Nguvu ya Rais Magufuli sasa inajulikana ilipo. Ni hatari kwa uchumi wetu

Kalamu1,


Magufuli Kama ameshindwa kuelewa mabadiliko tuliyoyataka watanzania unategemea nini hapa, walimu wamenifundisha ila pia haiondoi ukweli kuwa kuwa mwalimu ni matokeo ya kufeli
 
Ajira pia ameshindwa. Tangu 2015 hakuna kinachoeleweka mpaka leo 2020.Kwa kushindwa kwake,aliwaaminisha watu eti uhakiki wa watumishi akasumbua weeee hadi leo mamtu yakarudishwa kimyakimya lakini vijana graduands wa vyuo hakuna ajira hata ya dawa.Tangu hapo ni ajira za kuungaunga tena kwa kutaka ujiko tu wala si vinginevyo.
Ndo ushafeli hivyo......Huendi Mbinguni!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ajira mbona kaachia,hujaona za madaktari 1000 na baada ya hapo walimu wanaajiri.
www.tamisemi.go.tz
www.moh.go.tz
 
Nakumbuka zile mbwembwe nyingi za kufungua viwanda karibu kila wiki kwa wakati fulani mwanzoni mwa awamu yake. Viwanda vingi alivyovifungua, vyote vilikuwa ni juhudi za Rais Kikwete.

Siku hizi hata kusikia tu lile neno la viwanda ni nadra kabisa, na baadhi yetu hatujui kama wizara hiyo bado ipo au ilifutwa, maanake hata waziri mwenyewe hajulikani kama yupo au hayupo.

Zao la pamba, wakati wa Kikwete, lilikuwa limewekewa nguvu sana kiasi kwamba maeneo yote panapolimwa zao hilo palianza kuonekana kuwa shughuli ya kulifufua zao inafanyika. Simiyu ilianza kuonekana kama mkoa maalum wa kulima zao hili.

Juhudi za kulifufua zao hilo, ulikuwa ni mkakati wa kufufua viwanda vya nguo, ili pamba tunayozalisha isindikwe hapa hapa kwetu, na kulisha viwanda hivyo. Hali hii ilitia matumaini makubwa.

Sasa sikumbuki ni lini nimesikia habari zinazohusiana na mikakati hiyo, badala yake, inaelekea hata hiyo pamba kidogo itakayoendelea kuzalishwa, tegemeo letu ni kuwauzia wenye viwanda nchi jirani yetu hasa pale Kaskazini.

Hili litakuwa ni jambo la kusikitisha sana, kwa sababu tunapoteza fursa za waTanzania katika mnyororo mzima wa zao hili muhimu.

Na kwa uhakika, wenzetu hawa wamepania hasa na mikakati yao ya kushika soko zima la ukanda huu katika swala la nguo. Wamefufua viwanda vyao, na hata zao la pamba wakaamua kulima lile la aina mpya, lisiloshambuliwa na wadudu (genetically modified), bila shaka lengo lao likiwa kujitosheleza zaidi kwenye viwanda vyao.

Hata mitumba wameamua kuipiga marufuku, ingawa ndio waliotulazimisha tusalimu amri tulipotishiwa AGOA. Ni wajanja sana hawa watu!

Hili ni eneo moja tu la viwanda, ambalo limemshinda wazi wazi Rais Magufuli kulitilia mkazo unaostahili. Miaka mitano yake yote, mbali ya kuimba kwa nguvu sana hapo mwanzo kuhusu umhimu wa viwanda, mwisho wake, kama ni alama, anastahili F kubwa kabisa.

Rais Magufuli hatatuvusha kabisaa, katika maswala ya viwanda. Labda tutegemee hayo mengine, kama ya Miundombinu, sio viwanda.

Najua kuna maeneo mengine mengi yaliyomshinda, lakini hili la viwanda lipo dhahiri.
Hahahahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi operesheni ya Jesh ya kuendesha biashara ya korosho iliishia wapi 😃 😃 😃 😃 😃 viwanda vya kijeshi vya kubangua korosho!

Inashangaza Sana Mambo yanaharibika Wazee wameufyata. Hata Taasisi ya Mwalimu Nyerere siku hizi ni inazidiwa hata na Mke wa Godbless Lema, hakika hizi Zama Ni Zama!
Mwenye picha ya yale malori yakikaguliwa kwa ajali ya kwenda kusini please aitupie
Lakini ikawaje hao wajeda wakaondoka huko kimya kimya au bado wapo huko?
Dah kiki hizi za one man show na kujimwambafai muda kitu kizuri kuamua
 
Kalamu1,

Ajira pia ameshindwa. Tangu 2015 hakuna kinachoeleweka mpaka leo 2020. Kwa kushindwa kwake,aliwaaminisha watu eti uhakiki wa watumishi akasumbua weeee hadi leo mamtu yakarudishwa kimyakimya lakini vijana graduands wa vyuo hakuna ajira hata ya dawa. Tangu hapo ni ajira za kuungaunga tena kwa kutaka ujiko tu wala si vinginevyo.
Ndo ushafeli hivyo. Huendi Mbinguni!

Sent using Jamii Forums mobile app
Jambo lo lote likianza kwa mikogo tambua kabisa halitofika mbali
Hata team sifia washachoka kusifia
 
Busara zilikuwa ziaze ktk kufufua mazo ya biashara kwanza ili kuvutia uwekezaji ktk viwanda, Pia tuanze kufufua viwanda vyote alivyoanzisha Mwalimu. Badala yake tukaanza mkakati wa kujenga viwanda vipya bila dira ya aina yoyote! Tumeishia kuhesabu vyerehani na machine za kufyatulia matofali kama viwanda! Shame!
 
Back
Top Bottom