Nebukadneza: Mbabe wa vita, muabudu sanamu aliyekula majani kama ng’ombe

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,822
5,434
Kabla sijakuandikia stori ya huyu mwamba wa Babeli katika nchi ya Babiloni, ngoja nijaribu na mimi kujiuliza maswali kadhaa. Watu wanasema wale Waisrael wa zamani sio wa sasa hivi, hao wa zamani walikwenda wapi?

Wakati wa nyakati za mwisho tunaambiwa kwamba Waisrael wote duniani watarudi nchini kwao. Yaani woooote, hakutokuwa na Muisrael yeyote yule ambaye atabaki nchi nyingine. Na hii ndiyo sababu inayowafanya kuwapiga Waarabu na kuchukua sehemu ya nchi zao kwa kuwa wanajua mwisho wa siku wale wenzao zaidi ya milioni 16 lazima warudi nyumbani.

Sasa wakisharudi wote na kukosekana Muisrael mwingine nje ya taifa lao, hapo ndipo mataifa yote yatapigana na hawa majamaa. Watapigwa vibaya mno mpaka kukimbilia kwenye ule mlima aliopaa Yesu na kisha kushuka, na mwisho wa dunia ndivyo utakavyokuwa.

Sasa najiuliza tu. Kama Waisrael hawa si wale, kwamba hawapo tena, hawa ambao Biblia imewaandika wote watarudi, ni akina nani? I don’t know.

Okay! Tuje mdogo mdogo tusome mambo tupanue ubongo wetu. Unapowasikia Waisrael jua kwamba hilo taifa limekuwa likipigana vita tangu miaka ya zamani, tena zaidi ya nchi yoyote ile.

Ili Israel iwe sehemu salama ilikuwa ni lazima kupigana vita. Wamepigana vita zaidi ya elfu kumi, kuna walizoshinda na kuna walizopigwa vibaya. Hili taifa linapenda vita, yaani wakisikia watu wanataka kupigana nao, ndiyo kwanza wanafurahi.

Wamelelewa hivyo tangu kipindi cha akina Abraham. Wanapenda vita kuliko kula, yaani wakilala, wanawaza vita, wakiamka wanawaza vita. Na kubwa zaidi huwa vita vyao havichagui, wanaua wanawake na watoto, hawa hawachagui hata kidogo.

Ukisoma Biblia, zamani wafalme walikuwa wakiambiwa na mitume kwamba nendeni nchi fulani, pigeni nchi nzima, msiache mtu ama mmea wowote umesimama, hakikisha mnaua wanawake mpaka watoto. Na wakifika huko walikuwa wakiua nchi nzima, hata mtoto anayetambaa, walikuwa wanamdedisha. Yalikuwa ni maagizo kutoka juu.

Sasa jamani mnapoona Israel anapigana vita na kuua watoto na wanawake, hakuanza leo, ilikuwa tangu miaka hiyo ya nyuma, ni vita ambayo walizoea kupigana, hakushangai kwenye Biblia, tunakuja kushangaa sasa hivi.

Tuachane na hayo, kuna siku nitakuja na stori yao ndeeeefuuuuuu.

Tuje kwa huyu mwamba wa kuitwa Nebukadneza. Unapowazungumzia wafalme waliokuwa na nguvu kubwa, basi bila shaka hutoweza kulisahau jina la mwamba mmoja hivi wa kuitwa Nebukadneza.

Huyu jamaa alikuwa mtawala kipindi kile cha akina Daniel. Nenda kasome Daniel sura ya 1 mpaka ya 4, imemuelezea sana mfalme huyu kwa namna alivyokuwa na nguvu, Mungu alikuwa anamuonyesha mambo yajayo kwa kupitia ndoto, halafu Daniel ndiye akawa mtafsiri.

Tuje sasa. Huyu jamaa ametoka wapi?

Baba wa mfalme huyu aliitwa Nabopolaan. Huyu alikuwa mflame wa 65 wa nchi iitwayo Babiloni ambayo ilikuwa na mji wake uitwao Babeli. Sasa miaka hiyo mfalme huyu alikuwa kwenye mapigano makali ya Misri, kwa nini? Walikuwa wanagombania milki ya Ashuru, yaani kama leo hii Morocco na Algeria wasivyopatana kisa tu kuna maeneo Morocco anayatawala kimabavu na Algeria wakiamini hayo ni maeneo yao.

Sasa baba yake alipofariki dunia, Nebukadneza akaanza kutawala Babiloni na kuingia kwenye vita yake ya kwanza na Misri, vita hivyo vilikwenda kupiganiwa huko Eufrate katika utawala wa mwisho wa baba yake, hiyo ilikuwa ni mwaka 605 Kabla ya Kristo.

Wakati huo Misri ilikuwa na mfalme wao, Farao-Neto lakini alijikuta yeye na majeshi yake wakiangukia pua kwa kuchakazwa vibaya sana na Babiloni.

Hiyo vita haikupiganiwa Eufrate tu bali walihama na kwenda kupigania sehemu nyingine iitwayo Karkemishi katika mto Eufrate. Unaweza kusoma kitabu cha Yeremia 46:2.

Sasa hapa nakupa mambo mawili, historia kulingana na Biblia, halafu historia kulingana na vitabu vya darasani. Hapa inabidi nicheze kotekote ili muelewe vizuri.

Sasa kwa nini Babiloni iliamua kumpiga Misri? Kwanza hii ilikuwa ni adhabu ya Mungu, yaani aliona kulikuwa na maovu mengi sana Misri (Hawa jamaa wamepinda tangu zamani), akaamua kumpeleka Nebukadneza kwenda kupigana huko. Soma Yeremia kuanzia sura ya 46.

Lakini sababu ya pili ni kwamba Misri aliitaka miji ya Shamu na Palestina, kwa nini? Miji hiyo ilikuwa karibu na Babiloni na kwa sababu waliona majamaa wanaitawala dunia, basi ingekuwa kazi nyepesi sana kupambana nao kama tu wangeipata miji hiyo.

Sasa naye Babiloni hawakutaka kuona hilo linatokea. Wakapambana vilivyo mpaka kushinda vita hivyo. Wakati Nebukadneza anapambana kwenye vita ndipo akapokea taarifa kwamba mshua wake amekufa hivyo ilikuwa ni lazima kurudi nyumbani na kusimikwa kuwa mfalme.

Nebukadneza alikuwa mjanja sana. Yaani alikuwa akipambana na Wamisri ili wasichukue Palestina na Shamu lakini wakati huohuo alikuwa akipigana na watu wa mji huo ili awatawale.

Alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, na baada ya hapo, sasa akaamua kwenda huko Yuda ili kupigana na mfalme Yehoyakimu. Unaposema taifa la Yuda, inamaana ya Israel. Akaona hiyo haitoshi, akaufuata mji wa Siria (Syria) na kuupiga na miaka minne baadaye akarudi kupigana na Wamisri.

Hii ita hakushinda, na hata Wamisri hawakushinda. Sasa hilo likawapa viburi watu wengine na kuona mbona kama na sisi tunamuweza jamaa? Kwa nini tusmfuate na kumkung’uta?

Mtu wa kwanza kuwa kimbelembele na kuonyeshwa mfano alikuwa Yuda (Israel) alipoleta kukukakara zake, akapigwa vibaya mno na wakamteka mfalme Yehoyakini, halafu pale akampandikiza mfalme aliyemtaka yeye aliyeitwa Sedekia. Najua kwa Wakristo haya majina si mageni kwenu.

Miaka ilikwenda mbele, mataifa yalitaka kujitoa katika utawala wa Babeli lakini walishindwa kwa sababu majamaa walikuwa hatari wa vita.

Watu wakapitisha ndogondogo kwa mfalme wa Yuda, Sedekia na kumwambia mbona alijisahau mbaba? Kwa nini ulipe ushuru mkubwa kwa Babeli na wakati hata wewe unaweza kujinasua, alienda kupigana na Misri, ngoma droo, wewe unamshindwaje? Mpige umuondoe nchini kwako! Sedekia akaona poa, acha nimtwange, kuingia vitani tu, akapigwa yeye.

Mji wa Yerusalemu ukawa under attack, jamaa akaingia hekaluni, akachukua vyombo vya dhahabu vya humo ambavyo Wayuda walikuwa wakivitumia kwenye ibada zao (Hivi vyombo vilimletea shida sana mfalme Belshaza ambaye ni mtoto wa Nebukadneza). Akawateka watu, akamuua Sedekia, halafu nchi ya Yuda akaifanya kuwa mkoa na si nchi tena.

Sasa miongoni mwa mateka waliochukuliwa ndiyo walikuwepo akina Daniel, Shadraki na Abedenego

Sijui unapata picha hapo.

Yaani ukisoma Bible, halafu ukasoma na haya masomo ya darasani ya historia, unaanza kupata mambo mengi zaidi.

Itaendelea.
 
Kabla ya mwaka 1947, hakukuwa na nchi ama sehemu yoyote pale Duniani ikiyoitwa Israel! Israel ilianza kuitwa mwaka 1947.

Ata Yesu kipindi yupo hakukuwa na sehemu ikiitwa Israel pale mashariki ya kati, ata kipindi Abraham yupo hakukuwa na sehemu ikiitwa Israel pale mashariki ya kati.
 
Mwamba aligeuka mnyama wa mwituni akala majani kama punda mwitu kwa miaka 7, alipopona akanyoosha mikono akasema NIMEKUBALI! Mungu yupo na Ndiye anayetawala!. Picha linakuja akaja mfalme mwingine akajidai kuleta kiburi badala ya kujifunza kwa babaye! Mara paap! Mikono hiyoo (haijulikani imetoka wapi!) Ikapiga chata ukutani "MENE, MENE, TEKELI NA PERESI"... maana yake Imeisha hiyo....😄😄😄
 
Alikubali Mungu gani mkuu? Maana Mungu wa Wayahudi wala sio Mungu unamuamini wewe Mkristo. Tazama njia zenu za kumfikia huyo Mungu mnavyotafautiana pakubwa.
 
Kabla ya mwaka 1947, hakukuwa na nchi ama sehemu yoyote pale Duniani ikiyoitwa Israel! Israel ilianza kuitwa mwaka 1947.

Ata Yesu kipindi yupo hakukuwa na sehemu ikiitwa Israel pale mashariki ya kati, ata kipindi Abraham yupo hakukuwa na sehemu ikiitwa Israel pale mashariki ya kati.
Kàbla ya Mwaka 1947 hakukuwepo Taifa hilo ni kwa sababu walikuwa wametawanyika, na wengine kuuwawa na Adolph Hitler...

Biblia imetaja mara kadhaa kuhusu uwepo wa taifa la Israel ambao kimsingi ndio wayahudi (Jews).

Hapa kuna orodha ya mistari michache kati ya mingi katika Biblia inayozungumzia uwepo wa taifa la Israeli:

1. Mwanzo 12:1-3 - Ahadi kwa Ibrahimu kuhusu taifa la Israeli.
2. Kutoka 3:7-10 - Mungu anamwita Musa kuwaokoa Waisraeli kutoka utumwani Misri.
3. Kumbukumbu la Torati 30:1-5 - Ahadi ya Mungu kurejesha Israeli kutoka uhamishoni.
4. Yoshua 1 - Yoshua alichukua uongozi wa Waisraeli kuwaingiza katika Nchi ya Ahadi.
5. 2 Mambo ya Nyakati 6:14-42 - Maombi ya Sulemani kwa ajili ya taifa la Israeli.
6. Zaburi 136 - Sifa kwa Mungu kwa kumwongoza taifa la Israeli.
7. Isaya 43:1-7 - Ahadi ya Mungu ya kuwalinda Waisraeli.
8. Yeremia 30:1-3 - Mungu asema atawakusanya Waisraeli kutoka mataifa yote na kuwarudisha katika nchi yao.
9. Ezekieli 37:15-28 - Maono ya mifupa inayohusiana na kuunganisha taifa la Israeli.
10. Amosi 9:11-15 - Ahadi ya Mungu ya kurejesha Israeli kutoka uhamishoni na kurejenga tena falme zao.
 
Alikubali Mungu gani mkuu? Maana Mungu wa Wayahudi wala sio Mungu unamuamini wewe Mkristo. Tazama njia zenu za kumfikia huyo Mungu mnavyotafautiana pakubwa.
Swala sio kutofautiana kwa sababu hata wakristo wenyewe wanatofautiana kumfikia Mungu... Mroma na Mpentekoste wanasali tofauti kabisa ila wote ni wakristo.

Wakristo wanaamini wayahudi ni bloodline ya mitume, na Yesu alikuwa myahudi. Sasa wewe unataka kulazimisha unachokiamini wewe na wakristo wakiamini.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Kuna utofauti wa maana kati ya haya majina mawili???? 👇

1. Nebukadneza
2.Nebukadreza
 
Interesting 🤔, ukiendeleza naomba uni tag mkuu. Najua sio rahisi kuni tag but nitafurahi kama utani tag
 
Kuna utofauti wa maana kati ya haya majina mawili???? 👇

1. Nebukadneza
2.Nebukadreza
Jina la mfalme wa Babylonia ambaye alitawala katika karne ya 6 KK ni Nebukadneza.

Hilo jina Nebukadreza labda ni kutokana na kukosea matamshi tu
 
Kabla sijakuandikia stori ya huyu mwamba wa Babeli katika nchi ya Babiloni, ngoja nijaribu na mimi kujiuliza maswali kadhaa. Watu wanasema wale Waisrael wa zamani sio wa sasa hivi, hao wa zamani walikwenda wapi?

Wakati wa nyakati za mwisho tunaambiwa kwamba Waisrael wote duniani watarudi nchini kwao. Yaani woooote, hakutokuwa na Muisrael yeyote yule ambaye atabaki nchi nyingine. Na hii ndiyo sababu inayowafanya kuwapiga Waarabu na kuchukua sehemu ya nchi zao kwa kuwa wanajua mwisho wa siku wale wenzao zaidi ya milioni 16 lazima warudi nyumbani.

Sasa wakisharudi wote na kukosekana Muisrael mwingine nje ya taifa lao, hapo ndipo mataifa yote yatapigana na hawa majamaa. Watapigwa vibaya mno mpaka kukimbilia kwenye ule mlima aliopaa Yesu na kisha kushuka, na mwisho wa dunia ndivyo utakavyokuwa.

Sasa najiuliza tu. Kama Waisrael hawa si wale, kwamba hawapo tena, hawa ambao Biblia imewaandika wote watarudi, ni akina nani? I don’t know.

Okay! Tuje mdogo mdogo tusome mambo tupanue ubongo wetu. Unapowasikia Waisrael jua kwamba hilo taifa limekuwa likipigana vita tangu miaka ya zamani, tena zaidi ya nchi yoyote ile.

Ili Israel iwe sehemu salama ilikuwa ni lazima kupigana vita. Wamepigana vita zaidi ya elfu kumi, kuna walizoshinda na kuna walizopigwa vibaya. Hili taifa linapenda vita, yaani wakisikia watu wanataka kupigana nao, ndiyo kwanza wanafurahi.

Wamelelewa hivyo tangu kipindi cha akina Abraham. Wanapenda vita kuliko kula, yaani wakilala, wanawaza vita, wakiamka wanawaza vita. Na kubwa zaidi huwa vita vyao havichagui, wanaua wanawake na watoto, hawa hawachagui hata kidogo.

Ukisoma Biblia, zamani wafalme walikuwa wakiambiwa na mitume kwamba nendeni nchi fulani, pigeni nchi nzima, msiache mtu ama mmea wowote umesimama, hakikisha mnaua wanawake mpaka watoto. Na wakifika huko walikuwa wakiua nchi nzima, hata mtoto anayetambaa, walikuwa wanamdedisha. Yalikuwa ni maagizo kutoka juu.

Sasa jamani mnapoona Israel anapigana vita na kuua watoto na wanawake, hakuanza leo, ilikuwa tangu miaka hiyo ya nyuma, ni vita ambayo walizoea kupigana, hakushangai kwenye Biblia, tunakuja kushangaa sasa hivi.

Tuachane na hayo, kuna siku nitakuja na stori yao ndeeeefuuuuuu.

Tuje kwa huyu mwamba wa kuitwa Nebukadneza. Unapowazungumzia wafalme waliokuwa na nguvu kubwa, basi bila shaka hutoweza kulisahau jina la mwamba mmoja hivi wa kuitwa Nebukadneza.

Huyu jamaa alikuwa mtawala kipindi kile cha akina Daniel. Nenda kasome Daniel sura ya 1 mpaka ya 4, imemuelezea sana mfalme huyu kwa namna alivyokuwa na nguvu, Mungu alikuwa anamuonyesha mambo yajayo kwa kupitia ndoto, halafu Daniel ndiye akawa mtafsiri.

Tuje sasa. Huyu jamaa ametoka wapi?

Baba wa mfalme huyu aliitwa Nabopolaan. Huyu alikuwa mflame wa 65 wa nchi iitwayo Babiloni ambayo ilikuwa na mji wake uitwao Babeli. Sasa miaka hiyo mfalme huyu alikuwa kwenye mapigano makali ya Misri, kwa nini? Walikuwa wanagombania milki ya Ashuru, yaani kama leo hii Morocco na Algeria wasivyopatana kisa tu kuna maeneo Morocco anayatawala kimabavu na Algeria wakiamini hayo ni maeneo yao.

Sasa baba yake alipofariki dunia, Nebukadneza akaanza kutawala Babiloni na kuingia kwenye vita yake ya kwanza na Misri, vita hivyo vilikwenda kupiganiwa huko Eufrate katika utawala wa mwisho wa baba yake, hiyo ilikuwa ni mwaka 605 Kabla ya Kristo.

Wakati huo Misri ilikuwa na mfalme wao, Farao-Neto lakini alijikuta yeye na majeshi yake wakiangukia pua kwa kuchakazwa vibaya sana na Babiloni.

Hiyo vita haikupiganiwa Eufrate tu bali walihama na kwenda kupigania sehemu nyingine iitwayo Karkemishi katika mto Eufrate. Unaweza kusoma kitabu cha Yeremia 46:2.

Sasa hapa nakupa mambo mawili, historia kulingana na Biblia, halafu historia kulingana na vitabu vya darasani. Hapa inabidi nicheze kotekote ili muelewe vizuri.

Sasa kwa nini Babiloni iliamua kumpiga Misri? Kwanza hii ilikuwa ni adhabu ya Mungu, yaani aliona kulikuwa na maovu mengi sana Misri (Hawa jamaa wamepinda tangu zamani), akaamua kumpeleka Nebukadneza kwenda kupigana huko. Soma Yeremia kuanzia sura ya 46.

Lakini sababu ya pili ni kwamba Misri aliitaka miji ya Shamu na Palestina, kwa nini? Miji hiyo ilikuwa karibu na Babiloni na kwa sababu waliona majamaa wanaitawala dunia, basi ingekuwa kazi nyepesi sana kupambana nao kama tu wangeipata miji hiyo.

Sasa naye Babiloni hawakutaka kuona hilo linatokea. Wakapambana vilivyo mpaka kushinda vita hivyo. Wakati Nebukadneza anapambana kwenye vita ndipo akapokea taarifa kwamba mshua wake amekufa hivyo ilikuwa ni lazima kurudi nyumbani na kusimikwa kuwa mfalme.

Nebukadneza alikuwa mjanja sana. Yaani alikuwa akipambana na Wamisri ili wasichukue Palestina na Shamu lakini wakati huohuo alikuwa akipigana na watu wa mji huo ili awatawale.

Alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, na baada ya hapo, sasa akaamua kwenda huko Yuda ili kupigana na mfalme Yehoyakimu. Unaposema taifa la Yuda, inamaana ya Israel. Akaona hiyo haitoshi, akaufuata mji wa Siria (Syria) na kuupiga na miaka minne baadaye akarudi kupigana na Wamisri.

Hii ita hakushinda, na hata Wamisri hawakushinda. Sasa hilo likawapa viburi watu wengine na kuona mbona kama na sisi tunamuweza jamaa? Kwa nini tusmfuate na kumkung’uta?

Mtu wa kwanza kuwa kimbelembele na kuonyeshwa mfano alikuwa Yuda (Israel) alipoleta kukukakara zake, akapigwa vibaya mno na wakamteka mfalme Yehoyakini, halafu pale akampandikiza mfalme aliyemtaka yeye aliyeitwa Sedekia. Najua kwa Wakristo haya majina si mageni kwenu.

Miaka ilikwenda mbele, mataifa yalitaka kujitoa katika utawala wa Babeli lakini walishindwa kwa sababu majamaa walikuwa hatari wa vita.

Watu wakapitisha ndogondogo kwa mfalme wa Yuda, Sedekia na kumwambia mbona alijisahau mbaba? Kwa nini ulipe ushuru mkubwa kwa Babeli na wakati hata wewe unaweza kujinasua, alienda kupigana na Misri, ngoma droo, wewe unamshindwaje? Mpige umuondoe nchini kwako! Sedekia akaona poa, acha nimtwange, kuingia vitani tu, akapigwa yeye.

Mji wa Yerusalemu ukawa under attack, jamaa akaingia hekaluni, akachukua vyombo vya dhahabu vya humo ambavyo Wayuda walikuwa wakivitumia kwenye ibada zao (Hivi vyombo vilimletea shida sana mfalme Belshaza ambaye ni mtoto wa Nebukadneza). Akawateka watu, akamuua Sedekia, halafu nchi ya Yuda akaifanya kuwa mkoa na si nchi tena.

Sasa miongoni mwa mateka waliochukuliwa ndiyo walikuwepo akina Daniel, Shadraki na Abedenego

Sijui unapata picha hapo.

Yaani ukisoma Bible, halafu ukasoma na haya masomo ya darasani ya historia, unaanza kupata mambo mengi zaidi.

Itaendelea.
Ok
 
Back
Top Bottom