Car4Sale Nauza gari 2,200,000/=

Habari zenu wapendwa,

Naitwa Frank, nauza gari yangu aina ya Toyota Chasser Raffine, rangi ya dark blue, haidaiwi TRA wala insurance, ukinunua unawasha na kuondoka nayo kwakuwa aina tatizo lolote la kiufundi.

Hapo zamani ilikuwa ina engine ya 6 ila kwa sasa ina engine ya 4 cylinder, ulaji wake wa mafuta upo vizuri na gari ni ya yangu mwenyewe na kadi yake ninayo na gari hii nina muda nayo wa miezi 7 mpaka sasa ninaitumia mwenyewe kutoka nayo nyumbani kwangu Goba hadi kazini kwangu Kinondoni.

Gari hii ipo Dar es salaam na ninaiuza kwa bei ya Tshs. 2,200,000/= (milioni mbili na laki mbili) pungufu unaongea! (nimeambatanisha na picha).

Namba yangu ya simu ni 0716 00 23 23.
Hii gari kama nishawahi kuiona mitaa ya kinondoni studio karibu na invotech mitaa ile he ac ipo maana naona hapo ulipopigia picha ni kwa Fundi wa AC
 
Kwa anayejua magari, gari kama hilo hauwezi kuiuza zaidi ya milion 3 kwakuwa ni ya zaman ila kwa ubora ni gari ngumu sana watu wa mikoani wanazijua, na nimeweka bei hiyo kwakuwa mimi ndio mmiliki sina bei za tamaa ndo maana gari zote niliouza humu bei zangu huwa ni rahisi ila nikibugi kumpa dalali aniuzie ndo ataanzia milioni 4 ili na yeye apate!
Hi nzuri kwa biashara ya Taxi ntakucheki mkuu mana bodaboda vijana wanaharibu sana nakula hasara
 
Nashukuru sana mpendwa, watu wa kutoa kejeli nimeishawazoea halafu kama ingekuwa ndio gari yangu ya kwanza ningeishakata tamaa ila hii ni gari yangu ya tatu kuuza humu na gari zangu mbili za mwanzo nimeuza humu humu, gari yangu ya kwanza ilikuwa nissan march nyekundu ya mwaka 1998 nilipoitangaza humu nilipata maneno ya kukatisha tamaa lakini akatokea mteja kutoka mwanza akaja kuinunua na akasafiri nayo mpaka mwanza ila kama unavyojua kwa nissan watu humu waliponda ohoo spea zake ghari mara maneno ya kejeli kibao lakini mwisho wa siku niliuza, gari yangu ya pili ni nissan march.

Pia ya mwaka 2004 ile yenye muundo wa kobe watu waliniponda lakini mwisho wa siku nikamuuzia humu humu jamaa mmoja wa uhamiaji dar es salaam. sasa kwa gari yangu hii ya tatu kuuza humu na kukutana na maneno ya kejel hakika sintokata tamaa halafu uzuri wa hii gari engine yake unaweza kuiweka karibia gari zote za Toyota ikiwemo Hiace na Noah kwa hivyo nikikosa mteja kwa bei ninayoitaka mimi nitaendelea kuitumia na nikiichoka natoa engine, gear box na control box yake natafuta body nyingine ya gari ya toyota nafunga, na body ya chasser napeleka pale mabibo nauza, sasa wanaonibeza wanafikiri mimi ni mgeni wa haya mambo.

Nashukuru sana Ng'wanapagi kwa maneno yako mazuri.
Hivi Mkuu ile biashara yako ya kukopesha watu Pesa kisha wanaweka bondi magari yao bado unayo??
 
Mkuu gari huu utapata mteja fasta. Watu hatufanani , na haina maana kuwa gari ikiuzwa bei ndogo lazima iwe kimeo...Nina ushuhuda MTU alinunua kwa 1.8m collora e100 miaka 2 iliyopita na bado iko vema anatumia kwa shida zake za usafiri. Sio kila MTU akitaka kununua gari anataka ya showoff, wengine wanakaa msakuzi huko wana kibarua posta, hakika gari itamsaidia bila kujali no A,B,C, au D: gari matunzo, hata kama ni ya mda unajuaje ubovu wake wakati spea hubadilishwa Mara zinapoisha, na hii kwakwambia injini kabadili; pia una fursa ya kuikagua gari vizuri.
 
Mkuu gari huu utapata mteja fasta. Watu hatufanani , na haina maana kuwa gari ikiuzwa bei ndogo lazima iwe kimeo...Nina ushuhuda MTU alinunua kwa 1.8m collora e100 miaka 2 iliyopita na bado iko vema anatumia kwa shida zake za usafiri. Sio kila MTU akitaka kununua gari anataka ya showoff, wengine wanakaa msakuzi huko wana kibarua posta, hakika gari itamsaidia bila kujali no A,B,C, au D: gari matunzo, hata kama ni ya mda unajuaje ubovu wake wakati spea hubadilishwa Mara zinapoisha, na hii kwakwambia injini kabadili; pia una fursa ya kuikagua gari vizuri.
Safi sana IPILIMO Baeleze, maana kuna watu wako humu kazi yao ni kuharibu biashara za watu! Kwenye kuuza gari humu huwa sina presha hata kidogo na ndio maana hata gari zangu mbili za mwanzo niliuza humu humu licha ya watu kuikejeri biashara yangu. Gari hii naiuza ili niongezee hela nitafute gari nyingine na sio kwamba nauza kwakuwa ni mbovu hapana ni nzima kabisa halafu ndio naitumia kila siku from goba to kinondoni. Kuna baadhi ya wateja wa mikoani wameishaanza kunitafuta kwahivyo sina presha ya kuiuza hata kama nitakaa nayo mwaka mzima sina hata presha kwakuwa ni gari nzima, ngumu na inanisaidia. Asante sana Ipilimo
 
Gari ni matunzo tu na kujua thamani ya gari na umuhimu wake kwako. Mie nina creata ni number A lakini ukija na Number D yako haitii mguu
ImageUploadedByJamiiForums1458222987.209914.jpg
ila all in all mkuu Frank gari yako utaiuza na usikate tamaa. Stand still, be solid
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom