RICHSON JONAS
Member
- Oct 25, 2016
- 25
- 2
Sio siri huu ni ushambaMtu makini mara nyingi anapotaka kufanya uhuni hutumia akili nyingi sana kufanya uhuni wake,hutafakari kwa kina akishirikisha akili yake na ujanja wake afanyeje uhuni wake ufanikiwe na bado abaki salama bila kujulikana.
Mfano mzuri ni maofisini,kutokana na uwepo wa ufuatiliaji wa matumizi ya fedha,wapigaji makini hupiga kwa kutumia akili na ili ugundue ni lazima pia uwe na akili nyingi na ujanja wa kiwango chao.
Nimekuwa nikitafakari uhuni uliofanywa na RC Makonda toka kipindi anatangaza list ya wauza madawa,ni dhahiri kabisa Makonda Paul sio kwamba ni mshamba wa kiwango cha juu tu,Bali shule yake haijamsaidia. "Mhuni" hawezi kufanya uhuni akajianika wazi namna ile. Ndio maana kina Mange Kimambi wanamuokota mchana kweupe na kumuanika kwa sababu sio intelligent
Nitatoa mifano. Hapa ni town Dar,unapotaka kufanya uhuni tumia akili sana ukitumia uhuni wa kijijini inakuwa unawapa mzigo wanaokubeba
1.Kuwa mbwatukaji na unatumia cheti cha mtu.
Watu wengi tu wanatumia vyeti vya wengine. Kwa mtu aliyekuwa kafika rank ya Makonda alitakiwa kukumbuka hili na kuwa makini zaidi kwa sababu jambo hili lisingeweza kuwa siri. Ni kitu cha ajabu sana wewe umechafuka kiasi kile unaopata wapi ujasiri wa kuwa-attach wengine. Tena ingekuwa mtu makini asingekubali cheo kile unless hata angeomba awe RC wa Geita huko ambako hakuna mbilingembilinge.
2.Kumtumia "insane" kumchafua Gwajima.
Makonda hakutumia akili kabisa katika kumtumia yule dada kutaka kumchafua Gwajizzo. Na ndio maana hata dili ikabumburuka kabla hata haijaruka hewani. Ukitazama cheti cha hospitali utaliona hili,tena alivyomshamba amekiandika kile cheti mwenyewe,halafu akaingia front mwenyewe kulazimisha "kipindi chake" kichezwe. Huu ni ushamba.
3.Kuvamia ofisi za Clouds akiamini hatajulikana. Hivi hakuweza kufikiria hata kama kuna CCTV mle? Ni bora hata angewatuma watu wamfanyie kazi. Halafu anawatisha watu kwamba watafungwa miaka sita bila kwenda mahakamani,huu ni ushamba wa kiwango cha lami.
Nimesoma kwamba Makonda aliwaaonya wasitoe taarifa kwamba amefamia kituo. Huu ni ushamba, unawezaje kuwaziba midomo watu wale.
4.Kumuwekea loud speaker Mh.Rais
Mara kadhaa Makonda ameonekana kuongea na Rais akiwa kuweka loud speaker ili kuwaonesha watu yeye ni nani. Huu ni ushamba,"wahuni" hatuhitaji ujiko wala kutaka watu wajue sie ni kina nani. Kwa mtu wa namna ile hata kumuamini ni ngumu kwa sababu ni dhahiri hawezi kutunza siri
Hakuna ubishi kwamba mtu kama RC wa jiji kubwa ni lazima kunakuwa na siri kadhaa na Rais iwe za nia mzuri ana mbaya. Ndio maana hata wazushi wanazusha kwamba pengine Rais anaogopa kumtumbua Makonda kwa kuhofia kuvuja kwa siri maana hata yeye anajua kijana wake ni waruwaru
5.Kuweka plate namba ya RC kwenye gari binafsi
Huu ni ushamba wa madaraka. Na sio ethical kabisa,yaani ofisi yote ya RAS umekosa magari mazuri ya kutumia mpaka unaweka plate namba ya heshima kwenye gari binafsi?
Kwa hiyo uteuzi wa RC Makonda eidha haukuzingatia upekuzi au haikufanyika kwa kina. Kwa sababu kama upekuzi ungefanyika,kwa kuzingatia tu rekodi zake za chuo Makonda asingependekzwa kuwa RC Dar. Hata record za chuo tu kwa namna alivyokuwa akifeli ni ushahidi tosha kwamba mtu huyu anauwezo mdogo wa kufikiria kwa hiyo kumpa jiji kubwa kama Dar ingekuwa kumpa mzigo. Ni busara angepewa size yake