Ni akina nani walichoma BoT miaka hiyo?

Mliokula chumvi, Mtusaidie;
1. Ni nani aliyewasha jengo wakati huo
2. Nakama si binadam, chanzo chake ni nini has a?

Ilisemwa kuwa ilikuwa ni short ya umeme tu mkuu, ilitokea ghorofa ya pili.

Hivyo baadae watumishi kadhaa walifikishwa mahakamani kwa kusababisha moto na baadae wakaachiwa.

Lakini hadi kesho hakuna anaefahamu chanzo cha moto ule, na nafikiri ile kesi imefungwa.
 
Ilisemwa kuwa ilikuwa ni short ya umeme tu mkuu, ilitokea ghorofa ya pili.

Hivyo baadae watumishi kadhaa walifikishwa mahakamani kwa kusababisha moto na baadae wakaachiwa.

Lakini hadi kesho hakuna anaefahamu chanzo cha moto ule, na nafikiri ile kesi imefungwa.
Wapo wanao fahamu chanzo cha moto huo sema wako kimya tu pengine miaka miaka 10 ijayo itawekwa wazi ,
 
Nasikia eti Mtei yule miliki wa Chadema alikuwa waziri wa fedha. Na jamaa mmoja alifariki mwaka juzi alikuwa mwanachadema alikuwa agombea kila wakati ubunge kupitia chadema jimbo la shinyanga mjini yeye alikuwa gavana.
Tazama mburula Anaeli kashalipwa sasa karudi rasmi ktk mijadala ya, eti kuichafua CDM...
Sasa hata ukitumwa si utumie hata ubongo kidogo kutafuta taarifa za kweli anaeli mamaaa...
 
Go
Mkuu umeandika nusu ukweli na nusu siyo kweli. Kumbukumbu sahihi ni kwamba BOT iliungua moto mwaka 1984. Wakati inaungua waziri wa fedha alikuwa ni Kighoma Malima ambaye alikuwa katika nafasi hiyo kuanzia mwaka 1983 hadi 1985 na wakati huo gavana alikuwa ni Charles Nyirabu aliyedumu kwenye nafasi hiyo kwa miaka 15 kuanzia 1974 hadi 1989. Nyirabu alipokea kijiti cha ugavana kutoka kwa Edwin Mtei mwaka 1974.

Pia baada ya Kighoma Malima kutoka katika nafasi hiyo ya uwaziri wa fedha mwaka 1985 alirudi tena kwa mara ya pili kwenye nafasi hiyo mwaka 1994 ambako alihudumu kwa miezi kadhaa tu ndani ya mwaka huo huo na baadae kufariki 1995.

Kwa hiyo kwa upande wa Mtei alikuwa gavana kuanzia 1966 hadi 1974 na pia waziri wa fedha kuanzia 1977 hadi 1979 alipohitilafiana na Mwalimu Nyerere kuhusu kukubali au kutokubaliana na utekelezaji wa masharti ya IMF.

Bob Makani alikuwa ni naibu gavana kuanzia 1974 hadi 1986 hii ikimaanisha kwamba wakati BOT inaungua Mtei hakuwa gavana pale BOT wala waziri wa fedha isipokuwa Nyirabu na Bob Makani ndiyo walikuwa ofisi moja yaani Nyirabu akiwa gavana na Makani akiwa ni naibu wake na Kighoma Malima akiwa ni waziri.


Good history. I agree with you 100%
 
Mtoa mada anataka kujua nani aliichoma moto BOT badala ya kumpa jibu mnaanza kulumbana nani alikuwa na wadhifa gani wakati huo. Waswahili tujifunze kujibu maswali kwa usahihi badala ya kupiga chenga nyingi. Hata mimi sijui nani aliichoma moto benki hiyo ila nitafurahi nikipata jibu mujarabu.

Majibu yanayotolewa ni sahihi keani yanakanusha uongo. Kwani hujaona watu wameandika kuwa alikuewa Mtei?
 
Nyerere aliikalia ripoti ya Scotland Yard....
walimwambia ukiripoti vinginevyo tutakukanusha.....tetesi zilisema
haikuwahi kutangazwa hiyi ripoti

Kama nakumbuka vizuri Scotland Yard report yao ilikuwa inconclusive kwa sababu ushahidi uliharibiwa na viongozi. Mara tu baada ya.moto kuunguza BOT waziri mkuu wakati huo SAS waliingia ndani kuona jinsi benki ilivyoungua. Hilo lilikuwa kosa kubwa
 
Majibu yanayotolewa ni sahihi keani yanakanusha uongo. Kwani hujaona watu wameandika kuwa alikuewa Mtei?

Sawa, lakini wanamtaja Mtei kama kiongozi aliyekuwapo wakati wa kuchomwa moto Benki hiyo na siyo kama mtu aliyechoma au aliyesababisha uchomwaji moto huo.
 
Mtei alitoka kwenye uwaziri wa fedha mwaka 1979 na BOT imekuja kuungua 1984. Atakuwa alihusikaje mkuu?
1984 BOT INAUNGUWA MOTO.
1985 MZEE MWINYI ANKUWA RAIS WA JMT NA MWALIMU JKN ANABAKI KUWA MWENYEKITI WA CCM TU.
Sijui ni nchi ngapi ktk dunia hii centro bank imewahi kuunguwa moto yote kama ilivyo unguwa BOT?
 
Back
Top Bottom