Ngozi ya ng'ombe na Mbuzi zinaliwa?

whn i was in jobeg intered nigerian restaurant and my friend and i we were shocked to be save rosted goat including the skin.
It is very true

kwa kuwa umesoma uzi ulioandikwa kwa kiswahili na ukaelewa, basi ungechangia kwa kiswahili. Kiingereza chako kinachefua.
 
kwa kuwa umesoma uzi ulioandikwa kwa kiswahili na ukaelewa, basi ungechangia kwa kiswahili. Kiingereza chako kinachefua.

Mkuu sisi ma-Tanzania ni mazumbukuku! Umeona kilivyojaa ukakasi eeeh?
 
Hizi supu mbona maarufu sana kwenye baadhi ya maeneo mengi hapa jijini Dar es salaam!nami nilishazipiga sana kipindi niko mdogo!kama utakua na chapati zako ndimu pilipili inakwenda bila wasiwasi wowote
 
Aha!Ndio maana nilipoenda kwa wakwe zangu huko viatu vyangu na mikanda yangu ilitoweka katika mazingira ya kutatanisha!tena nina wasiwasi na ile pilau yenye nyama nyembamba nilyokula siku ya mwisho!
 
Binafsi nimeshakula ngozi ya ng'ombe mara mbili kijijini kwetu na niliipenda sana ukipika hasa kwenye matoke. Uhayani inaitwa O'lui lwe e'nte.

Uandaaji wake kama huna roho ngumu basi huwezi kula hiyo ngozi.

Uandaaji wake: Unachukua ngozi ya ng'ombe unaiweka kwenye mfuko wa plastiki(Naironi), unaifukia chini ya udongo kwa siku nne na kuendelea mpaka hapo itakapooza.

Ukijiridhisha kuwa imeoza basi utaifukua na itakuja ikiwa na harufu kali sana,pia itakuwa na mafunza (Maggots). Unachukua kiwembe kikali na kuanza kuparura ili kuondoa manyoya kwenye ngozi, ukijiridhisha yameisha basi utaisafisha kwenye maji ya moto vizuri alafu utaibanika kwenye moto mpaka itakapokauka vizuri,unaweza pia kuiwekea chunvi ama ndimu ili kukata shombo.

Nyama ile ya ngozi ni tamu sana ukiitumia kwenye ndizi bukoba. Siku ya kwanza kula sema ukweli nilijamba hatari sana na ushuzi ulikuwa ukinuka kama nimemeza panya aliyeoza, na harufu yake haikati haraka ukiigusa mikononi.

cc. KakaKiiza
Nakuulila kyoma............ekyo ekye nzito......mmmmmmhhh
 
Binafsi nimeshakula ngozi ya ng'ombe mara mbili kijijini kwetu na niliipenda sana ukipika hasa kwenye matoke. Uhayani inaitwa O'lui lwe e'nte.

Uandaaji wake kama huna roho ngumu basi huwezi kula hiyo ngozi.Uandaaji wake: Unachukua ngozi ya ng'ombe unaiweka kwenye mfuko wa plastiki(Naironi), unaifukia chini ya udongo kwa siku nne na kuendelea mpaka hapo itakapooza.

Ukijiridhisha kuwa imeoza basi utaifukua na itakuja ikiwa na harufu kali sana,pia itakuwa na mafunza (Maggots). Unachukua kiwembe kikali na kuanza kuparura ili kuondoa manyoya kwenye ngozi, ukijiridhisha yameisha basi utaisafisha kwenye maji ya moto vizuri alafu utaibanika kwenye moto mpaka itakapokauka vizuri,unaweza pia kuiwekea chunvi ama ndimu ili kukata shombo.

Nyama ile ya ngozi ni tamu sana ukiitumia kwenye ndizi bukoba. Siku ya kwanza kula sema ukweli nilijamba hatari sana na ushuzi ulikuwa ukinuka kama nimemeza panya aliyeoza, na harufu yake haikati haraka ukiigusa mikononi.

cc. KakaKiiza
Wewe wa Bugabo-Buzi nini?maana nasikia huko wanafukua vilivyozikwa
 
Huko shida sana. Wanakula mpaka mbegu za ----- wakiita (maharagwe poli). Wakati ni sumu Kali sana ile
 
pita pale mitaa ya mbagala rang3 midA yA jionI ujipatiE xupU yakO yA ngozI pa1 nA ubongO
 
Wewe wa Bugabo-Buzi nini?maana nasikia huko wanafukua vilivyozikwa

Mkuu huko ndio kwenu nini? Hivi mshaacha kula nyama za watu? Kule hakufai wanachafua taswira ya mkoa wa Kagera kwa tabia zao za kula nyama za watu.
 
Wana wa JF. Leo nimeshuhudia watu wakila ngozi ya Ng'ombe iliokaushwa kisha kuchomwa na kisha kuparuliwa manyoya na kukatwa vipande vipande na kuchemshwa supu na watu kunywa! Wengine hununua na kwenda kuunga ili wale na ugali!

Hii nimeikuta Kilwa, mkoa wa Lindi na wameniambia ngozi hizi hutoka maeneo ya Mbagala Dar. Ama kweli maisha bora kwa kila Mtanzania nimeiona wandugu.

kipindi nasoma shule ya msingi (2000s) turiani pale maeneo ya magomeni, kulikuwa na mzee mmoja alikuwa anauza supu ya ngozi za n'gombe. aisee ilikuwa tamu vibaya mnoo halafu alikuwa anauza na chapati. basi ilikuwa kila saa 12 jion tupo pale tunapata kitu cha ngozi ya supu.
 
Back
Top Bottom