Ndanda vs Yanga kucheza DSM

TUNALETA USHABIKI , HISIA NA MTAZAMO
HASI KATIKA MAMBO AMBAYO NI RAHISI SANA
KUELEWEKA.....
Young Africans imejenga hoja makini ambayo
Ndanda na kamati ya ligi wameiona ina mashiko
na wameridhia .
Kuridhia sio tu kwa utashi binafsi bali kwa
kuchungulia vifungu na kanuni za ligi
zinasemaje ?!! Je kuna katazo la moja kwa moja
au makubaliano hayo yanaruhusiwa?! katiba au
kanuni za ligi hazina muhuri wa katazo hilo iwayo
yote kwa asilimia 100% .
Mambo ambayo yanaweza kufanya kituo cha
mchezo husika kuhamishwa
a. Ubovu wa uwanja
b. Usalama mdogo
c. Miundo mbinu mibovu itakayopelekea kuifanya
timu moja kushindwa kufika kirahisi.
d. Marekebisho ya uwanja ( ujenzi kuendelea)
e. Makubaliano binafsi kati ya timu mwenyeji na
mgeni kuhamisha kituo kwa sababu ambazo za
msingi na zenye ushawishi ( mantiki)
Kagera wamehama kituo chao mara ngapi?!
Mechi za Simba na Yanga ambazo mnasoma
historia zimechezwa Mwanza , Arusha au
Dodoma mnazikua sababu ? ( mechi za ligi kuu/
daraja la kwanza)
Ruvu JKT amehama viwanja vingapi ?! Hakuanzia
mabatini huyu ?! Mlihoji?!
Kwanini Yanga na Simba hawachezi Manungu ,
Mwadui , Karume na Chamazi? . Si mnajua
sababu?! Ni kweli ulaya hamna lakini kila jambo
la ulaya ni sahihi kutumika kama kigezo katika
nchi ambayo ndio kwanza inatambaa kisoka?
Uzalendo.....
Licha ya ratiba ngumu ya mechi zote tano za
mwisho wa ligi kuipangia timu kucheza nje ya
uwanja wake wa nyumbani na Yanga kujitahidi
kuzipangua kwa jasho na damu huku ikitumia
bajeti kubwa lakini bado mnaongea??!
Ucheze Dar - Mwanza , Mwanza - Shinyanga ,
Shinyanga- Mbeya , Mbeya - Mtwara , Mtwara
kumalizia Songea na ndani yake una mechi za
kombe la shirikisho.
Hivi ratiba hiyo mngewapangia Coastal na kwa
mechi zinazofatana hizo si wangeishia njiani ?!
Yanga imelazimika kutumia bajeti kubwa ya
kuruka na ndege kila mahali ndani ya nchi ili
iendane na ratiba hiyo pasi kuchosha wachezaji
na kujiathiri wenyewe kutetea kombe lao na
uwakilishi wa nchi kimataifa . Hili si lilihitaji
makala ndefu na air time radion za kuipongeza
klabu hii ( likewise to Azam ) kuliko misuli ya
shingo kuwatoka kupinga issue Ndanda?
Yanga inacheza mechi ya marudiano na
Esparanca May 18 kule kwao Luanda . Mmeweka
ngumu ligi kusogezwa mbele na kwa bwana
mkubwa mlishitaki sawa tu, mechi na Ndanda ni
May 15 ( ilivyopangwa awali kabla ya kurudishwa
may 14) . Timu iondoke Mbeya May 11 fanya
wameishiwa hawana nauli ya ndege , wamecheza
jana ( may 10 ) pale Sokoine ina maaana leo May
11 waianze safari ya kuelekea Mtwara . Wafike
kule May 12 jioni sana kisha may 13 wapumzike
14 mzigoni . Warudi Dar wajiandaa lini kwa
mazoezi Dar? Na waende lini kule Angola
kufanya climatization kabla ya mechi?!
Tujadili mambo ya msingi sio kila jambo kupinga
tu . Hongera Ndanda kwa uzalendo na njoo Dar
ujivunie mihela ya kutosha maana siku hiyo
yenye kombe uwanjani na mechi kufanyikia Dar
huku mkipewa uenyeji ni kicheko tu .
Huenda mechi hii ikawa ndio mechi ambayo toka
Ndanda wapande daraja wakapata gate collection
ya maana .
Na Zoom Out
 
Mie baada ya kuisikia habari hii nilisangaa mno na kuona ni UTOTO, lakini baada ya kusikiliza kipindi cha michezo cha radio Uhuru nikakubaliana nao kuwa bodi ya ligi na TFF wamefanya UHUNI mtupu.
 
SOMENI KANUNI HIZI HAPA HALAFU MJIULIZE
.........
Uwanja wowote utakaotumika kwa michezo ya
Ligi Kuu ni lazima uthibitishwe na TFF. Kilabu
itachagua na kutambulisha uwanja wake wa
nyumbani na kuiarifu TFF/TPLB katika kipindi
cha Uthibitisho wa ushiriki Ligi Kuu.
(2) Katika mazingira maalum timu inaweza
kucheza mchezo wake wa nyumbani katika
uwanja mwingine endapo kuna sababu nzito na
za msingi, utambulisho wa uwanja katika
mazingira haya pia unawajibika kufanywa katika
kipindi cha uthibitisho wa kushiriki ligi au kwa
maombi maalum kwa TPLB angalau siku saba (7)
kabla ya tarehe ya mchezo husika.
(3) Katika kutambulisha uwanja wake wa
nyumbani timu itawajibika kuainisha vipimo vya
uwanja huo, aina ya majani (asili au bandia),
kama unaweza kuchezewa mechi usiku au la,
una uwezo wa kuingiza watu wangapi (stadium
capacity) na mamlaka inayomiliki uwanja huo.
(4) Endapo timu yoyote haina uwanja wa
nyumbani unaofaa kwa mchezo wa Ligi Kuu
inaweza kuchagua uwanja mwingine katika mji au
mkoa jirani na mkoa wa timu husika ndani ya
Tanzania Bara ilimuradi uwanja huo uwe na sifa
zinazokubalika na uthibitishwe au kuidhinishwa
na TFF, baada ya uteuzi wa uwanja timu
haitaruhusiwa kubadilisha uwanja huo kinyume na
sababu za kikanuni.
(5) Kutokana na sababu za kiusalama, uwanja
kutofikika au sababu nyingine yoyote ya msingi,
TFF kwa kushauriana na timu mwenyeji husika
inaweza kuhamishia mchezo husika katika
uwanja wa mji au mkoa jirani unaokidhi haja hiyo.
(6) TFF ina mamlaka ya mwisho ya kuhamisha
mchezo katika uwanja mwingine au kubadilisha
kituo cha mchezo kwa sababu inazoona zinafaa
kwa mchezo na wakati husika.
........ ......
Kanuni hii mbona haina kipengele cha MARIDHIANO? Hivi ingekuwa timu ya Ndanda ndo mabingwa na mchezo wao wa mwisho uwe Dar wangekubaliwa? Najiuliza mara kwa mara timu kwa nini Yanga huwa haichezi kwenye uwanja wa Chamazi?
 
TUNALETA USHABIKI , HISIA NA MTAZAMO
HASI KATIKA MAMBO AMBAYO NI RAHISI SANA
KUELEWEKA.....
Young Africans imejenga hoja makini ambayo
Ndanda na kamati ya ligi wameiona ina mashiko
na wameridhia .
Kuridhia sio tu kwa utashi binafsi bali kwa
kuchungulia vifungu na kanuni za ligi
zinasemaje ?!! Je kuna katazo la moja kwa moja
au makubaliano hayo yanaruhusiwa?! katiba au
kanuni za ligi hazina muhuri wa katazo hilo iwayo
yote kwa asilimia 100% .
Mambo ambayo yanaweza kufanya kituo cha
mchezo husika kuhamishwa
a. Ubovu wa uwanja
b. Usalama mdogo
c. Miundo mbinu mibovu itakayopelekea kuifanya
timu moja kushindwa kufika kirahisi.
d. Marekebisho ya uwanja ( ujenzi kuendelea)
e. Makubaliano binafsi kati ya timu mwenyeji na
mgeni kuhamisha kituo kwa sababu ambazo za
msingi na zenye ushawishi ( mantiki)
Kagera wamehama kituo chao mara ngapi?!
Mechi za Simba na Yanga ambazo mnasoma
historia zimechezwa Mwanza , Arusha au
Dodoma mnazikua sababu ? ( mechi za ligi kuu/
daraja la kwanza)
Ruvu JKT amehama viwanja vingapi ?! Hakuanzia
mabatini huyu ?! Mlihoji?!
Kwanini Yanga na Simba hawachezi Manungu ,
Mwadui , Karume na Chamazi? . Si mnajua
sababu?! Ni kweli ulaya hamna lakini kila jambo
la ulaya ni sahihi kutumika kama kigezo katika
nchi ambayo ndio kwanza inatambaa kisoka?
Uzalendo.....
Licha ya ratiba ngumu ya mechi zote tano za
mwisho wa ligi kuipangia timu kucheza nje ya
uwanja wake wa nyumbani na Yanga kujitahidi
kuzipangua kwa jasho na damu huku ikitumia
bajeti kubwa lakini bado mnaongea??!
Ucheze Dar - Mwanza , Mwanza - Shinyanga ,
Shinyanga- Mbeya , Mbeya - Mtwara , Mtwara
kumalizia Songea na ndani yake una mechi za
kombe la shirikisho.
Hivi ratiba hiyo mngewapangia Coastal na kwa
mechi zinazofatana hizo si wangeishia njiani ?!
Yanga imelazimika kutumia bajeti kubwa ya
kuruka na ndege kila mahali ndani ya nchi ili
iendane na ratiba hiyo pasi kuchosha wachezaji
na kujiathiri wenyewe kutetea kombe lao na
uwakilishi wa nchi kimataifa . Hili si lilihitaji
makala ndefu na air time radion za kuipongeza
klabu hii ( likewise to Azam ) kuliko misuli ya
shingo kuwatoka kupinga issue Ndanda?
Yanga inacheza mechi ya marudiano na
Esparanca May 18 kule kwao Luanda . Mmeweka
ngumu ligi kusogezwa mbele na kwa bwana
mkubwa mlishitaki sawa tu, mechi na Ndanda ni
May 15 ( ilivyopangwa awali kabla ya kurudishwa
may 14) . Timu iondoke Mbeya May 11 fanya
wameishiwa hawana nauli ya ndege , wamecheza
jana ( may 10 ) pale Sokoine ina maaana leo May
11 waianze safari ya kuelekea Mtwara . Wafike
kule May 12 jioni sana kisha may 13 wapumzike
14 mzigoni . Warudi Dar wajiandaa lini kwa
mazoezi Dar? Na waende lini kule Angola
kufanya climatization kabla ya mechi?!
Tujadili mambo ya msingi sio kila jambo kupinga
tu . Hongera Ndanda kwa uzalendo na njoo Dar
ujivunie mihela ya kutosha maana siku hiyo
yenye kombe uwanjani na mechi kufanyikia Dar
huku mkipewa uenyeji ni kicheko tu .
Huenda mechi hii ikawa ndio mechi ambayo toka
Ndanda wapande daraja wakapata gate collection
ya maana .
Na Zoom Out
Kiswahili fasaha+ujumbe maridhawa,itakua ajabu kubwa mkia usielewe ulichoandika,asante kwa ufafanuzi makini.
 
TUNALETA USHABIKI , HISIA NA MTAZAMO
HASI KATIKA MAMBO AMBAYO NI RAHISI SANA
KUELEWEKA.....
...............! Ni kweli ulaya hamna lakini kila jambo
la ulaya ni sahihi kutumika kama kigezo katika
nchi ambayo ndio kwanza inatambaa kisoka?
Uzalendo......
Na Zoom Out
Mkuu umetiririka vya kutosha, ila nimekunwa na hiyo sentensi. Je pana tija gani basi ligi yetu iende sambamba na UEFA? Wawakilishi wetu wanashiriki mashindano yanayoandaliwa na CAF!
 
Ndanda wanalipa fadhila za mwaka jana Hahaaaa soka la bongo bhna full maajabu
 
jkt ruvu kwa mara tofauti tofauti imekuwa ikitumia viwanja tofauti kama viwanja vyao vya nyumbani huku sababu za kufanya ivyo zikiwekwa bayana hii pia imetokea kwa kagera sugar. hivi hii hali ya chuki dhidi ya yanga baada ya kukubaliana na ndanda mechi yao kuchezewa taifa na sababu zimewekwa wazi inatoka wapi. mbona hatujaona hizo harakati zenu kuitetea azam inayolazimishwa bila kupenda na tff kucheza mechi 2 zote dhidi ya simba na yanga kama mwenyeji taifa huku akiwa na uwanja wake si wa kukodi kama timu nyingine hizi.maana hoja ya kwamba simba ya yanga zina mashabiki wengi na chamanzi ni padogo hazina mashiko maana kuna timu ulaya uwezo wa viwanja kujaza mashabiki ni mdogo kama wa uwanja wa majimaji na man u, chelsea, arsenal n.k wanaenda kuchezea huko. wanaokosoa hili la ndanda v yanga taifa wametanguliza chuki pasina kufuatilia ukweli kwamba yapo mazoea kama haya kwenye ligi yetu. hapa tatizo ni chuki dhidi ya yanga tu
 
Viongozi wa Ndanda wametukosea watu wa Kusini.. Imetukosesha uhondo na Haki yetu kama timu ya nyumbani.. Na mara nyingi mechi tunazocheza na Yanga au SIMBA ndio mechi zinazo vuta watu lakini viongozi wameziba pamba masikioni... Ili kosa litawatafuna milele
 
ndanda wameona mbali na kuona ni heri wakapate hizo million zaidi ya 100 za mapato ya mechi maana taifa itajaa si mchezo kwani mwali atakuwa anakabidhiwa rasmi
 
ndanda wameona mbali na kuona ni heri wakapate hizo million zaidi ya 100 za mapato ya mechi maana taifa itajaa si mchezo kwani mwali atakuwa anakabidhiwa rasmi
Na ukizingatia Ndanda ndio watakuwa wenyewe, kwanini wasiingiza Mkwanja wa kufanyia usajiri eti wasikilize maneno ya Akina Shafii Dauda ambao hawaisaidii timu pindi inapokuwa na Ukata!!!!!!!! Ndanda wametumia fursa
 
Viongozi wa Ndanda wametukosea watu wa Kusini.. Imetukosesha uhondo na Haki yetu kama timu ya nyumbani.. Na mara nyingi mechi tunazocheza na Yanga au SIMBA ndio mechi zinazo vuta watu lakini viongozi wameziba pamba masikioni... Ili kosa litawatafuna milele
Kuna siku umewahi kutoa japo shilingi 1000 ili kuisaidia Ndanda hasa kipindi inapopitia kwenye Ukata!!!!!!
 
Wa matopeni hamna hela ya kununua mechi tuwakopeshe maana tunazo nyingi bank .mnyama paka ukiona manyoya juwa kaliwa.
 
Ni jambo la kiungwana sana hili, Ndanda wameonyesha uzalendo na kujali maslahi mapana ya Nchi.
Kwa namna ya miundombinu ya usafiri wa Nchi yetu ulivyo hakika Yanga wangechoka kwenda Mtwara na kurudi halafu waunganishe Angola.

Nawapongeza Ndanda fc na bodi ya ligi kwa kuangalia maslahi ya nchi, Yanga akisonga mbele kwenye kombe la shirikisho ni faida kwa nchi nzima.

Si mnasema nyie mnasafiri kwa ndege?? Mtwara ndege zinatua mbona
 
Ni jambo la kiungwana sana hili, Ndanda wameonyesha uzalendo na kujali maslahi mapana ya Nchi.
Kwa namna ya miundombinu ya usafiri wa Nchi yetu ulivyo hakika Yanga wangechoka kwenda Mtwara na kurudi halafu waunganishe Angola.

Nawapongeza Ndanda fc na bodi ya ligi kwa kuangalia maslahi ya nchi, Yanga akisonga mbele kwenye kombe la shirikisho ni faida kwa nchi nzima.
Kuchoka Mtwara kivipi? Barabara ni nzuri, Uwanja wa ndege Upo na ni saa 1 kutoka Dar ushafika Mtwara. Visingizio vya kuchoka havina mashiko makubwa. Makubaliano KUNTU hayo, labda kwa kuwa Ndanda iko hoi kifedha watapata advantage ya kuhost mchezo huo hasa ikizingatiwa Ndanda atakua mwenyeji na siku ya mechi hiyo Yanga atakabdhiwa Kombe na hivyo unaweza kuvuta watu wengi na hivyo kipato kwa Ndanda kuongezeka.
 
Maisha haya ni vise versa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom