Ndugu zangu, muda mwingine sisi wenyewe tunawapa nafasi maadui zetu watudhuru

Habari za jumapili wadau? Tunaishi kwenye jamii ambazo hazipendi kuona wengine wakifanikiwa.

Wengi wetu tumekuwa tukipenda kuweka wazi mipango yetu, hasa kwenye social network, WhatsApp, insta etc.

Sijui lengo huwa ni nini? Kuwaringishia wengine au kuwahamasisha wengine.

Nina mkasa wa rafiki yangu ambaye tulikuwa tukifanya kazi pamoja, ni mwanaume, ila alipenda sana kushare mipango yake WhatsApp status.

Watoto wake wakiwa wanaenda shule ataposti wakiwa wanapanda gari, ( school bus).

Hata alipoenda kununua kiwanja alipost, nimenunua kiwanja, hata alipoanza ujenzi alpost gari likibeba matofali.

Akaanza kujenga msingi wa nyumba akapost, huwezi amini nyumba ilikomea kwenye msingi, balaa sijui lilitokea wapi alifukuzwa kazi.

Minong’ono ilianza baada ya kufukuzwa kazi ngoja tuone sasa, si alikuwa anaringa, maisha yalibadilika ghafla watoto akawatoa private akawaleta santi kayumba, kazi kupata ikawa ngumu kicha ya elimu aliyonayo.

Usafiri ameuza, sasa hivi anagongea vibarua vya ujenzi ili familia iishi, mara nyingi nakaa nae anajiuliza ni wapi nimekosa mimi? Nabikia kumtia tu moyo ni mapito tu haya.

Ndugu zangu mipango yako ni ya kwako, haina faida yeyote wengine waijue, jamii zetu nyingi ni za kinafiki tunafuatiliana sana, hivyo kama utakuwa mtu wa kuweka wazi mipango yako nakupa pole.
Wenzake wakifanya show off wanakua wamezindikwa yeye anafanya show off mweupe utadhani haijui jamii yetu ya kitanzania.
 
Mimi sio mtu wa kupost mishe zangu, ila siezi kataza watu wasipost mambo yao kwa kuhofia kwamba one day wataanguka.

Kama mtu anafurahia jambo fulani na anataka kushare na company yake mbona safi tu.
Hayo maisha usifanyie bongo au Africa. Lasivyo utapigwa majuju mpk ukome 🤣
 
Habari za jumapili wadau? Tunaishi kwenye jamii ambazo hazipendi kuona wengine wakifanikiwa.

Wengi wetu tumekuwa tukipenda kuweka wazi mipango yetu, hasa kwenye social network, WhatsApp, insta etc.

Sijui lengo huwa ni nini? Kuwaringishia wengine au kuwahamasisha wengine.

Nina mkasa wa rafiki yangu ambaye tulikuwa tukifanya kazi pamoja, ni mwanaume, ila alipenda sana kushare mipango yake WhatsApp status.

Watoto wake wakiwa wanaenda shule ataposti wakiwa wanapanda gari, ( school bus).

Hata alipoenda kununua kiwanja alipost, nimenunua kiwanja, hata alipoanza ujenzi alpost gari likibeba matofali.

Akaanza kujenga msingi wa nyumba akapost, huwezi amini nyumba ilikomea kwenye msingi, balaa sijui lilitokea wapi alifukuzwa kazi.

Minong’ono ilianza baada ya kufukuzwa kazi ngoja tuone sasa, si alikuwa anaringa, maisha yalibadilika ghafla watoto akawatoa private akawaleta santi kayumba, kazi kupata ikawa ngumu kicha ya elimu aliyonayo.

Usafiri ameuza, sasa hivi anagongea vibarua vya ujenzi ili familia iishi, mara nyingi nakaa nae anajiuliza ni wapi nimekosa mimi? Nabikia kumtia tu moyo ni mapito tu haya.

Ndugu zangu mipango yako ni ya kwako, haina faida yeyote wengine waijue, jamii zetu nyingi ni za kinafiki tunafuatiliana sana, hivyo kama utakuwa mtu wa kuweka wazi mipango yako nakupa pole.
Perfect content.
 
Ujaelewa uzi kaka
Mipango inatakiwa kifanyika sirini watu waone matokeo
Same kwa hao uliowataja unajua strategic ambazo zipo kichwani mwa elon musk,mo na dangote
Elon Musk ana mpango wa kwenda mars na dunia nzima inajua.
Halogeki?

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Africa unaweza zimwa hata kwa kuhisiwa tu.
Ninyi mnaishi Africa ipi.
Yani uanze kupata hela alafu watu wasijue.
 
Naelewa huwezi jua kila kitu kilichopo kwenye mawazo ya mtu, hata mtu akipost Kanunua kiwanja hatujui hela alipataje , huenda kapost kumotivate wengine so watakao amua kuchukia ni juu yao.

Binafsi nakubali kuwa wapo watu wasiofurahishwa na mafanikio ya wengine, ila siamini kama mtu anaweza kuzuia baraka zisikufikie kisa ameona unamaendeleo.

If it was meant to happen, It will happen and the vice verse is true.
Kuwa msiri mkuu dunia hii ina mambo ya kutisha.

Mafanikio yako huleta majeraha kwa wengine(umekiri mwenyewe),baraka ni intangible kwa matomaso.

Vipi kuhusu majambazi na vibaka wakiona umeposti mbongotee watafurahia au watakutafuta then waokote na wakutoe roho ili mchezo wa kupost ukuishe.
 
Attachments

  • IMG-20250216-WA0001.jpg
    IMG-20250216-WA0001.jpg
    66.3 KB · Views: 1

Similar Discussions

Back
Top Bottom