Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,794
- 31,804
NAWAKUMBUKA SANA
Kwenye picha hapo chini wa kwanza kulia ni Sheikh Abdallah Muhsin, Sheikh Ali Muhsin, Mwandishi na Farouk Abdullah.
Muscat mwaka wa 1999.
Nimeweka kitabu cha kumbukumbu ya maisha ya Sheikh Ali Muhsin nakala ya Kiingereza na Kiswahili, Tafsir yake ya Qur’an Tukufu na Tafsir ya Al Bukhari kutoka Kiarabu kuja Kiswahili ya Sheikh Abdallah Muhsin.
Masheikh wawili kutoka familia moja na baba yao pia alikuwa sheikh na ndiye alikuwa mwalimu wao.
Farouk Abdullah ndiye aliyetafsiri kitabu cha maisha ya Sheikh Ali Muhsin, "Conflict and Harmony in Zanzibar," kutoka Kiingereza kuja Kiswahili.
Hawa wote wametangulia mbele ya haki miaka mingi iliyopita.
Nawakumbuka sana.
Sheikh Ali Muhsin alifungwa jela miaka 10 baada ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Maisha yake ya kifungoni katika jela tofauti Tanzania Bara ni chuo cha kutosha.
Sheikh Ali Muhsin aliandika vitabu kadhaa akiwa kifungoni na vyote vimechapwa baada ya yeye kutoka jela.
Baada ya kutoka ifungoni na kutambua kuwa hatokubaliwa kamwe kutoka Tanzania kwa njia halali aliamua kutoroka kwa kupitia njia za panya.
Sheikh Ali Muhsin alifanya mipango madhubuti ya kukimbia Tanzania akisaidiwa na watu wake wa karibu.
Ukisoma kisa cha kutoroka kwake kwenye kitabu chake utadhani unaangalia filamu kutoka Hollywood ya mtu anawakimbia Gestapo.
Kabla hajavuka mpaka wa Horohoro kuingia Kenya alikamatwa mpakani na askari.
Ilikuwa usiku.
Wale askari walimwachia baada ya kuwaeleza yaliyomfika na kwa nini aliamua kutoroka.
Wale askari waliamua kumuachia na wakamsindikiza kuvuka mpaka hadi upande wa Kenya lakini walichukua fedha, saa ya mkono aliyokuwa amevaa na kitambaa cha suti alichokuwanacho.
Mkasa huu na yale aliyopitia kifungoni yeye na wenzake inaweza ikitengenezwa filamu ya kuvutia sana.
Kitabu cha Sheikh Ali Muhsin ndiyo kitabu cha kwanza katika vitabu vya historia ya Mapinduzi ya Zanzibar kuandikwa na wale waliopinduliwa.
Baada ya kitabu cha Sheikh Ali Muhsin kuchapwa Dubai kikafuatia kitabu cha Aman Thani, "Ukweli ni Huu," Issa Nasser Ismail, "Zanzibar Kinyang'anyiro na Utumwa," "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," alichoandika Dr. Harith Ghassany mimi nikiwa Research Assistant wake.
Kupitia Sheikh Ali Muhsin katika safari hii ya Muscat nikakutana na kujulishwa kwa hao wote hapo juu.
Hawa wote wakawa watu wangu wa karibu sana hadi walipohitimisha maisha yao hapa duniani na katika uhai wao nilinufaika kwa mengi kutoka na elimu zao na waliyopitia.
Hakuna Mzanzibari aliyeshuhudia mapinduzi ambae hana historia ya mapinduzi.
Kuna kisa alinieleza Sheikh Abdallah Muhsin.
Hiki ni kisa cha kuhuzunisha cha muuaji mtesaji na waliouliwa.
Ajabu ya Rahman.
Kisa hiki akaja kunieleza Mzee Aboud Jumbe.
Hawa Wazanzibari waliuliwa Aboud Jumbe akiwa Rais wa Zanzibar.
Aboud Jumbe hakujua kuhusu haya mauaji.
Kaja kupata taarifa mauaji yameshatokea.
Mzee Jumbe anasema alihuzunika sana.
Kisa hiki hiki tena akaja kunieleza muhusika mwenyewe kwa kinywa chake yule aliyewakamata.
Miaka mingi ilikuwa imepita baada ya mauaji yale.
Sikumuomba anieleze ila yeye baada ya kuuliwa Karume aliondoka Zanzibar akaja Dar-es-Salaam kuishi mafichoni.
Inaelekea kwake yeye Zanzibar ilikuwa haikaliki tena kwake.
Watu mfano wake hawakuwa na kazi ya kufanya chini ya utawala wa Aboud Jumbe.
Akiwa mgonjwa ilimjia fikra ya kutaka kuandika maisha yake katika ukachero Zanzibar na yote aliyopitia.
Wanesema ilikuwa akipita mtaa fulani siku nzima watu hawana raha hawajui nani atakuja kugongewa mlango usiku achukuliwe.
Hii si sifa ya Muislam.
Yawezekana alijua hana muda mrefu wa kuishi.
Bila shaka aliona kueleza yaliyotokea itamsaidia kuutua mzigo wa msongo wake wa mawazo iliokuwa umemwelemea kifuani.
Kifua chake kilikuwa kinafurukuta kwa joto kali.
Kupitia watu akanitafuta.
Tulikutana.
Alinitaka tukae kitako tuandike kitabu cha maisha yake.
Bila shaka alikuwa kajuta na alitaka akutane na Mola wake, Allah Hakimu Muadilifu akiwa keshatubia.
Kila niingiapo Maktaba na kuona vitabu hivi nawakumbuka wazee wangu hawa na mengi niliyojifunza kutoka kwao.
Kulia Sheikh Abdallah Muhsin, Sheikh Ali Muhsin, Mwandishi na Farouk Abdullah, Muscat 1999