Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,188
- 3,370
Katika karne hii tumebarikiwa maendeleo ya makubwa mno katika teknolojia na sasa dunia imekua kama kijiji. Yapo mengi sana yaliyofanywa katika teknolojia ila internet ni teknolojia ambayo imekuwa na faida nyigi sana ikiwemo kuanzishwa kwa mtandao wa paypal ambao hurahisha kutuma na kupokea pesa kwa usalama zaidi. kwa lugha nyepesi huu mtandao ni kama m-pesa ya dunia.
Nchi nyingi sana wakiwemo hata majirani zetu kenya waliiona fursa ya kujiunga na mtandao wa paypal, leo hii muuzaji wa kenya anaweza kulipwa pesa na mnunuzi wa ujerumani anaehitaji huduma / bidhaa.
Tanzania tunachoweza kufanya kwenye huu mtandao ni kufanya malipo tu na sio kupokea malipo, kwa mfano tunaweza kununua bidhaa / huduma za kenya ila haiwezekani mtu wa marekani au kenya kununua bidhaa zetu kwa kutumia paypal, hii imesababisha watanzania wengi tushindwe kuuza bidhaa na huduma zetu mtandaoni kwa sababu wanunuzi wengi wanapendelea kununua bidhaa zao kwa paypal ambayo ni salama.
Kwa hapa Tanzania hiki kitu kimepigiwa kelele sana pasipo kua na dalili yoyte ya utekelezaji, Kinachobakia watu wanatumia internet kucheki youtube, kufatilia umbea instagram, kuchati whatsapp na kutafuta wachumba facebook na badoo.
Tunakwama wapi katika kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda, Kuwepo kwa paypal Tanzania ni kuleta uchochezi wa kupanua viwanda kwasababu soko litavuka hadi mipaka.