NEC: Uchaguzi mdogo Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini kufanyika Januari 13, 2018. Je, Kitila kumrithi Nyalandu?

Natabiri Chadema watashiriki Uchaguzi huu Halafu Matokeo yakitangazwa wanasingizia Hujuma
 
Chadema wangeacha tu, kwa jinsi ninavyo wafahamu ccm hawawezi kuruhusu nyarandu arudi bungeni tena watamng'ang'ania huko jimboni hata kwa kumuibia kura asirudi
Nyalandu alikua ccm miaka mingapi asizijue mbinu za ccm kuiba kura na jinsi ya kuzizuia??kama hajui ama haelewi wizi wa kura unafanyikaje basi hilo ni galasa halina mchango wowote
 
Ingekuwa mm ndo Mwenyekiti wa Chadema nisingempa apeperushe bendera ya chama hope kuna mgombea wa 2015 aliyepambana na Nyalandu ningemkabidhi apeperushe benderaaa hawa watu wanaohamaham siyo wa kuaminiwa kabisa........
Umeongea ukweli usio chembe ya unafiki
 
Yani nyie mnachekesha kweli kitila mkumbo akagombee kwenye jimbo ambalo wakaazi wote ni kabila la kinyaturu..mnyiramba hawezi kupewa hata wiweje labda wafanye kama ilivyokuwa kwa madiwani watangaze asiyeshinda kwa nguvu!
 
Eti Kitila Mkumbo atoke kwao Ndago Iramba Magharibi atembee Kilomita zaidi ya 120 kuja kugombea Ubunge Singida Kaskazini kwa Wanyaturu....msituchukulie poa basi, kumbukeni Mnyaturu mmoja alishawatoa jasho hadi mkapiga risasi 38 na bado hakufa, can't you pipo learn???
 
Mi nacho shauri upinzani msishiriki kwa sababu matokeo yashajulikana fanyeni.uanaume kama wa Raila odinga
 
John Mmbaga:
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) IMETANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO KATIKA MAJIMBO YA UCHAGUZI YALIYOWAZI PAMOJA NA KATA KAMA IFUATAVYO:-

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya Uchaguzi Mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika tarehe 13 Januari mwaka 2018.

Akitoa taarifa kwa umma jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Mhe. Jaji Mkuu (Mst. Zanzibar) Hamid Mahmoud Hamid, alisema Tume imetangaza uchaguzi huo kufuatia kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuwepo nafasi wazi ya jimbo la Singida Kaskazini kufuatia kuvuliwa uanachama wa CCM mbunge wa jimbo hilo Lazaro Nyalandu na hivyo kupoteza sifa ya kuwa mbunge.



Kwa upande wa Jimbo la Songea Mjini, Jaji Mst. Hamid alisema kuwa Spika aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi ya jimbo hilo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Leonidas Gama huku Tume ikipokea Hati ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ikithibitisha kuwa Jimbo la Longido kuwa wazi baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo.



Aliongeza kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi za madiwani katika kata sita Tanzania Bara.


Mhe. Jaji Mst. Hamid alizitaja kata zinazohusika katika uchaguzi huo kuwa ni Kimandolu (Halmashauri ya Jiji la Arusha), Kihesa (Halmashauri ya Manispaa ya Iringa), Bukumbi (Halmashauri ya Wilaya ya Uyui), Kurui (Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe), Keza (Halmashauri ya Wilaya ya Ngara) na Kwagunda (Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe).

Alisema utoaji fomu za uteuzi katika majimbo hayo na kata hizo sita utakuwa ni kati ya tarehe 12 hadi 18 Desemba, 2017 wakati katika jimbo la Songea Mjini utoaji fumo utakuwa kati ya tarehe 14 hadi 20 Desemba, 2017.

“Uteuzi wa wagombea katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido na kata za Keza, Kimandolu, Kwagunda, Bukumbi, Kurui na Kihesa utafanyika tarehe 18 Desemba, 2017 na uteuzi wa wagombea katika jimbo la Songea Mjini utafanyika tarehe 20 Desemba, 2017” alisema Jaji Mst. Hamid.

Alifafanua kuwa kwa upande wa kampeni za uchaguzi huo katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido na kata zote sita zitaanza tarehe 19 Desemba, 2017 na kumalizika tarehe 12 Januari, 2018.

Katika jimbo la Songea Mjini, alisema kuwa kampeni za zitaanza tarehe 21 Desemba, 2017 na kumalizika tarehe 12 Januari, 2018 wakati siku ya uchaguzi katika majimbo yote matatu na kata zote sita itakuwa tarehe 13 Januari, 2018.

Mhe. Jaji Mst. Hamid alivikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi wazingatie Sheria, Kanuni, Taratibu, Miongozo na Maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo wa majimbo hayo na kata Sita.



Mwisho
 
Nitashangaa sana kama Chadema watakubali kushiriki uchaguzi huu.

Namshauri Nyalandu atunze heshima yake ajiweke pembeni na ubatili huu.

Tunawapa onyo Chadema, mkishiriki uchaguzi huu Freeman Mbowe jiandae kutujuwa invisibles, tutakung'owa hata kwa mapanga kwenye hiyo nafasi yako.

Wewe Mbowe utakuwa ni sehemu ya wasaliti wa Taifa hili.

Movement iliyopo sasa tunataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Freeman Mbowe ukienda kinyume na hili tutakushikisha adabu.

Tunakuamini, usinaswe na huu mtego wa maccm.
Mkuu ukisusa wenzio wanakula, sasa sijui utakuwa umemkomoa nani? Hapa watafute njia ya kupambana na POLISI na UVCCM! Pia kuna huu ujinga wa kuwanyima barua mawakala wa vyama vya upinzani! Hapo red brigade wajiandae kuwateka ma-DED wanaofanya ujinga huo!
 
Kwa sasa ccm inanunua diwani kati ya million 20 - 25 na wabunge ni kati ya 50-100 milioni. Slave trade again
 
Kwa gharama tu jimbo moja uchaguzi ni mil 250 .. ifikie kipindi hawa wanaohama au kuacha walipe hizi gharama au kutokufanya uchaguzi kabisa... ili iwe fundiaho kwa sisi wapiga kura kuchagua watu wasio na misimamo.... tena ikibidi kuwa na sheria kabisa.. . Hizo mil 250 zingetumika kugawa mikopo kwa kila jimbo nafikili tungefika mbali sana.. ..
 
KULIKO KUPOTEZA FEDHA NYINGI KATIKA UCHAGUZI NI BORA.....

MAJIMBO YA.....

SINGIDA KASKAZINI.

LONGIDO..........

SONGEA MJINI.......

KINONDONI

TUME YA UCHAGUZI IKAMTANGAZA ALIYESHIKA NAFASI YA PILI KATIKA UCHAGUZI WA 2015 NDIO MBUNGE HALALI WA JIMBO.
 
Kwa sasa ccm inanunua diwani kati ya million 20 - 25 na wabunge ni kati ya 50-100 milioni. Slave trade again
Mkuu mbona 2015 Lowassa alifanikiwa kuinunua Chadema yote tena kwa dau zuri. Wanasiasa wengi wanatanguliza maslahi yao huwa nawaonea huruma sana Wafuasi, Mashabiki, Wapambe na Wananchi wa Kawaida. Maana haya Makundi niliyoyataja huwa yanapenda pale wasipopendwa.
 
Hapa issue ni katiba tu Kwa wale waliosoma PPR POLITICAL SCIENCE ..wataelewa yaani ikifikia issue kama hizi mbunge kafariki au kajiuzuru..basi yule mbunge ambaye alikuwa kamfuata upande wa kura nyingi basi ndio apewe kiti kukwepa gharama za uchaguzi.. naamini tume ingemtangaza kama mbunge mpya. Kwani amechaguliwa na majority.. na ndio maana hata kwenye usahili huwekwa reserve wa baadae baada ya kuitwa kazini wale wasio report au kunapokuwa na uhaba wa wafanyakazi..
 
Back
Top Bottom