliwe sifa na askari wachache wenye tamaa.Maana haiingii akilini vijana wanapora mchana kweupe,Kisha kukodi mapikipiki na kuendesha kwa Fujo Barabara kwa pesa za uhalifu bila hofu.Hii ni dharau kwa vyombo vyombo usalama!Kama nilivyotangulia kusema waathirika wakubwa ni watoto,mabinti/kinamama na wanafunzi.Tuna jukumu la kuwalinda na hili genge ambalo linaundwa na vijana wapatao 200+.
Pia nashauri askari waliokaa muda mrefu wahamishwe maana tayari wanaishi maisha ya kishikaji sana na hawa wahalifu.Hawa wengi wao ni maaskari yunifomu tu ila ethics hakuna.
Maeneo ya kuwapata hawa vibaka
1.Eneo la nyuma linalozunguka uwanja wa michezo wa sabasaba.Hapa kuna jengo ambalo halijakamilika lililotazamana na Barabara ya kutoka kanisa la adventista,Bunda mjini.Pembeni mwa jengo hili hulitumia kucheza kamari na kuvutia bangi
2.Kijiwe maarufu kinachoitwa kwa Mama D mtaa wa posta(Hapa nasikia hapagusiki wala kuingilika !!)
3.Eneo la uswahilini (ukerewe road) huku ndio makazi ya wahalifu walio wengi na licha ya kuwa ndipo makao makuu ila wengi wao wamezaliwa huku.Nashauri operation ikipita huku ndipo nguvu kubwa iwekwe.Narudia nguvu kubwa iwekwe.Nasema hivi maana nyakati za usiku vijana hawa hutanda Barabara ya ukerewe wakiwa na mapanga na huyatumia kutisha raia na kuyanoa barabarani.Hii hutisha wapita njia na watumiaji wa vyombo vya moto.Hili eneo ni hatari sana.Navililia vyombo vya ulinzi na usalama kuwekeza nguvu zaidi hapa.
4.Baa ya Kamani
Nayaanika wazi maovu yote ya hili kundi
.1.Kukaba na kupora hasa watoto,kinamama,wanafunzi ,wazee nk
2.Kutapeli watu kwa kuwauzia dhahabu feki
3.Kuharibu miundombinu ya maji hasa koki za mabomba
4.Kudhalilisha wasichana/wanawake kwa kuwabaka
5.Kero za kelele hasa nyakati za jioni na usiku wa manane.
6.Kuhatarisha maisha ya wananchi kutokana na kuendesha pikipiki kwa Fujo barabarani
7.Kuvuta bangi hadharani
8.Kuongeza taharuki kwa wananchi
9.Kutishia maisha kwa wale wanaoonekana kuwa kikwazo kwako
10.Kupiga na kujeruhi
Vijana hawa wanashirikiana pia na baadhi ya bodaboda wasio waaminifu katika kufanikisha matukio yao ya kihalifu. Baadhi ya bodaboda hao ni kijana mmoja ajulikae kwa jina la Tanrod(kituo anachopaki hakijajulikana) na wengine wengi tu.Mwingine anajulikana kwa jina la samwel anayepaki maeneo ya Karibu na baa ya Boma,ukerewe road.(Maeneo ya Karibu na kwa mama Nyangeta).Pia Kuna haja ya kuchunguza vijiwe vya bodaboda maana wengi wao ni wahalifu hasa nyakati za usiku ambapo hupora simu na kukimbia.
Ukweli ulio wazi
Hapajawa na mipango thabiti ya kupambana na hawa wahalifu.Sababu nimezieleza hapo juu.Lakini pia kitendo cha vijana hawa kufanya uhalifu hadharani na kutamba wazi ni dharau na matusi kwa jeshi la Polisi.Mbaya zaidi kundi hili linazidi kukua siku hadi siku na kuvutia vijana wengi kujiunga nalo.Wapo waliositisha masomo ili kulitumikia na pia wapi walioacha kazi zao halali mfano bodaboda ili kulitumikia.Kushindwa kulidhibiti hili kundi inaweza pelekea wananchi kukosa Imani na jeshi na mwisho wa siku ni kujichukulia Sheria mkononi.Bado wito wangu kwa POLISI,kamateni hawa vijana,wanafahamika vizuri.Mkiendesha msako mkali serious mna nafasi ya kuibadili historia ya bunda,mtakumbukwa vizazi na vizazi kwa kuifanya bunda kuwa sehemu salama na tulivu.
RC-MARA,DC-BUNDA,RPC-MARA na OCD BUNDA
Chondechonde wakuu mkiona kuna ulazima wa nyie kulivalia njuga hili fanyeni hivi bila kupepesa macho hali ni mbaya.Ila mkazo wenu uwe zone ya uswahilini huko ndiko Kuna basement ya hili kundi japo lina coordinate pia na vikundi kutoka Nyasura nk
Mungu awabariki
Tuna jukumu la kuilinda Bunda,tutokomeze hawa vibaka na wahalifu ili tulinde ustawi wa mji wetu
UPDATE
Kuna askari wapatao wawili ambao ni wanufaika msivyo na maadili ya kazi mmekutana na baadhi ya wahalifu na kuapa kumtafuta mtoaji wa taarifa hizi.Tunakusanya taarifa za ushahidi zaidi ili tuzifikishe ngazi husika muweze kuchukuliwa hatua stahiki.Majina yenu tunayo.