Nchi imekosa wenye busara hadi wanaacha Naibu Spika anaiharibu?

Madhara ya kutofuata sheria, kanuni na taratibu ndiyo yanayowakumba wabunge wa upinzani. Zipo kanuni na taratibu za kumshitaki au hata za kumtoa NS au hata spika mwenyewe lakini wabunge hawa hawakutaka kuzifuata badala yake wakaamua kuchukua hatua za kisanii na kuingia mitaani. Sasa wamejikuta njia panda: mitaani hakuingiliki na bungeni hapaingiliki maana mama yuko pale 24 hours hadi 2020!!!
 
Dr Akili, tukiliacha hili liendelee nani anaharibikiwa hapo? Ndio maana tunasema busara iingilie kati la sivyo budget ya 2016/17 itakuwa ya hovyo haijapata kutokea, na pamoja na wananchi kuumia lakini hata serikali ya ccm ndiyo itakayoshindwa kutekeleza majukumu yake na kupoteza ushawishi wake. Yaani kuanguka.
 
Na uzuri CCM ni vilaza. Hawajui kuikosoa bajeti kama wapinzani.
Ndo maana wamekaa hapo kama makondoo.
 
Dance la sisiemu ukawa wataendelea kulicheza kama sisiemu wanavyotaka ukawa walicheza, wakichenji biti la songi ni hao hao sisiemu watawaamrisha ukawa wachezaje, na bila kusita watacheza!
 
Ni maagizo kutoka juu kuwa tulia aendelee kukalia, na mzee Kikwete hataki kuingilia hayo mambo kwa sababu ameshaonekana na makufuli kuwa yeye ndiye ameharibu kila kitu pamoja na wazee wenzie.
Kwa hiyo kolabo ya Kikwete na wazee wengine wenye busara wamenyamaza ili mambo yamharibikie makufuli ili watanzania wajaji wenyewe.
 
Tumefika mahali pa kuacha Naibu Spika mteule anaikosesha nchi mjadala mpana wa budget kwa kiburi chake na hakuna mwenye busara wa kuliona hili?

Wabunge wa upinzani wameshtaki kuwa hawatendei haki hivyo akiwa anasimamia vikao hawataingia, lakini kinachotangazwa ni kuwa Wabunge wamegomea bunge.

Huo sio ukweli hata kidogo, kama kuna tatizo Wenyeviti wa Bunge wangeweza kuendesha vikao kama kawaida wakati huu Spika mwenyewe akiwa hayupo lakini la ajabu Naibu spika anang'ang'ania kila siku awepo ili watoke kwa makusudi mazima ambayo wenye busara wanashindwa kuliona hilo.

Kwa kauli zao za chini kwa chini (labda kuogopa kushughulikiwa) wa CCM wamekuwa wakilalamika kuwa kwa uwepo wao pekee hakuna cha maana kitakachorekebishwa katika budget hiyo.

Swali langu jee wale wazee na wengine wenye busara katika kushauri nchi hii kwenda katika misingi ya uhakika ya kusonga mbele wamepatwa na nini hadi kukaa pembeni na kumuacha mteule huyu wa Rais (ndio ukweli) akiharibu mfumo huu wa mihimili mitatu ya nchi kwa jeuri ya kugangamala lazima aongoze vikao?

Nina uhakika Ndugai angekuwepo asingeruhusu hilo liendelee kabla ya kuwekwa sawa.
Katiba mpya ilitaka kumpunguzia kiongozi fulani nguvu, wasiojua wakapiga makofi kwamba sio sahihi ... sasa tunayoyaona ndo hayo ... akikaidi maamuzi ya flani ... hatujui hatima yake ....

Kwa hali yoyote ile nchi ikiongozwa na maandishi yenye tafsiri zenye utata matokeo yake ndo haya ... mtalalamika hadi mchoke, dawa ni moja tu - msikilizeni mzee wetu Warioba na mapendekezo yake ya katiba mpya.
 
Wenye busara wapo wengi ndani ya ukumbi wa bunge, nadhani huwa unaona wakati upinzani wanaposusa, wale wengi huamia kwenye viti vinavyoachwa wazi halafu kunakuwa hakuna tofauti yoyote ile, inakuwa kama vile hakuna lililotokea ukumbini.
Hao hao wengi na wenye busara ndio wamemteua Dr Tulia, na anawakimbiza kweli wale vichwamaji, kwa sababu walishamzoea yule Mama Makinda ambaye aliingia bungeni mwaka 1975, karibu nusu au robo tatu ya wale wanaosusa, walikuwa bado hawajazaliwa.
Sasa wamekutana na dada wa kinyakyusa, hapelekeshwi kijinga. Shule ya sheria imelala kichwani, ni mwendo wa vifungu na kanuni, hakuna mambo ya kitoto ya kupiga kelele kama watoto wa darasa la tatu.
 
Umemaliza?
 
Kweli uhuru wako unautumia vizuri ... ila sijui kama unatafakari kabla ya kuchangia lolote.

Wanaobaki ndo wenye busara kweli???
 
Bidhaa bora huchaguliwa na wengi. Kususa, kuzira na tabia nyinginezo kama hizo haziwezi kuupaisha upinzani. Na wenye kujua thamani ya maamuzi ya busara kwa sasa wanawaangalia wapinzani jinsi wanavyochemka kila kukicha.
 
Hata watumiaji wa gongo ni wengi zaidi ya watumiaji wa bia. Je gongo ni bora zaidi ya bia?
 
Kumbe kwa kukaa pale kuna posho? Sasa ndio maana kimama kimekomaa tuu. Lakini kwa wenye kujua kusoma nyuso za watu, uso wa yule mama una majibu mengi kwa sasa. Uko kama uso wa mtu mchawi ambaye mtaani wamejitokeza watu na kumwambia wewe mchawi!
Wabongo mnajua kuchambua.
 
Nashangaa ccm wanasema hawana hela za mkutano mkuu! Wavalishe mashati kijani waende ajenda zao bungeni wamalize....nafasi zile za ukaw wakae wana ccm wamalize.....wampe kiti JPM maana bunge limekuwa mkutano wa ccm
 
Pole sana kaka Chakaza, mchezo huu kwa kawaida hautaki hasira.
Kaka mchezo haunitii hasira bali matokeo. Baada ya July bajeti hii hewa itaanza kuwa implemented na hapo maumivu yatajitokeza hata yale ambayo busara ingetumika yangeweza kuwekwa sawa.
Mimi na wewe twaweza kupambana na kasoro hizo na athari kuwa ndogo lakini jee wale ndugu zetu wengi walio vijijini na hata mijini tunawafikiriaje?
Kweli kwa ushabiki wetu huu wa kama Yanga na Simba turuhusu uwape mateso hata na kupoteza maisha pale palipo na uwezekano wa kuzuia? Tuna tofauti gani na wauaji wengine hapa duniani?
Unajua kuwa ujuapo kuwa chakula hiki kina sumu na unamuona mwenye njaa anataka kula nawe humzuii Lisa haikuhusu nawe unakuwa muuaji sawa na aliyeweka sumu?
Nakuomba nawe Mungu akusaidie moyo huo ukutoke
 
Tangu JPM amepewa nchi imepita miezi saba tu. Ngoja tumpe muda, ngoja tuzipe muda reforms ambazo Mama Samia alizizungumzia siku ile alipoongea na kinamama.
Warusi wanao msemo usemao "matuimani hufa mwishoni". Cha muhimu ni kuwa na positive mindsets, mengineyo ni mitihani tuliyoumbiwa na Mungu.
 
Back
Top Bottom