Ngozi ya ng'ombe na Mbuzi zinaliwa?

Albosignathus

JF-Expert Member
Apr 26, 2013
4,886
1,038
Wana wa JF. Leo nimeshuhudia watu wakila ngozi ya Ng'ombe iliokaushwa kisha kuchomwa na kisha kuparuliwa manyoya na kukatwa vipande vipande na kuchemshwa supu na watu kunywa! Wengine hununua na kwenda kuunga ili wale na ugali!

Hii nimeikuta Kilwa, mkoa wa Lindi na wameniambia ngozi hizi hutoka maeneo ya Mbagala Dar. Ama kweli maisha bora kwa kila Mtanzania nimeiona wandugu.
 
Binafsi nimeshakula ngozi ya ng'ombe mara mbili kijijini kwetu na niliipenda sana ukipika hasa kwenye matoke. Uhayani inaitwa O'lui lwe e'nte.

Uandaaji wake kama huna roho ngumu basi huwezi kula hiyo ngozi.

Uandaaji wake: Unachukua ngozi ya ng'ombe unaiweka kwenye mfuko wa plastiki(Naironi), unaifukia chini ya udongo kwa siku nne na kuendelea mpaka hapo itakapooza.

Ukijiridhisha kuwa imeoza basi utaifukua na itakuja ikiwa na harufu kali sana,pia itakuwa na mafunza (Maggots). Unachukua kiwembe kikali na kuanza kuparura ili kuondoa manyoya kwenye ngozi, ukijiridhisha yameisha basi utaisafisha kwenye maji ya moto vizuri alafu utaibanika kwenye moto mpaka itakapokauka vizuri,unaweza pia kuiwekea chunvi ama ndimu ili kukata shombo.

Nyama ile ya ngozi ni tamu sana ukiitumia kwenye ndizi bukoba. Siku ya kwanza kula sema ukweli nilijamba hatari sana na ushuzi ulikuwa ukinuka kama nimemeza panya aliyeoza, na harufu yake haikati haraka ukiigusa mikononi.

cc. KakaKiiza
 
Ngozi ya moooh!!! Mkuuu huwa inaliwa kutokana na uhaba wa chakula au ni msosi wa kawaida tu!? Halafu inaozeswa kwanza!!!!?? Duuuh ngachoka!!!
 
Ngozi ya moooh!!! Mkuuu huwa inaliwa kutokana na uhaba wa chakula au ni msosi wa kawaida tu!? Halafu inaozeswa kwanza!!!!?? Duuuh ngachoka!!!

Hailiwi kwasababu ya uhaba wa chakula but kama kitoweo cha kawaida. Inaozeshwa ili iwe rahisi kuondoa manyoya.
 
Sasa cha ajabu nini hapo? Kwa yeyote anayekula supu ya mkia, kongoro, pua na masikio huyo anakula ngozi...unafikiri kwa nini pale manzese uwanja wa fisi panaitwa hivyo? Hapaanikwi ngozi pale!
 

jamaa wa ghana wanakunywa sana supu na ngozi ya ng'ombe...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…