Nauli boti za AZAM, wahusika mnajua yanayofanyika?

SUMATRA kazi hiyo, najua mmo humu. Tekelezeni wajibu wenu, vinginevyo bahasha zinawahusu.
 
Kwamaana iyo mmliki wa Azam anapata pesa isiyokuwa ya halali,kama yupo humu Jf basi alizingatie hilo
 
Mama zao wale watu ni wajinga wa kutupwa? Hawafai kabisa, hawana utu kabisa, unaweza kuenda pale unataka uwahi msiba, nauli yenyewe umechangiwa ikafika hiyo 25000, halafu unafika pale wanakuletea ujinga na njaa zao, Mungu atawalipa
 
Umeona eee kumbe tangu mwaka jana hili tatizo lipo?inaonekena limeota mizizi na hakuna hatua zinazochukuliwa,lakini mm nimeamua kulivalia njuga,nitaliandika mitandaoni kote hadi kwenye magazeti na hata Azam head office nitalifikisha
Mkuu sio mwaka jana, lipo miaka mingi tu, kama miaka 3 nyuma ilishawahi kunitokea, nikahairisha safari kwa mda ule, nikasafiri mda uliofata
 
Ni kweli kabisa hata mie nilishafanyiwa huo ujinga ila nikomaa naye yule dada hadi nikamwambia nimekurekodi kila kitu na ninalipeleka mbele hili suala, akatepeta akanirudishia huku kanuna kinoma.
 
Sio walanguzi na wala sio madalali,ni ofisini kwenyewe kabisa tena kwenye dirisha la kukatia tiketi,wanaolangua ni hao wenyewe wanaokatisha tiketi,wanakwambia tiketi kwenda Zanzibar ni elf 50 au 35 wakati kwenyewe tiketi inaandikwa elf 25..ukilalamika unaambiwa kaa pembeni wenye hela wakate tiketi
Inavyoonekana hii ofisi ina walakini. Na wenye kampuni wanaiendekeza hiyo hali. Tuiombe SUMATRA iingilie kati ili wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria
 
Habari wan jamvi.

Usafiri wa baharini kati ya Zanzibar na Dar es salaam, umeboreshwa sana na boat nzuri sana za Bakharesa, boat zao ni nzuri sana na zimesaidia sana.

Tatizo linalojitokeza kwa sasa ni ulanguzi wa tiketi, na ulanguzi huu ungekua unafanyika na madalali wa nje (middlemen) hapo tungesema mengine, lakini ulanguzi unafanyika ndani kabisa katika ofisi, (ndani kwa mkatisha tickets), nitatoa mfano ulio hai kabisa kwa ndugu yangu ambae nilikua nasafiri nae kutoka Dar kwenda Zanzibar, siku ya tarehe 8 May, mimi nilikua nina ticket number kwa sababu nilishalipa in advance, mwenzangu alikua yeye anataka kukata ticket palepale ofisini bandarini,tulipofika akaambiwa ticket zipo ila ni Tsh 50,000 kutoka Dar - ZNZ, kwa sababu ya haraka na ulazima wa safari, ikabidi alipe, lakini cha ajabu ticket ilipotolewa imeandikwa Tsh 25,000, ikawa ni kelele sana, na tukataka tutafute wakutusaidia, lakini haikuwezekana kabisa, ticket za boat hua ni Tsh 50,000 kwa watanzania kama ni VIP seat, lakini kalipa Tsh 50,000 halafu akapewa ticket ya Economy class......huu ni wizi wa waziwazi kabisa, na inakera sana.

Kuna watu wengine walikua wanakuja na hio Tsh 25,000 tu na wanaambiwa tiket ni elf 50, na hawana nyengine,yaani unawaona wanaishiwa nguvu kabisa, hadi unawaonea huruma.

Nauliza hvi vyombo vinavyohusika na udhibiti wa nauli hawajui haya yanayotendeka??? au wako pamoja na hao walanguzi???

Naomba kuwakilisha.
Habari!

Mimi ni mmoja wa waajiriwa kutoka kampuni ya Kilimanjaro Fast Ferries.(Finance departmet).
Tumekua tukipata changamoto nyingi juu ya ulanguzi wa tiketi. Tunaomba radhi kwa yaliomkuta ndugu yako.
Ili tupate kukusaidia nahitaji kujua book ID no. na jina la sales officer aliyekuuzia hio tiketi.
Je ulipotozwa Tsh 50,000/- ukapatiwa tiketi ya daraja la economy ambayo gharama yake ni Tsh 25,000/- ulichukua hatua gani?
 
Asante kwa majibu yako, please naomba uni PM contacts zako ili tuwasiliane kwa ukaribu, hii kitu inakera sana na inaumiza watu sana, unakuta mtu kachangiwa nauli ili awahi msibani, unafika unaambiwa bei imepanda.

Kusema ukweli mm sikuchukua jina la huyo sales officer wenu,huwezi hata kuwauliza wanakua ni wajeuri vibaya mno, na dharau juu, ila kama mnataka kufatilia tumeni mtu ajifanye kama anaenda kununua tiketi, ikiwa imebakia kama saa moja boti kuondoka, unaenda na elf 25 wanakwambia tiketi zimebaki za elf 35 au 50 tu na ulilipa wanakupa tiketi ya elf 25. Ukiwa mkali anakuja mlinzi anakwambia kaa pembeni.....yaani ni maudhi na uzalilishaji mkubwa.
 
atatokea tu, unajua wamekuwa kama enzi zile PW, aisee walikuwa na nyodo sana hawa watu, lakini baada ya FN kuingia, 5H, wamfanyie nani nyodo na sasa kuna TC, sasa hivi wanakubembeleza, aliwahi kutokea 1 anaitwa Royal, kwanza alikuwa na mbio kumzidi azam, lakini hakudumu, ila kutokana na mambo ambayo sitaweza yasema jamaa aliwafanyia mtima nyongo, sasa hivi ukifika zanzibar unaziona zimepaki, ila huyu kidogo alionekana mnyoosha, manake azam anaondoka dar au zanzibar yeye baada ya nusu saa anaondoka na anamuacha kwenye maji, jamaa anachanja mbuga, ila nasikia aliwahi kumfanyia jeuri huyu royal, wakati azam anaondoka ka nusu saa hivi yeye akaja nyuma yake na akamzunguka kisha huyo dar, kile kitendo kiliwakera sana wafanyakazi, tangu hapo sijamsikia tena royal,
Ndio vitu gani hivyo mkuu?
 
Habari!

Mimi ni mmoja wa waajiriwa kutoka kampuni ya Kilimanjaro Fast Ferries.(Finance departmet).
Tumekua tukipata changamoto nyingi juu ya ulanguzi wa tiketi. Tunaomba radhi kwa yaliomkuta ndugu yako.
Ili tupate kukusaidia nahitaji kujua book ID no. na jina la sales officer aliyekuuzia hio tiketi.
Je ulipotozwa Tsh 50,000/- ukapatiwa tiketi ya daraja la economy ambayo gharama yake ni Tsh 25,000/- ulichukua hatua gani?
....kafie mbele!
..tafuteni solution ya kudumu,sio kuomba radhi kwa mtu mmoja mmoja wakati tatizo ni la muda mrefu sana na limeathiri watu wengi!
....ungekuwa karibu ningekulamba makofi wallah!
 
Report the matter to relevant authorities-with all evidence. Ukilalamika tuu bila kutafuta suluhu haikusaidii wewe wala jamii iliyokuzunguka.
 
azam upande wa tiket kwa kweli wanamatatizo sana kiukwel wanatupiga sana then hawana fear wala ubinadam..juzi nimechelewa boti nafika bamdarin na boti inatoa nanga niliyotakiwa kuondoka nayo mambo ya mvua usafir wa daladala ilikuwa niondoke saa 1 asubhui...wakaniambia ili niondoke na boti ya saa 3 asbhui hio nilipe tena elfu kumi na tano...nilishangaa sana nikajaribu kuwapliz wakagoma nilivyotoa 15nikaweza kusafiri na kilichofanyika ni kupigiwa stamp ktk tiketi ile ile nikamuliza yule jamaa sasa kufanya hivi ndio 15 elfu na me ni mteja wenu kuniambia tu nisubir boti inayofata imeshindikana.ndio azam hao
 
Asante kwa majibu yako, please naomba uni PM contacts zako ili tuwasiliane kwa ukaribu, hii kitu inakera sana na inaumiza watu sana, unakuta mtu kachangiwa nauli ili awahi msibani, unafika unaambiwa bei imepanda.

Kusema ukweli mm sikuchukua jina la huyo sales officer wenu,huwezi hata kuwauliza wanakua ni wajeuri vibaya mno, na dharau juu, ila kama mnataka kufatilia tumeni mtu ajifanye kama anaenda kununua tiketi, ikiwa imebakia kama saa moja boti kuondoka, unaenda na elf 25 wanakwambia tiketi zimebaki za elf 35 au 50 tu na ulilipa wanakupa tiketi ya elf 25. Ukiwa mkali anakuja mlinzi anakwambia kaa pembeni.....yaani ni maudhi na uzalilishaji mkubwa.
Jina la sales officer na book ID no. viko kwenye tiketi yako.
Tunashukuru kwa maoni yako, Kampuni iko kwaajili ya wateja wetu. Na suala hili linafuatiliwa na hatua kali zitachukuliwa. Kampuni inahitaji ushirikiano wenu ili kutokomeza tatizo hili. Endapo kitendo hicho kinatokea siku za mbeleni (hatutegemei kirudie) kamwe usikubali kulipia tiketi kwa gharama ya juu zaidi ya bei halisi inayoonekana kwenye tiketi. Ni vyema unapopoewa tiketi yako ihakikishe kabla hujaondoka kaunta. Na kama haujaridhishwa una haki ya kuhoji papo hapo kwa wahusika. Hakikisha unanunua na kulipia tiketi yako ndani ya ofisi yetu au kwa wakala wetu ambaye ni Ballack Safaris na sio vinginevyo. (Kwa wateja wa Dar es salaam)
 
Tafadhali nitumie PM tuwasiliane zaidi. Mimi ni mgeni kwenye mtandao huu.
 
Jina la sales officer na book ID no. viko kwenye tiketi yako.
Tunashukuru kwa maoni yako, Kampuni iko kwaajili ya wateja wetu. Na suala hili linafuatiliwa na hatua kali zitachukuliwa. Kampuni inahitaji ushirikiano wenu ili kutokomeza tatizo hili. Endapo kitendo hicho kinatokea siku za mbeleni (hatutegemei kirudie) kamwe usikubali kulipia tiketi kwa gharama ya juu zaidi ya bei halisi inayoonekana kwenye tiketi. Ni vyema unapopoewa tiketi yako ihakikishe kabla hujaondoka kaunta. Na kama haujaridhishwa una haki ya kuhoji papo hapo kwa wahusika. Hakikisha unanunua na kulipia tiketi yako ndani ya ofisi yetu au kwa wakala wetu ambaye ni Ballack Safaris na sio vinginevyo. (Kwa wateja wa Dar es salaam)

Thanks kwa ufatiliaji,nitakujulisha mapema kama tatizo lipo au halipo,maana mm ni msafiri sana wa boat zenu,this time, nitawa record, ila hii inakua ni nguma sana, kwa sababu hata ukimfata hawezi kukubali atasema mimi nimekulipisha kama ilivyoandikwa kwenye ticketi, kwa sababu unapolipa elf 50 ukapewa tiketi ya elf 25 unakua hupewi receipt ya ile elf 50 uliyotoa, unapewa tu ticket na imeandikwa elf 25, sasa hata ukimfata siku ya pili,atakwambia ushahidi uko wapi, atasema mm nimekulipisha elf 25, unakua huna ushahidi, ila tutakachofanya ni kurecord sauti na ikiwezekana hata video, tunataka hili jambo likomeshwe kabisa,na naomba na nyinyi mfatilie kwa ukaribu, pananuka rushwa sana pale,hasa Dar es salaam terminal.Rushwa nyengine ni ile wanakufata kama uko economy class, wanakwambia kama unataka kwenda VIP nipe elf 10 au 15 nikupeleke VIP, kuna rushwa mbaya sana , na wanaharibu sifa nzuri ya AZAM MARINE.
 
Hua zinapitia system kabisa, na ni electronic, ndio maana unaweza kuenda na tickets numbers tu na kupata tickets.
Usijifanye uko ulaya. Unadhani kila mtanzania anaweza ku access mtandao? Mimi mwenyewe nnauzoefu na kutumia mtandao, kuna siku nilihangaika we na si kufanikisha kwani mara mtandao uko down na sio friendly.

Watumiaji tu mshauri ni Bakhresa achukue maoni na aboreshe huduma kuondoka na na ulanguzi. Ulanguzi ni dhulma.
 
Back
Top Bottom