G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,772
- 36,648
Ni matumani yangu kuwa Prof. Sifuni Mchome ambaye alitoka pale kitivoni UDSM ataamua kwa hekima na busara zake kung'atuka kutoka kwenye wadhifa wa katibu mkuu wizara ya elimu, sayansi na technologia pamoja na mafunzo ya ufundi anaotumikia kwa sasa!
Wakati Joyce Ndalichako (Dr. wa taaluma ya hisabati pamoja na tehama) akiwa katibu mtendaji wa baraza la mitihani (NECTA), Prof. Sifuni aliteuliwa na Kikwete aliyekuwa rais kuchunguza madudu ya NECTA kwenye maswala ya mitihani.
Prof. Sifuni aliibuka na tuhuma nzito dhidi ya Dr. Ndalichako na hapo kukaanza mambo lukuki yaliyopelekea Dr. Ndalichako kung'oka NECTA kwa mizengwe. Prof. Sifuni alikaimu nafasi yake na baadaye akateuliwa na Kikwete kuwa katibu mkuu wa wizara inayohusika na elimu na ubunifu wa Tanzania.
Kwa dhati kabisa nilimpinga Prof. Sifuni kwa matendo yake ya makusudi kuvuruga elimu! Aliivuruga elimu ikavurugika! Alijifanyia anavyotaka! Natamani kizazi kilichopitia BRN kifutike ili tuanze moja!
Mbaya zaidi Sifuni alimtuhumu Ndalichako kwa maslahi binafsi! Wakaunda timu na Kawambwa wakaanza kufanya yao! Kwa hakika waliyafanya!
Kwa dhati kabisa, Sifuni asisubiri kufukuzwa! Ajipime aondoke mapema! Asipofanya hivyo atafukuzwa! Na wengi wetu tunaliunga hilo mkono kwa dhati kabisa! Hatuwezi kuwa na wavurugaji halafu tukahubiri mabadiliko!