Davidmmarista

JF-Expert Member
Apr 11, 2024
1,628
3,030
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika kuanzia Novemba 11 hadi Novemba 29, 2024.

Matokeo hayo yametolewa rasmi leo, Alhamisi, Januari 23, 2025, na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Mohammed.

Wanafunzi pamoja na wazazi sasa wanaweza kuyaona matokeo hayo kupitia tovuti rasmi ya NECTA.

Bonyeza hapa kutazama matokeo ya kidato cha nne mwaka 2024/2025

Hongera kwa waliofanikiwa, na kwa wale ambao hawakufikia malengo, bado kuna nafasi ya kujifunza na kufanikiwa zaidi!

===================================================

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limezuia matokeo ya wanafunzi 459 wa kidato cha nne mwaka 2024 kwa sababu mbalimbali zilizosababisha wasifanye mitihani yote.

Hata hivyo wanafunzi hao wamepewa fursa ya kurudia mitihani ya kidato cha nne mwaka huu 2025.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Said Mohamed, akitangaza matokeo ya kidato cha nne leo Alhamisi Januari 23, 2025 amesema wanafunzi hao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani ya kidato cha nne kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.

Aidha, Baraza la Mitihani limetangaza kufuta matokeo ya wanafunzi 67 wakiwemo watano walioandika matusi kwenye mitihani.

Dk Said Mohammed amesema wanafunzi hao wameandika matusi ni tatizo la maadili.

“Maadili, matusi hayakubaliki chumba cha mtiani na kila mahali, mwaka huu wametokea wanafunzi watano wameandika matusi,”
 
Matokeo ya Form Four 2024/2025​

Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha nne (matokeo ya kidato cha nne 2024), almaarufu kama ertificate of Secondary Education Examination(CSEE), ni mojawapo ya mitihani muhimu inayosimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
Mtihani huu hufanyika kila mwaka kwa wanafunzi wa shule za sekondari kote nchini Tanzania, ikiwa ni hatua muhimu ya tathmini ya maendeleo ya kitaaluma baada ya miaka miwili ya masomo.

Tunawatakia Mafanikio mema wote mliofanya mtihani huo.

Matokeo.jpg
 
Nilisoma St. Kayumba, matokeo si haba, nimejaribu kufuatilia wale niliomaliza nao wapo wapi siku hizi nakuta almost wote tuliomaliza na kujitahidi si haba Mungu ametujaalia huko mbeleni hakuna aliyepotea kwenye Radar. Ujumbe wangu ni huu, hawa waliofaulu St. Kayumba wana-possibility kubwa sanaa ya kuja kufanya vizuri iwapo hawatozembea. Sizisemi vibaya shule za private lakini ninao ushuda wa jamaa wawili waliomalizaga St. Lakini walipokuja kujiunga kwenye St kayumba matokeo ya Six walizungusha. Nilishangaa sanaaa.
 
Kuwapa Mzimuni Sec mtihani sawa na St Francis Girls sec ni uonevu. Hawa watoto wa St Francis wote One ya 7. Mzee LIKUD bado unaamini kwenye St Kayumba? Nenda kaangalie Mzimuni Sec
Trust me wengi wamesoma huko as Center of exam lkn sio sehemu ya kukusaidia kufaulu wengi hata hawaendi wanashinda tuition za mwenge,mchikichini na huko mitaani pia,kayumba ni kwenda kufanya mock exams/necta only
 
Nilisoma St. Kayumba, matokeo si haba, nimejaribu kufuatilia wale niliomaliza nao wapo wapi siku hizi nakuta almost wote tuliomaliza na kujitahidi si haba Mungu ametujaalia huko mbeleni hakuna aliyepotea kwenye Radar. Ujumbe wangu ni huu, hawa waliofaulu St. Kayumba wana-possibility kubwa sanaa ya kuja kufanya vizuri iwapo hawatozembea. Sizisemi vibaya shule za private lakini ninao ushuda wa jamaa wawili waliomalizaga St. Lakini walipokuja kujiunga kwenye St kayumba matokeo ya Six walizungusha. Nilishangaa sanaaa.
Kama upo na miaka kuanzia 35 kwenda juu basi hoja yako ni sahihi .

Ila Kwa zama hizi shule za serikali hazina weledi Kama zamani .

Fatilia utaona.
 
Nilisoma St. Kayumba, matokeo si haba, nimejaribu kufuatilia wale niliomaliza nao wapo wapi siku hizi nakuta almost wote tuliomaliza na kujitahidi si haba Mungu ametujaalia huko mbeleni hakuna aliyepotea kwenye Radar. Ujumbe wangu ni huu, hawa waliofaulu St. Kayumba wana-possibility kubwa sanaa ya kuja kufanya vizuri iwapo hawatozembea. Sizisemi vibaya shule za private lakini ninao ushuda wa jamaa wawili waliomalizaga St. Lakini walipokuja kujiunga kwenye St kayumba matokeo ya Six walizungusha. Nilishangaa sanaaa.
Ndugu yangu usitafute kichaka kabisaa kama una uwezo somesha mtoto Ems kama huna sawa peleka tu huko mwakinyumbi primary suala ni uwezo tu tusilete janja janja
 
Ndugu yangu usitafute kichaka kabisaa kama una uwezo somesha mtoto Ems kama huna sawa peleka tu huko mwakinyumbi primary suala ni uwezo tu tusilete janja janja
Ki-ukweli sizikandii kabisa EMS hata kidogo, nazikubali kwa asilimia kubwa sanaa. Ila nilipofika chuo ndo nilipokutana na maajabu waliokuwa wanakimbiza almost walikuwa wametoka St Kayumba, wengi wa waliotoka Private walikuwa wababaishaji. Sass sijui nini hutokea hapo katikati
 
Back
Top Bottom