Nawaza kumletea mzee nguo kama zawadi ya valentine. Ni sawa au nitakuwa nimekosea?

yassird200

JF-Expert Member
Jan 2, 2025
389
695
Wakuu! Binafsi mimi si mtu wa masuala ya mapenzi hata kwenye siku kama ya leo.

Leo nilikuwa na mpango wa kuwatembelea wazee, lakini kwa kuwa ni siku ya upendo, nikaona si vibaya nikichukua chochote kwa ajili yao. Kuhusu huyo mzee, ishu si yeye kama mtu, bali ni mama yake.

Sasa nawaza kumletea nguo—je, hiyo itakuwa sawa au nitakuwa nimekosea?

Shida ni kwamba si utaratibu wangu kufanya hivi mara kwa mara, nikaona bora niulize ushauri. Au nikae kimya, niende hivyo hivyo, wataelewa wenyewe huko? 😅

Nisaidieni mawazo!
 
Nunua
-Mchele 10kgs
-Mfuko mmoja wa ngano
-Sukari 10kgs
-Nyanya na vitunguu vya kutosha
-Mkungu wa ndizi mbichi

andaa
-Kibunda atleast 100k kwa kila mmoja, na 5k kwa madogo kama wapo
 
Kama unajua size yao wanunulie tena itakuwa kumbukumbu ya mda mrefu pesa na chakula vitaisha na watasahau mbona wakati tulivyo wadogo wazee walikuwa wanatununulia nguo iweje saiv jitu linakwambia siwezi mnunulia nguo mzazi wangu anaona aibu huo ni ujinga
 
Nunua
-Mchele 10kgs
-Mfuko mmoja wa ngano
-Sukari 10kgs
-Nyanya na vitunguu vya kutosha
-Mkungu wa ndizi mbichi

andaa
-Kibunda atleast 100k kwa kila mmoja, na 5k kwa madogo kama wapo
Mkuu huko nikufirisiana na budget ya 150k pekee
 
Kama unajua size yao wanunulie tena itakuwa kumbukumbu ya mda mrefu pesa na chakula vitaisha na watasahau mbona wakati tulivyo wadogo wazee walikuwa wanatununulia nguo iweje saiv jitu linakwambia siwezi mnunulia nguo mzazi wangu anaona aibu huo ni ujinga
Ndio nlitaka kuanza kujifunza kuwapa wazee zawadi nje ya pesa
 
Nunua vitenge vya kutosha vya mama chukua na makoti ya mzee kama upo vizuri mchukulie mzee boda boda au gari ndogo, watafurahi sana utakuja kunishukuru hayo masuala ya mchele sijui unga achana nayo.
 
Back
Top Bottom