Pre GE2025 NCCR na vyama vingine wana mkakati gani pamoja na kushiriki uchaguzi kwenye mazingira yaleyale ya 2019,2020 na 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

tripof

JF-Expert Member
Apr 2, 2024
853
1,146
Mimi ni muumini wa demokrasia na uchaguzi huru na haki, na ni mwana mageuzi kutokea NCCR sasa naomba nifahamishwe mikakati iliyopo ya kukabiliana na changamoto za sasa za uchaguzi iwapo watashiriki.

Mimi ninaamini iwapo kama hapatakuwa na mifumo na utashi wa kisiasa CCM lazima ichukue kata, majimbo na Urais na kwa uhakika NCCR hawatapata mbuge hata wa dawa labda kama wana vizia kupata Luzuku kwa ushiriki na idadi ya kura. Vinginevyo tupeni na nyinyi mkakati wenu.

Hiki ni chama cha siasa kina lengo la kushika dola. je kwenye uchaguzi usio wa haki na huru mnatarajia kujinasua vipi. Tupeni mkakati.

Soma
 
Wao wenyewe wanajua hawana madhara,wanategemea waitwe wapewe kiasi flani,wagange njaa.
 
Ni ma vyama mapandikizi ya CCM, yenyewe yalishasema reform zote zimefanyika kwa hiyo yapo tayari kwa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom