Neema kwa wafanyakazi yatangazwa na Rais Magufuli

Tuwe wavumilivu,nazani akiimalisha vyanzo vingine vya mapato kodi ya mishahara itashuka zaidi huu ni mwanzo na amekaa muda mfupi sana...........Pia jamaa angefuta kodi yote sisi wenyewe tungekuja kumlaani humu ndani kwamba amekurupuka na amepoteza pato la taifa (binadamu hatuna wema ni kawaida yetu yetu kutengeneza dhana ya ushawishi kwenye taswira ya udhaifu kama mtu hatumkubali)
 
Asilimia 2 iliyoshuka itakufanya kipato chako kiongezeke Sh. 3,800 tu kwa mwezi sana na kilo 2 za sukali kwa mwezi. Hata hivyo Serikali itakosa mapato kiasi kikubwa mno. Chukua kwa mfano watumishi 500,000 × 3,800 = 1,900,000,000 kwa mwezi Serikali itakosa kama mapato. Sijui Tz kuna watumishi wangapi.

Si haba mwanzo mzuri. ila najua wengi hawajui namna ya kutafuta kodi halisi. Punguzo hilo ni kwa kiasi kinachozidi 170,000 hadi 360,000= 190,000 x 2% = 3,800.
 
Wakati bara JPM amepunguza 2% ambapo ni 1,200 Tsh kwa kipato cha chini......wenzetu Zbar wamepigwa double salary! Ila isije kuwa tofauti inakuwa mzigo wa Bara kufidia!
 
WADAU SIJAELEWA KUHUSUHIZI ASILIMIA, NDIYO KODI ZENYEWE? INA MAANA KAMA UNAPATA MSHAHARA 1,200,000/= UNAKATWA 30%%???
20160502_072234.jpg
 
Hii kitu inabidi ielezwe vizuri ieleweke. Ni kweli wafanyakazi wote watakata 9% ( single digit) ya gross earning zao au kodi zitapungua kwa 2% kwa income bands zote. Kama ni hivyo, ni nani beneficiries wa hiyo single digit- ni watumishi wa kima cha chini?
Yap!! Kima cha chini tu ndiyo wamepata neema. Wengi wetu tunalipa 24% sasa hiyo single digit haituhisu. Sisi tusubiri kama kutakuwa na nyongeza ndiyo tuona impact fulani.
 
Tuwe na Shukrani hata kwa hicho kidogo, binafsi kitanisaidia kupanda daladala, karibu 20,000 imepona.

Shukrani ya nini bibiye? Wajibu wetu kama raia ni kufanya kazi na kulipa kodi.

Shukrani ni kwa Mungu tu na si mwanadamu hasa kwenye stahiki zetu. Sanasana Rais na serikali yetu ni wakututumikia sisi waajiri wao.
Kwa ufupi rais ni mtumishi wetu kimantiki, angalao huku kwetu Afrika ni kinyume chake. Huku rais ni zaidi ya wafalme na machifu wa kale.
 
Tatizo PAYE sio fixed
utaambiwa asilimia 9 lakini utakwata zaidi
kuna ujanja unatumika hawasemi
watu wanakatwa hadi asilimia 30 ya mshahara

Watu wa mahesabu ni wajanja sana,wanakuaminisha namba ndogo ukija uhalisia unakuta umekatwa zaidi ya 20%. Afadhali amejaribu kupunguza watu wa TRA nao wawe na huruma na watumishi katika kuweka hizo fomulars zao.
 
Wakubwa ni kigezo gani hutumika kuchagua/kuteua mfanyakazi bora? Maana kuna watu wanastaafu hawajawahi kupata ufanyakazi bora.Je,ni mwajiri au chama cha wafanyakazi ndiyo mwenye kutoa zawadi?
 
Back
Top Bottom