Natamani kuifanya familia yangu kuwa kama ya Bakhresa na ya akina Mo Dewji, nipeni muongozo

Kazanazo

JF-Expert Member
Aug 16, 2023
1,654
3,033
Wakuu kwenye familia yetu tuna asset muhimu kama ardhi, mashamba na nyumba kadhaa ila usimamizi ndio hakuna.

Kama mtoto niliesomeshwa na kuhitimu elimu ya juu natamani siku moja familia yangu iwe familia kubwa na yenye miradi endelevu kwa manufaa ya familia na jamii kwa ujumla.

Wakuu, kwa heshima na taadhima naomba mnipe muongozo na mawazo kipi nifanye ili kufikia malengo yangu ya kuifanya familia iwe kama ya Bakhresa.

Natanguliza shukrani.
 
Wakuu kwenye familia yetu tuna asset muhimu kama ardhi, mashamba na nyumba kadhaa ila usimamizi ndio hakuna

Kama mtoto niliesomeshwa na kuhitimu elimu ya juu natamani siku moja familia yangu iwe familia kubwa na yenye miradi endelevu kwa manufaa ya familia na jamii kwa ujumla

Wakuu, kwa heshima na taadhima naomba mnipe muongozo na mawazo kipi nifanye ili kufikia malengo yangu ya kufaifanya familia iwe kama ya Bakhresa

Natanguliza shukrani

Kuwa na ule utamadanu wa kutojiibia kwanza ukifanikiwa kuwa nao warithishe watoto wako .
 
Kikubwa ni kufanya biashara nyingi.mfano kama kwenye kilimo,kuuza mazao yaliyochakatwa tayari,kwenye madini,ufugaji n.k.Kwa kuanza unaweza kuanza na kimoja unachopenda lakini usijisumbue na ajira serikalini labda uanzie ngazi ya ukurugenzi na kuendelea.serikalini ni kujichelewesha tu
 
Jibu kwanza maswali yafuatayo:-
1. Wazazi wako bado wapo hai?
2. Baba yako alikua ana wake wangapi?
3. Mmezaliwa wangapi na wewe ni mtoto wa ngapi?
4. Ndugu zako mlio zaliwa nao wana ajira ama wana namna wanajiingizia kioato?
5. Hali ya mahusiano ndani ya familia yenu yapoje?
6. Umewahi kumshirikisha mzazi wako kama unatamani kuendeleza mashamba, kuboresha majengo ama kuendeleza viwanja?
 
Back
Top Bottom