Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 26,003
- 19,064
Ndugu zangu Watanzania,
Ikiwa tutaacha Taifa likajenga utamaduni wa watu wakatumia mitandao ya kijamii kuchafua viongozi wetu,kuwapaka matope, kuwadhalilisha, kuwatukana matusi bila kuchukuliwa hatua wala kukamatwa ili watoe ushahidi tutakuwa tunariharibu Taifa letu.tutakuwa tunaharibu maadili na utamaduni mzima wa kuheshimiana na kukosoana kwa staha.
Imeshakuwa kero sana kwetu wananchi kuona mara nyingi sana Mdude Nyagali akitumia mitandao ya kijamii kumtolea RAIS wetu lugha za matusi, kumdhalilisha ,pamoja na kumhusisha ,kumzushia tuhuma za uongo, uchonganishi na zenye lengo la kumchafua pasipo ushahidi wa aina yoyote ile.
Amekuwa akifanya hivyo mara nyingi sana.na kitendo cha kukaliwa kimya pasipo kuchukuliwa hatua za kukamatwa,kuhojiwa,kufikishwa mahakamani kumemfanya ajione yupo juu ya sheria,kujiona anaogopwa ,kujiona yeye anaweza kufanya lolote,kusema chochote, kumtukana yeyote, kumdhalilisha yeyote,kumvunjia heshima yeyote,kumzushia yeyote pasipo kuchukuliwa hatua wala kukamatwa wala kuhojiwa wala kukemewa.
Imefanya watu wabaki wanashangaa inakuwaje mtu huyu anayefanya kazi ya kumchafua Mheshimiwa Rais kila siku anaachwa bila kuchukuliwa hatua? Watu wanashangaa kwanini anafumbiwa macho muda wote? Wahusika mnasubiri mtu huyu aropoke au aseme nini au amchafue vipi na kwa kiasi gani Rais wetu ndipo mumchukulie Hatua? Je sheria zinatumika kwa baadhi ya watu na kufungwa pingu kwa wengine kutokutumika?
Kwanini hamumkamati na kumhoji ili atoe ushahidi wa tuhuma anazozitoa? Yeye ni nani katika Taifa hili? Hii haikubaliki wala kuvumilika kuona akimchafua Rais wetu Pasipo kuchukuliwa hatua kali za kisheria. ni lazima tufahamu ya kuwa hakuna uhuru usio na mipaka,hakuna uhuru au demokrasia kwa ajili ya kutukana , kudhalilisha,kuwashushia heshima wengine pamoja na kuwapaka matope wengine. Uhuru una kwenda sambamba na wajibu wa kuzingatia haki za watu wengine .
Soma Pia: Mdude Chadema: Hotuba ya Rais Samia jana ni hotuba mbovu zaidi kuwahi kutokea Tanzania
Huwezi ukawa unachafua watu wengine halafu ukasema ni demokrasia au uhuru.uhuru na demokrasia ina mipaka yake. Nawakumbusheni ya kuwa Mbali ya kuwa RAIS Samia ni Mama mwenye watoto, wajukuu lakini kubwa ni kuwa Ni Rais wetu ,ni kiongozi wetu tunaye muangalia na anayegusa Maisha yetu moja kwa moja. Kwa hiyo hatufurahishwi wala kupendezwa kuona Rais wetu akichafuliwa na mtu au kuzushiwa mambo yasiyo na ushahidi wa aina yoyote ile.hii haikubaliki hata kidogo.
Ni lazima tabia hii mbaya na chafu inayofanywa na watu aina ya Mdude Nyagali waliokosa adabu na staha tuipinge,kuikemea ,kuishambulia na kuikataa kabisa hapa Nchini.ni lazima tuseme tunataka uhuru na demokrasia lakini siyo uhuru wa kuwatusi na kuwachafua wengine bila ushahidi wa aina yoyote ile.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.