Ndugu wafidiwe pesa katika mitandao ya simu ikitokea wenye Akaunti zenye salio wameaga dunia

Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
2,426
6,263
Habari ndugu Watanzania,

Nimesukumwa kuandika uzi huu, kutoka kwenye uzi mwingine uliofunguliwa juu ya madai ya mtu kumtumia mzigo mteja wake, na mteja imetokea ameaga dunia kabla ya kupokea mzigo.

Niliwahi kufungua uzi kipindi cha nyuma unaoendana na huu ukiuliza ndugu wanafidiwa vipi maslahi ya salio za ac zao pindi wanapo aga dunia hususani kwenye hii mitandao ya simu ambapo kuna watumiaji wengi kuliko bank.

Kwa mfumo wa sasa ni mpaka ndugu wafatilie au wapate akili ya kufuatilia, ikiwa hawajafuatilia basi pesa za marehemu zinapotelea kwenye mitandao ya simu pasipo familia au wahitaji wa marehemu kufaidika.

Napendekeza yafuatayo yafanyike ili stahiki za ndugu zipatikane na si kunufaisha makampuni yasiyo stahili urithishwaji wa pesa za marehemu.

Mapendekezo yangu.

1. Mtu anapojiunga na MPESA, TIGOPESA, TTCL PESA, AIRTEL MONEY, HALO PESA na AZAM PESA basi sharti kuu moja wapo liwe ni kuweka namba za ndugu wa karibu wasiopungua 5.

2. Ac ya mteja isipokua active kwa mwaka mmoja akumbushwe kufanya miamala aidha iwe kutoa au kuweka pesa kutathmini uhai wa ac ya mteja.

3. Baada ya mteja kukumbushwa kuhusu kufanya miamala ndani ya miezi miezi 3, ikitokea mteja amekua kimya kwa kipindi cha miezi 3, zile namba za ndugu wakaribu zipewe taarifa juu ya uhai wa ac ya mteja itafungwa endapo mteja hatotoa ushirikiano kwa kipindi husika, hapa ndugu wanaweza kumtafuta au kama kuna taarifa zozote za ugonjwa uliopelekea mgonjwa kutoweza kushika simu yake kwa muda mrefu au vifo basi kuwe na namna ya kuwasilisha taarifa ili salio la mteja lirejeshwe kwa wanafamilia kwa taratibu za mirathi.

4. Kiwekwe kiwango maalum ambacho kitaruhusu taratibu zote hizi kufanyika, kwa mfano, huwezi kuwa na salio la 5000 kwenye simu yako lifanye kampuni kusumbuka kwa kiasi chote hicho kutafuta ndugu wa marehemu au mtu aliepotea bila kutumia ac yake. Kiwango kiwe kiasi cha shilingi za kitanzania laki 100,000/= na kuendelea, chini ya hapo zitabaki kuwa mali ya kampuni ya simu, nimesema hivi kwasababu mifumo ya kuwataarifu wateja na kutunza data za wateja ina gharama zake pia lazima kiwango cha thamani ya kuwatafuta ndugu kizingatiwe na kipewe uzito kulingana na salio la mteja.

Nina uhakika kuna pesa nyingi sana za watu zinapotea bila kuwa traced na wanaostahili kunufaika, tupaze sauti hili jambo lifanyiwe kazi.

Na hili liwe applicable kwa huduma zote ambazo mteja anapotokea kupoteza mali au pesa pasipo watu wakaribu kutaarifiwa endapo atakua ameaga dunia.

Karibuni kwa maoni.
 
Ipo hivi Mkuu,

Endapo mtu atafariki basi familia na haswa aliyechaguliwa kusimamia miradhi ana jukumu la kufuatilia mali na madeni yote ya marehemu.

Huko kwenye mitandao ya simu, baada ya kupata idhini yaa kusimamia mirathi basi ataenda kwenye mtandao husika na benki pia. Ataomba Statement na salio lililopo. Kisha salio hilo litahamishwa kwenye akaunti ya msimamizi na kisha akaunti ama line hiyo kufungwa.

Hivyo, badala ya yote hayo basi jamii ielimishwe juu ya namna bora ya kufuatilia mirathi ya mpendwa wao.

Nakupa nyongeza,
Mitandao ya simu wala haibaki na hela za wateja waliotokomea bila taarifa. Bali fedha hizo hukaa na baada ya muda fulani, fedha hizo huwekwa kwenye akaunti maalum serikalini. Ikitokea mdai akajitokeza basi atapatiwa fedha zake. Kama hatotokea, basi hutaifishwa kwa manufaa ya Umma.

Hata hivyo, nawatahadharisha wote. Kuna ujanja na ulaghai mwingi sana hufanyika benki pamoja na huko kwenye mitandao ya simu.

Maafisa wa benki na mitandao yaa simu wasio waaminifu, wakishaona barua ya mirathi, basi hela ya marehemu inapigwa panga. Mfano kwenye akaunti ya benki au simu kuna Million 3, basi unaweza kushtukia unaambiwa kuna laki 9. Nyingine yote itatolewa kwa njia wanazojua wao. Walioacha hela nyingi benki ndiyo hunufaisha zaidi.

Hivyo, kama una line (chip) ya mhusika jaribuni kuitumia walau Tsh 100. Salio litajionyesha na walau mtakuwa na uhakika ni kiasi gani kilichopo ili msijisumbue ama kupigwa na wataalam..

Kwa benki, omba statement ya marehemu. Japo wapo wataalam wa kuzichezea lakini si wote.
 
Ipo hivi Mkuu,

Endapo mtu atafariki basi familia na haswa aliyechaguliwa kusimamia miradhi ana jukumu la kufuatilia mali na madeni yote ya marehemu.
Asante kwa nyongeza, nadhani bado ipo namna ya kuwajulisha ndugu ili kuepuka ujanja wa watumishi wa tasisi za kibenki na mitandao ya simu wasio waaminifu, aidha kwa kutaarifu kiwango halisi cha salio kilichopo kwa ndugu watano wa mtu aliyepotea baada ya muda fulani kupita, kwakua kazi hii itakua inafanywa na mfumo kwa asilimia 95, sioni kama kutakua na uingiliwaji na wale watumishi wajanja wajanja, kwasababu vitu vyote hivi vinakua programmed kwenye mfumo ongozi, ambapo mianya ya kuingiliwa lazima ziwekwe process ndefu.
 
Sio kufa tu hata account za watu ambazo hawajazifuatilia muda mrefu zinapigwa. Imagine acc ya mtu hajacheki salio wala kuweka au kutoa fedha kwa miaka let's say mitano. Naskia branch managers ndo zao, huwa wanazipitia accounts za branch yake akikuta iko dormant anaanza kuifuatilia kwa ukaribu. Ikipita muda anapita nayo. Anatengeneza kadi analink na ile acc anapita na pesa
 
Kuliko utake mitandao Ikuforce uweke namba za ndugu ili wapate gawio kwanini usiandike urithi na kuacha kwa lawyer zenye maelezo yote unayotaka ?!!!

Hii ni kuongeza overheads ambazo hazina ulazima wakati individuals wanaweza kuzifanya wenyewe...
 
Shukrani kwa maoni, nisahihi kabisa ulichosema lakini kama unavyojua kwa mazingira yetu na tamaduni zetu watu wengi hawapo tayari kufanya hivyo, kuna dhana ya kujichuria kifo japo haina uhalisia, lakini ni vyema kufanya kitu ambacho kitalazamisha stahiki ziende kwa wahusika, Hatuna sheria ya kulazimisha watu waandike urithi na hata ikiwekwa sidhani kama itatekelezwa ipasavyo kwa individual level, hivyo basi ni rahisi kutumia mifumo ya kisasa wezeshi kuepukana na mambo ya maamuzi ya mtu binafsi.

1. Kuandika urithi ni uamuzi wa mtu anaweza aandike au asiandike.

2. Mfumo kutambua mali za marehemu au mpotevu unatoa fursa ya kuwapa taarifa ndugu wa karibu lakini haimaanishi wao ndo watakabidhiwa hizo pesa au mali hapana, bali utaratibu wa mirathi utafuatwa kama kawaida lengo hapa ni kuepusha kupotea kwa pesa/stahiki za marehemu pasipo ndugu ama wanafamilia kujua.
 
Ukipeleka mirathi kwenye kampuni za simu na documents zote kwamba wewe ni msimamizi wataangalia amount iliyopo na kukupa accordingly
 
Ukipeleka mirathi kwenye kampuni za simu na documents zote kwamba wewe ni msimamizi wataangalia amount iliyopo na kukupa accordingly
Ewaa sasa unaelekea nilipokusudia, vipi kama marehemu alikua na namba isiyofahamika kwa msimamizi wa mirathi?
au msimamizi wa mirathi asipoenda kabisa, huoni kama waliopata taarifa watatoa shinikizo juu ya ufuatiliaji wa pesa husika na hivyo kusaidia wanufaika halali wapate stahiki zao?
Hapa ndio nimekusudia mkuu, taarifa ziwepo kama wakiamua kwenda au kutokwenda ni juu yao ila taarifa ziwepo.
 
Sio kufa tu hata account za watu ambazo hawajazifuatilia muda mrefu zinapigwa. Imagine acc ya mtu hajacheki salio wala kuweka au kutoa fedha kwa miaka let's say mitano. Naskia branch managers ndo zao, huwa wanazipitia accounts za branch yake akikuta iko dormant anaanza kuifuatilia kwa ukaribu. Ikipita muda anapita nayo. Anatengeneza kadi analink na ile acc anapita na pesa
BOT wayapitie haya mapungufu.
 
Back
Top Bottom