Mshobaa
JF-Expert Member
- Apr 7, 2013
- 1,713
- 675
Wakuu salaam,
Nadhani sasa ifike mahali sisi wananchi tuache kudanganywa kwa ahadi hewa. Tumesha kuwa watu wazima sasa, sio watoto.
Huu mradi sote tulishuhudia utiaji saini wake na Mh. Mchengerwa mwaka jana, mwezi Oktoba, na kuahidi utekelezaji wake ufanyike mara moja.
Naomba kuuliza, ni kitu gani kinakwamisha huu mradi wa kimkakati kabisa ambao fedha zake tumeshuhudia Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba akitia saini ya makabidhiano kuonyesha fedha zishapokelewa?
Je, viongozi ni kwa vile hawaishi sehemu ambazo miradi hii inapita ndio maana ukimya umetawala?
Mfano wa barabara ambazo tumeambiwa zitatengenezwa ni pamoja na ile ya Mpigi-Magoe pamoja na daraja lake lililoharibiwa na mvua za El Nino tangu mwezi Machi mwaka jana.
Kuna hii ya Msumi, kuna Goba-Korea na nyinginezo ambazo zipo katika Manispaa ya Ubungo.
Naomba serikali yetu sikivu iangalie umuhimu wa hizi barabara maana zinasababisha kero kubwa kutokana na ubovu wake.
Hii ndio inachangia ugumu wa maisha kwa sababu gharama ya usafiri kwa maeneo tajwa ni ghali pengine kuliko sehemu nyingine yoyote.
Sehemu ya kilomita 5 nauli huanzia TSh 1000 hadi 2000, ambapo njia zingekua nzuri gharama zingepungua.
Nawaomba TARURA kama wapo humu JF waje watupe majibu ni nini kinaendelea.
Nashukuru!