Nguvu ya Muziki

chofachogenda

Senior Member
Oct 6, 2016
107
199
NGUVU YA MUZIKI

Kila mikimtazama binti yangu Darina akijaribu kumumunya maneno na kucheza kwa hisia kila akiskia nyimbo anayoipenda ama kuifahamu kuipitia simu ya mama yake au radio au hata nikijaribu kumuimbia mwenyewe nyimbo ambazo nimemkaririsha japo hawezi kuziimba vyema sababu ya umri wake mdogo ,au kila wakati anapogoma kula basi huwa anawekewa muziki anaoufahamu na hapo mara mara moja ataanza kufukia matonge kama sio yeye yule aliyekuwa anatema chakula dakika mbili zilizopita. Hii huwa inanipa majibu kwamba muziki una nguvu ya ziada ukiachana na kuwa hobi au kuburudisha peke yake. Na hii ni kwa aina yote ya muziki ambayo ipo duniani mfano regge,bongofleva, hiphop, dance, gospel, Qaswida , Rock,RnB n.k.

Kama unaona story yangu na mwanangu haina mashiko je unaifahamu story ya wimbo unaoitwa Gloomy Sunday uliopelekea vifo vya watu zaidi ya mia moja ikiwemo na mtunzi mwenyewe aliyotunga huo wimbo. Mtunzi wa wimbo huo bwana Rezso Seress aliandika wimbo huo baada ya kuachwa na mpenzi wake pamoja na kupiga ala za muziki za huzuni. Hali iliyopelekea watu wengi kujiua kila wanaposikiliza wimbo hasa wale walioachwa na wapenzi wao kiasi cha kupigwa marufuku nchini Hungary na hata ulipotafsiriwa kwa lugha nyingine uliendelea kuleta matokeo hayohayo na kupigwa marufuku nchini uingereza mwaka 1968. Huu ni wimbo ambao ulipelekea mpenzi wake ambaye alimuacha pia kujia na kupelekea yeye mwenyewe mtunzi pia kujiua. Je huamini kama muziki una nguvu ya ziada kwenye mwili wa mwanadamu.

Kila ubongo wa mwanadamu bila kujali umri unapokea na kurespond kwa aina fulani ya muziki anaoupenda.Wanasema kwamba kila mtu ana keynote yake ambayo ikiguswa medulla itarespond tu hiyo kama mapenzi tungesema umefikishwa kileleni. Aina tofauti za muziki zinaweza kuathiri ubongo tofauti kama vile aina mbalimbali za muziki zitakavyoweza kukugusa kulingana na hali fulani au mood fulani ambayo unayo kwa muda huo.

Watu wengi wanasikiliza muziki kwa matumizi mbalimbali kama vile kusoma inasaidia kufocus kwa baadhi ya watu, Kufanya mazoezi hii inasaidia kuongeza energy na kufanya zaidi ya ambapo ungefanya bila muziki. Hivyo muziki sio huondoa tu uchovu wa mwili lakini vilevile huondoa uchovu wa akili.

Ndio maana sishangai kwamba kwenye maandiko matakatifu ya kikristo kusema kwamba huko peponi kutakuwa na suala moja tu muhimu yaani kuimba na kusifu tafsiri ya harakaharaka hapa ni kwamba hata Mungu mwenyewe anapenda kusikiliza muziki la sivyo angechagua kitu kingine badala ya kuimbiwa hivyo muziki sahihi una nguvu ya kiungu ndani yake ndio maana kwenye biblia kuna maandiko mbalimbali yanayohusisha kumuimbia au kumpigia muziki Bwana Mungu mfano Ufunuo wa Yohana 14;3-4,Zaburi 98:1-7,Zaburi 150:1-5 Zaburi 105:2, 2 mambo ya nyakati 5:13 n.k.

Hata hivyo mpinzani mkuu wa Mungu Lucifer ama Ibilisi kabla ya kufurushwa na kuja duniani baada ya uasi alikuwa anahudumu katika sekta hii ya muziki moja ya sekta muhimu huko mbinguni na hata kwenye quran tukufu inadaiwa kwamba shetani anatumia sauti yake (muziki) kutoposha na kufanya watu washindwe kuzingatia kusoma na kusikiliza Quran tukufu ndio maana kwa baadhi ya waislam muziki ni haramu. Katika hadithi ambayo ameipokea Imamu Bukhari mtume Muhammad (S.A.W) anasema “Watatokea katika umma wangu watu (ambao) watahalalisha zinaa na hariri na ala (nyenzo) za muziki”. Hii kauli inapigilia msumari kwamba muziki ni haramu ndio maana wazee wa Taliban hakuna mambo ya muziki muziki kwenye tawala yao.

Katika kila tamaduni ambayo unaifahamu hapa duniani basi jua wana aina yao ya muziki kwa ajili ya matumizi mbalimba katika jamii husika mfano shughuli za kiroho kama matambiko, burudani, kufikisha ujumbe, kuonya jamii,

Muziki una nguvu ya kuponya mwili (music therapy), kutusafirisha mbali kihisia kututoa katika hali fulani ya kimwili na kutupeleka katika hali fulani ya kiroho kwa kuteka kabisa hisia zetu nadhani nyie wenyewe mashaidi kama ukisikiliza nyimbo yako pendwa au ukikukugusa automatically unajikuta unasafiri mbali sana kihisia ushawahi kusikiliza kaya ya bob marley huku unavuta mmea hahahahaaa ama katika makanisa ya kilokole kikifika kipengele cha kuabudu basi itaimbwa nyimbo ambayo itasaidia watu kuhama kabisa katika physical dimension na kufika katika hali ya kiroho kitu ambacho huanza kuona baadhi ya waumini machozi yanawatoka, wengine wanaanza kunena kwa lugha na wengine kulipuka mapepo, muziki pia unaleta hali fulani ya kufurahi ama kuleta energy ndio maana gym yoyote lazima itakuwa na muziki tu watoto wa mjini tunasema vibe (positive vibration),

Muziki unatukumbusha baadhi ya matukio katika maisha yetu ambayo tuliwahi yapitia katika maisha yetu au vipindi fulani katika maisha yetu mfano kwa upande wangu kila ikipigwa yule ya AY basi naishia kumkumbuka sweet mangi fulani hivi ambaye nilikuwa namtamani kwelikweli lakini sikuwa na ujasiri wa kumwambia yaliyo moyoni (domo zege) nikawa naishia kuumia moyoni tu alafu ndio na yule ya AY inatoka kipindi hicho wacha kabisa basi kila nikiusikia huu wimbo mawazo yanarudi kulekule

Pia muziki husaidia kubadili tabia msanii Niki Mbishi aliwahi kuelezea namna gani aliweza kupata mrejesho kwa mashabiki wake waliosikiliza wimbo wake uitwao Kijusi kuhairisha kutoa mimba kutokana na ujumbe walioupata kwenye wimbo huo au kuchochea harakati fulani mfano muziki wa reggae ulijikita sana katika kutetea sana haki za mtu mweusi na kutokana na ujumbe ambao umebebwa kwenye muziki husika lakini muziki

Hutumiwa kuelezea hisia zetu hapa ndio tutafahamu umuhimu wa kuwa na mashairi ya kujenga ndani ya muziki sababu muziki ni nyenzo muhimu katika kusaidia kubadili tabia, lakini kubwa zaidi muziki hutumika kuelezea hisia zetu aidha kwa muimbaji mfano wewe msikilize Sugu katika wimbo wake wa hayakuwa mapenzi utanielewa namaanisha nini kutoa hisia au sisi wahenga wa kisasa ambao tulikuwa tunaandika dedication ya nyimbo kila mwisho wa barua ya mapenzi kabla ya ujio wa simu za mkononi, lakini pia mpangaji wetu Khadija alivyokuwa anatumia taarab kufikisha ujumbe au vijembe siku nzima akikorofishana na wenzie kuhusiana na zamu ya usafi wa nyumba

Muziki kisayansi ni tiba tosha ndio maana kuna Music therapy yaani tiba ya kutumia sauti za muziki inaweza kuwa beat tu au hizi nyimbo zetu za kawaida kwa ajili ya kusaidia matatizo mbalimbali katika miili yetu. Katika aina hii ya tiba mtu anawekewa mziki ambao unakuwa unaojirudiarudia kwa kutumia aina fulani ya keynote ambayo itafanya medulla oblongata kuvibrate taratibu sambamba na keynote na punde tu mapigo ya moyo yanakuwa sawa na kusababisha msawazo ndani ya mwili na mwili utarespond na kujirekebisha wenyewe sehemu ambayo ina kasoro Kwa hiyo ndugu zangu msisahau kupata vitamin Music kama anavyosema msanii wa kizazi kipya Bell 9 kwenye wimbo wake maarufu wa Vitamin Music aliomshirikisha msanii wa hiphop Joh Makini.

Aina hii ya tiba inasaidia kutibu vitu mballimbali ikiwemo matatizo ya moyo, msongo wa mawazo, inasaidia watu wenye usonji(Autism) kufocus,kurudisha kumbukumbu, shinikizo la chini la damu (lower blood pressure), kuongeza kujiamini.

Kama tunavyofahamu kwamba kila dawa kwa na namna fulani pia ni sumu ndivyo hivyo pia ilivyo katika suala zima la muziki. Mfaano kwa upande wangu kuna baadhi ya miziki nikisilkiliza huwa napata maumivu ya kichwa kutwa nzima badala ya kunifanya niwe sawa mfano zile singeli michano achana na hizi za kina Mejakunta kuna zile kama wanarapurapu lakini singeli wanapenda sana kuzisikiliza bodaboda kwa sauti ya juu huku wakiwa kwenye mwendo mkali huku wakiburuza sandals zao kweny lami aisee zile nadhani zipo katika frequency ambayo haziendani na mwili wangu. Maana mimi ni mpenzi wa karibia aina azote za muziki ila ule hapana.

Kutokana na hilo basi muziki pia una hasara zake hapa nadhani zile hoja za muziki haramu ndio zinakaa vizuri sasa. Moja ya hasara hizo ni kama zifuatavyo

Hisia kali kupindukia. Hivi ushawahi ushawahi kuwa na mawazo alafu unasikiliza nyimbo za huzuni hapa badala ya kutibu tatizo unaongeza tatizo hebu sikiliza kidogo So sick ya NE-YO kagusia kitu kama hichi , Rafiki mmoja alishawahi nisimulia tukio moja kipindi anasali katika parokia ya Makuburi jijini DSM basi mtunzi mahiri wa nyimbo za kikatoliki bwana Bernad Mukasa na kwaya yake waliimba wimbo moja ya huzuni inaitwa Mbele ya Jeneza kilichotokea kanisani kulitokea vilio vya kuombleza kiasi ambacho padre wa kanisa kupiga marufuku nyimbo hiyo kuimbwa tena kanisani. Kwa hiyo badala ya kufariji iliishia kutonesha vidonda vya waumini kaitafute You Tube alafu utaaniambia.

Mashairi yenye upotoshaji. Miziki yetu mingi tunayoiskiliza sasa hivi ni kama unamkaribisha shetani kwenye sebule yako kama sio kichwa chako.Kuna nyimbo nyingi unatamani usikilize tu kwa earphone mwanao asisikie lakini hata wewe mwenyewe unaishia kupanda tu mbegu ya ibilisi maana kitu unachopanda kwenye conscious mind huwa kinaenda kumea kwenye subconscious mind. Aina ya mashairi ambayo nyimbo zinabeba ni hovyo kama sio muziki wa ngono maana sio hisia ni kitendo ndio kinachotamkwa basi ni violence yaani mafujo fujo wenyewe wanaita gangster rap. Aina hii ya muziki ikichekewa jamii inapotea walahi si unaona kwa Biden huko maniga wanvyopigana shaba. Mashairi ya kishenzi yanachochea tabia hasi kwenye jamii.

Kurudisha kumbukumbu sio kila aina ya kumbukumbu ambayo mziki inaleta inakuwa ni nzuri wakati mwingine muziki huleta kumbukumbu mbaya na zenye kuumiza na ndio maana mpaka leo kuna watu wakisia wimbo fulani huishia kulia labda inamkumbusha kifo cha mzazi wake ama mpenzi wake au tukio lolote lile ambalo halikuwa zuri katika kpindi fulani cha maisha yake. Wakati nasoma kuna rafiki yangu wa kike ambaye kila akisikia wimbo wa Celine Dion uitwao Goodbye’s basi huishia kumkumbuka marehemu mama yake hivyo huishia kulia na kukosa raha kutwa nzima.

Kwa mimi ninachoamini ni kwamba muziki umebeba nguvu zote chanya na hasi sasa kazi kwako kusikiliza vitu vya kukujenga au vya kukubomoa.

Kwa kumalizia naomba kila mmoja aweke nyimbo zake au wimbo wake mkali ambayo ukiisikiliza hisia zako zinaenda mbali kabisa.

“MUSIC IS THE SOUNDTRACK OF YOUR LIFE”​

Kikuweli nina mengi ya kuandika ila kwa leo tuishie hapa mengine siku nyingine .Asanteni wote mlionisaidia kufanikisha makala hii;

BENJAMINS
 
Unaijua muvi ya Coco?

Basi ni kwamba "He will listen, to music"

Napenda nyimbo nyingi ila wimbo ambao siwezi usahau mashairi yake ni "You ain't know" wa lil wayne na birdman. Ndiyo wimbo pekee ninaouweka kama ringtone nikitaka kuweka ringtone.
Screenshot_2021-08-19-15-02-39-90.jpg
 
Umeandika vizuri sana kihisia km Music. Kweli Music ni kitu cha ajabu sana ukianzia kwa mtoto hata mimi mwanangu akisikia music hua anachanganyikiwa kwa kucheza nadhani Music ni Ulevi ndio maana uislaam umepinga mziki
 
Asante kaka ni kweli kabisa Kuna sheikh mmoja aligusia hilo kwa namna fulani.
 
Unaijua muvi ya Coco?

Basi ni kwamba "He will listen, to music"

Napenda nyimbo nyingi ila wimbo ambao siwezi usahau mashairi yake ni "You ain't know" wa lil wayne na birdman. Ndiyo wimbo pekee ninaouweka kama ringtone nikitaka kuweka ringtone.
View attachment 1898096
Hyo ngoma ya Luniz I got 5 in it sichoki kuisikili
Hii ngoma sasa uwe na muziki wenye bass ebwana unakua unatikisa kichwa huku hautamani wimbo uishe.
Acha kabisa mkuu hi nymbo ni ya Miaka ya 90 uko ila ukiskiza leo badi iko hot, atar sana
 
hahahaa nimeusikiliza huo wimbo nikajiridhisha sababu ya watu kujiua baada ya kuusikiliza.

mtunzi anakusimanga,kama ni muhanga huwezi pata amani.
nimeishi kijijini ambako hakukuwa na umeme,siku ambazo nilikuwa napata furaha isiyoelezeka,ni siku amabayo nilikuwa nikitumwa bettery 6 mpya dukani,maana ilikuwa ni tiketi ya burudani kwa siku nne mbele ya kusikiliza tape za miziki mbali mbali.
kwa sasa natumia earphone muda mwingi sana.bahati mbaya siwezi mweleza mwingine akanielewa ni raha kiasi gani huwa napata nikiwa nasikiliza muziki.
 
Hakika nakubali, muziki Una kitu fulani. Mi pia ni mpenzi wa muziki karibu aina zote, lkn nyimbo hizi hapa hunipa hisia sana, na nimekuwa mwaminifu kwa hz nyimbo kiasi siwezi kuitaja moja nikaacha zingine;

1. It feels so good ya mwanadada flan anaitwa sonique. Aisee hiki kitu kinanikosha sana na kunipa hisia........kimepigwa kwa ufundi mkubwa mno lkn very simple

2. Ebitebi ya papy tex. Hiki kibao kinanikumbusha miaka ya 90 huko tulivyokuwa tunajimwaga barabarani baada ya kurudi shule kucheza.....siwezi kusahau ile enzi aisee. Muda umeenda wapi!!

3. Nawashukuru wazazi wangu ya ddc mlimani park.....hiki kitu huwa najikuta mpaka nalia wakati mwingine; lile guitar lilivyocharazwa kwa masikitiko. Dah!!

4. Ni wewe mpenzi wangu nikupendae ya kilwa jazz band. Hiki kitu kinanipa picha ya utulivu wa mapenzi ya mababu zetu aisee.....kinanipa hisia sana huku nikiwakumbuka bibi na babu yangu wazaa mama aisee.

5. Kighetogheto ya juma nature (kibra). Huu wimbo ulinikuta nikiwa shule fulani ya bweni, aisee ulitubamba sana hususani ile sehemu anayozungumzia shule....kwmb sijui bora daftari atungie verse, kwmb mwalimu akiingia darasani kila swali anamuuliza yeye kwani ye ndo nani. Iligusa sana maisha yetu ya shule hii nyimbo. Naipenda hadi kesho na kila nikiisikia najikuta nimerudi shule na rafiki zangu wale. Dah, kibra una heshima sana kwangu kutokana na kawimbo kako haka kilicho simple

6. Irene ya senzo.....acha tu hiki kitu
7. Mickey ya DMX, hiki kitu ni very classic
8. Cherioh baby ya jamaa flan hv wa Jamaica km sikosei, nimemsahau jina, UB40 walikuja kuurudia baadae wimbo wenyewe. Sikomi kuusikiliza
9. Aysha wa mwanamuziki fulani wa Indonesia anaitwa Yasin....kitu kimoja Chenies hisia sana.
10. Ndaya ya m'pongo love....dah, r.i.p dada yangu!

Ngoja niishie hapa maana nimeanza kujisikia tofauti
 
hahahaa nimeusikiliza huo wimbo nikajiridhisha sababu ya watu kujiua baada ya kuusikiliza.

mtunzi anakusimanga,kama ni muhanga huwezi pata amani.
nimeishi kijijini ambako hakukuwa na umeme,siku ambazo nilikuwa napata furaha isiyoelezeka,ni siku amabayo nilikuwa nikitumwa bettery 6 mpya dukani,maana ilikuwa ni tiketi ya burudani kwa siku nne mbele ya kusikiliza tape za miziki mbali mbali.
kwa sasa natumia earphone muda mwingi sana.bahati mbaya siwezi mweleza mwingine akanielewa ni raha kiasi gani huwa napata nikiwa nasikiliza muzik
Aisee muziki acha tu ndio maana masela wengi wanaanza maisha kwa sabufa na godoro
 
Hapa
Hakika nakubali, muziki Una kitu fulani. Mi pia ni mpenzi wa muziki karibu aina zote, lkn nyimbo hizi hapa hunipa hisia sana, na nimekuwa mwaminifu kwa hz nyimbo kiasi siwezi kuitaja moja nikaacha zingine;

1. It feels so good ya mwanadada flan anaitwa sonique. Aisee hiki kitu kinanikosha sana na kunipa hisia........kimepigwa kwa ufundi mkubwa mno lkn very simple

2. Ebitebi ya papy tex. Hiki kibao kinanikumbusha miaka ya 90 huko tulivyokuwa tunajimwaga barabarani baada ya kurudi shule kucheza.....siwezi kusahau ile enzi aisee. Muda umeenda wapi!!

3. Nawashukuru wazazi wangu ya ddc mlimani park.....hiki kitu huwa najikuta mpaka nalia wakati mwingine; lile guitar lilivyocharazwa kwa masikitiko. Dah!!

4. Ni wewe mpenzi wangu nikupendae ya kilwa jazz band. Hiki kitu kinanipa picha ya utulivu wa mapenzi ya mababu zetu aisee.....kinanipa hisia sana huku nikiwakumbuka bibi na babu yangu wazaa mama aisee.

5. Kighetogheto ya juma nature (kibra). Huu wimbo ulinikuta nikiwa shule fulani ya bweni, aisee ulitubamba sana hususani ile sehemu anayozungumzia shule....kwmb sijui bora daftari atungie verse, kwmb mwalimu akiingia darasani kila swali anamuuliza yeye kwani ye ndo nani. Iligusa sana maisha yetu ya shule hii nyimbo. Naipenda hadi kesho na kila nikiisikia najikuta nimerudi shule na rafiki zangu wale. Dah, kibra una heshima sana kwangu kutokana na kawimbo kako haka kilicho simple

6. Irene ya senzo.....acha tu hiki kitu
7. Mickey ya DMX, hiki kitu ni very classic
8. Cherioh baby ya jamaa flan hv wa Jamaica km sikosei, nimemsahau jina, UB40 walikuja kuurudia baadae wimbo wenyewe. Sikomi kuusikiliza
9. Aysha wa mwanamuziki fulani wa Indonesia anaitwa Yasin....kitu kimoja Chenies hisia sana.
10. Ndaya ya m'pongo love....dah, r.i.p dada yangu!

Ngoja niishie hapa maana nimeanza kujisikia tofauti
Ngoja niingie you tube kusikiliza ngoma ulizozitaja ambazo sizifahamu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom