NEC: Uchaguzi mdogo Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini kufanyika Januari 13, 2018. Je, Kitila kumrithi Nyalandu?

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,661
21,645
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika Januari 13 mwakani(2018).

Katika majimbo hayo matatu ni jimbo moja pekee ambalo tayari limepata mgombea .Lazaro Nyalandu atagombea jimbo hilo kupitia CHADEMA.

Je atakutana na nani kutoka CUF, NCCR, ACT na CCM? Je atashinda? Vipi akishindwa ataomba kurudi CCM na kusema CHADEMA haina nia ya kushika dola?

=======

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika Januari 13 mwakani.

Akitoa taarifa kwa umma jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid amesema tume imetangaza uchaguzi huo baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika ya kwamba nafasi ziko wazi.

Jimbo la Singida Kaskazini liko kutokana na kujivua uanachama wa CCM aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Lazaro Nyalandu, Songea Mjini baada ya kifo cha Leonidas Gama na Longido baada ya Mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yamempa ushindi Onesmo Ole Nangole.

Akizungumzia uchaguzi wa kata sita amesema waziri mwenye na serikali za mitaa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi za madiwani katika kata hizo Tanzania Bara

Alizitaja kata zinazohusika katika uchaguzi huo kuwa ni Kimandolu(Arusha), Kihesa (Iringa), Bukumbi (Uyui), Kurui (Kisarawe), Keza (Ngara) na Kwagunda (Korogwe).

Amesema utoaji fomu za uteuzi katika majimbo hayo na kata hizo sita utakuwa ni kati ya Desemba 12 hadi 18, 2017 wakati katika jimbo la Songea Mjini utoaji fumo utakuwa kati ya Desemba 14 hadi 20 mwaka huu.

Alifafanua kuwa kwa upande wa kampeni za uchaguzi huo katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido na kata zote sita zitaanza Desemba 19 na kumalizika Januari 12.

Katika jimbo la Songea Mjini, amesema kuwa kampeni za zitaanza tarehe 21 Desemba, 2017 na kumalizika tarehe 12 Januari, 2018 wakati siku ya uchaguzi katika majimbo yote matatu na kata zote sita itakuwa tarehe 13 Januari, 2017.

Jaji Hamid alivikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi wazingatie sheria, kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo wa majimbo hayo na kata sita.


Chanzo: Mwananchi
 
Nitashangaa sana kama Chadema watakubali kushiriki uchaguzi huu.

Namshauri Nyalandu atunze heshima yake ajiweke pembeni na ubatili huu.

Tunawapa onyo Chadema, mkishiriki uchaguzi huu Freeman Mbowe jiandae kutujuwa invisibles, tutakung'owa hata kwa mapanga kwenye hiyo nafasi yako.

Wewe Mbowe utakuwa ni sehemu ya wasaliti wa Taifa hili.

Movement iliyopo sasa tunataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Freeman Mbowe ukienda kinyume na hili tutakushikisha adabu.

Tunakuamini, usinaswe na huu mtego wa maccm.
 
Kwenye hizo chaguzi Chadema ikishiriki kindakindaki basi kina watu wengi watakufa na kufungwa. Pili upinzani utashinda Ila Mshindo atatangazwa wa ccm tu. Ushauri, Chadema ishiriki ili kupata platform ya kukutana na wananchi na kuwaeleza ccm ilivyo over , wasijali sana ushindi maana kichaa kapewa rungu na familia zenu viongozi cdm zinawahitaji.
 
Nitashangaa sana kama Chadema watakubali kushiriki uchaguzi huu.

Namshauri Nyalandu atunze heshima yake ajiweke pembeni na ubatili huu.

Tunawapa onyo Chadema, mkishiriki uchaguzi huu Freeman Mbowe jiandae kutujuwa invisibles, tutakung'owa hata kwa mapanga kwenye hiyo nafasi yako.

Wewe Mbowe utakuwa ni sehemu ya wasaliti wa Taifa hili.

Movement iliyopo sasa tunataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Freeman Mbowe ukienda kinyume na hili tutakushikisha adabu.

Tunakuamini, usinaswe na huu mtego wa maccm.
Naunga mkono hoja 100%.... Mbowe akiingiza timu uwanjani atajustify ushindi wa CCM wa wizi na ni ujinga kushiriki hku ukijua hutotangazwa mshindi
 
kama ni kweli chadema wamemsimamisha atashinda kazi ni kutangazwa na tume baada ya kushinda.ilanasikitika baadhi ya watu wakipoteza maisha au kubaki vilema siku hiyo kwasabau ya jeshi la polisi kuhakikisha mteule wa ccm akisimikwa kwa nguvu
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika Januari 13 mwakani
Katika majimbo hayo matatu ni jimbo moja pekee ambalo tayari limepata mgombea .Lazaro Nyalandu atawakilisha jimbo hilo kupitia Chadema.
Je atakutana na nani kutoka Cuf,NCCR ,ACT na CCM,Je atashinda?vipi akishindwa ataomba kurudi CCM na kusema CHADEMA haina nia ya kishika dola?
nyarandu kashuka kwenye daradara sasa ni karai jipya lina subiri kubeba zege kwenda 2020
 
Ingekuwa mm ndo Mwenyekiti wa Chadema nisingempa apeperushe bendera ya chama hope kuna mgombea wa 2015 aliyepambana na Nyalandu ningemkabidhi apeperushe benderaaa hawa watu wanaohamaham siyo wa kuaminiwa kabisa........

Nyalandu kafanya Kama Lowassa, kalipia kabisa fees ya kugombea Ubunge
 
Back
Top Bottom