Expensive life
JF-Expert Member
- May 2, 2020
- 2,882
- 9,261
Habari za jumapili wadau? Tunaishi kwenye jamii ambazo hazipendi kuona wengine wakifanikiwa.
Wengi wetu tumekuwa tukipenda kuweka wazi mipango yetu, hasa kwenye social network, WhatsApp, insta etc.
Sijui lengo huwa ni nini? Kuwaringishia wengine au kuwahamasisha wengine.
Nina mkasa wa rafiki yangu ambaye tulikuwa tukifanya kazi pamoja, ni mwanaume, ila alipenda sana kushare mipango yake WhatsApp status.
Watoto wake wakiwa wanaenda shule ataposti wakiwa wanapanda gari, ( school bus).
Hata alipoenda kununua kiwanja alipost, nimenunua kiwanja, hata alipoanza ujenzi alpost gari likibeba matofali.
Akaanza kujenga msingi wa nyumba akapost, huwezi amini nyumba ilikomea kwenye msingi, balaa sijui lilitokea wapi alifukuzwa kazi.
Minong’ono ilianza baada ya kufukuzwa kazi ngoja tuone sasa, si alikuwa anaringa, maisha yalibadilika ghafla watoto akawatoa private akawaleta santi kayumba, kazi kupata ikawa ngumu kicha ya elimu aliyonayo.
Usafiri ameuza, sasa hivi anagongea vibarua vya ujenzi ili familia iishi, mara nyingi nakaa nae anajiuliza ni wapi nimekosa mimi? Nabikia kumtia tu moyo ni mapito tu haya.
Ndugu zangu mipango yako ni ya kwako, haina faida yeyote wengine waijue, jamii zetu nyingi ni za kinafiki tunafuatiliana sana, hivyo kama utakuwa mtu wa kuweka wazi mipango yako nakupa pole.