Ni dawa gani ya usingizi wanayoitumia wezi kupuliza madirishani?

Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,857
1,538
Salaam JF.

Nilikuwa naomba uzoefu wenu wanaJF, hasa katika hizi dawa wa wanazotumia wezi kuwaibia raia wema kuwapulizia madirishani wakati wa usiku wanapolala.

Kwanza nilikuwa nataka kufahamu jina lake, na pili wapi wanapozipata lengo si kwa ajili ya matumizi binafsi lengo ni kufahamu.

Sababu: Wizi wa kuvunjiwa milango na madirisha umekithiri kibaya zaidi wezi wanathubutu kuwaibia walala hoi hadi maafisa wa serikali wenye silaha. Juzi kati Mh. Fulani ambaye ana cheo kikubwa tu serikalini alipigwa vitu vyake vyote sebuleni na mwingine kasafishwa sebule yote na watoto wa mjini, akiwemo pia mwanajeshi mstaafu naye alivunjiwa nyumba na wezi kusafisha sebule lakini kabla ya kuiba wezi walikunywa chai iliyokuwa sebuleni na kuondoka.

Inavyoonesha, hii dawa inawapa kiburi sana, usishangae hadi usalama huwa wanapigwa.
-----------

Kwa mujibu wa makala ya uchambuzi ya Fikrapevu.com

Je, unaifahamu Dawa ya usingizi inayotumiwa na wezi kuwapulizia watu kabla ya kuiba? Inaitwa Chloroform.

Kwa muda mrefu kumekithiri vitendo vya uhalifu unaohusisha wezi kuingia kwenye nyumba za watu nyakati za usiku na kuwapulizia dawa ya usingizi na kisha kuchukua chochote wanachokitaka ndani ya nyumba.

Baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha aina hiyo ya uhalifu na ushirikina lakini ukweli ni kwamba ipo dawa mojawapo ya usingizi ambayo hutumiwa na wezi wengi kutekeleza uhalifu huo. Dawa hiyo kitaalamu inaitwa Chloroform.

Dawa hiyo ina uwezo wa kumlegeza au kumzimisha mtu kiasi kwamba ashindwe kujitambua na kuhisi chochote na wahalifu wakafanya chochote wanachoweza kwa muda wa kutosha. Wataalamu wa afya huitumia katika shughuli za kitabibu hasa wakati wa upasuaji.

Ili kufahamu madhara na tahadhari ya kuchukua juu ya dawa hii inapotumika, soma zaidi makala hii kwa kina (na nyinginezo makini ambazo ungependa kuzifahamu) kupitia => Ni dawa gani ya usingizi wanayoitumia wezi kupuliza madirishani?
 
Back
Top Bottom