Nataka kuacha kazi, ushauri tafadhali!

MIE NILIFANYA HIVYO 2008 JULY 21. NAKUMBUKA NILIMWAMBIA WIFE HUU NDIO MSHAHARA WA MWISHO SOO USITARAJIE KUNIONA NAPOKEA MSHAHARA..ISHI KISAIKOLOJIA KUWA MUME HANA KAZI NA FAMILIA INATAKIWA IENDE...TUPO MJINI JIANDAE KUPIKIA KUNI, JIANDAE KUTIMULIWA NYUMBA YA KUPANGA, JIANDAE KILA KITU KUYUMBA...

BAADA YA MIEZI 6 NIKAGUNDUA NIMEWEZA KUWEKA AKIBA BADALA YA ZAMANI NILIKUWA NADAIWA MADENI PESA HAITOSHI KILA SIKU DUKANI KWA MANGI UNATIA MISALA UNAICLEAR MWISHO WA MWEZI.

PEOPLE FEAR WHAT THEY DO NOT UNDERSTAND...AND...FIGHT THE WAR THEY CAN NOT CONQUER...

A MAN WAS BORN TO DIE CONTINUOUSLY AND START AFRESH......

MPAKA LEO SIJUTII KUACHA KAZI JAPO ZIPO SIKU MAMBO YANAKUWA MAGUMU ILA SIO KWA SABABU MUNGU HAKUNIPA RIZIKI ...HAPANA.. ILA NI KWA SABABU RIZIKI NILIYOPEWA NILIITUMIA VIBAYA KUSHINDWA KUNIFIKISHA SIKU YA RIZIKI NYINGINE.

NAOMBA MLETA MADA USOME USHUHUDA WANGU HUU NA HIZO QUOTES ZA KISHUJAA ZIKUTIE NGUVU KUFANYA MAAMUZI.

UKIMALIZA CHUO KIKUU TUNATARAJIA UWE NA UWEZO MKUBWA WA KUYATATUA MATATIZO KULINGANA NA MAZINGIRA YALIYOKUZUNGUKA...KINYUME CHA HAPO ELIMU ULIYOIPATA HAIKUSAIDII KITU NA PIA UNAKUWA HUJAELIMIKA...UMEPITA CHUO KAMA WANAOPITA KUJIUNGA VIFURUSHI VYA CHUO.
Mkuu asante sana kwa ushuhuda wako,na kujitolea muda wako kuandika huu ushauri wako.Nakuhakikishia kuwa ntaufanyia kazi.Kuhusu elimu ya chuo,hilo lisikupe taabu mkuu,elimu ya chuo siku hizi ni elimu tu kama ya Madrassa uliyoyasema hapo awali.asante sana kwa ushauri wako!.Pia naamini kwamba uzi unapowekwa hap Jf,unawekwa na mtu mmoja ila unawanufaisha watu wengine maelfu huenda hata zaidi ya aliyeuweka.
 
SHULE NTAKWENDA KILA NTAKAPOPATA NAFASI NA NISEHEMU YA KUCHUKUA UJUZI SIWEZI KUWA MUOGA WA MAISHA KWA KUOGOPA KUJIAJIRI,,, MWINGINE ANAUMIA KISA SIFA KAAJIRIWA PAMBANA MTOTO WA KIUME AKISTAAFU KAFA PRESHA KATEPELIWA KAKIINUA MGONGO KOTE AU BIASHARA IMEKUFA MANA ANATAKA MATOKEO YA HARAKA ILI ALE.
 
mkuu mi mwenyewe niliacha nlijikuta hela naishia kulipa madeni, nauli na kula na unaowasikia mafisadi na wizi chanzo ni maslahi madogo wanaongeza kipato kwa njia za hatar mala mhasibu kazidisha sifur mala mkaguz anataka pesa akubebe mwanzo maisha yalikuwa magumu saiv nasonga na hata waliotoboa maisha ni wale wenye usubutu na kujituma siamini kama MUNGU KAUMBA KIUMBE CHAKE KITESEKE maisha si lazima kuajiriwa tujue na kujiajiri.

SAFI SANA
Kumbe wanaosema ajira nzuri ni kwa sababu ni wadokozi kwenye ajira zao. Unamkuta mtu ni store keeper kwenye store ya chakula - kila siku anaondoka na kilo mbili za mchele, mara unga , mara maharage, mtu huyu lazima awaze kwamba akiacha kazi hatapata chakula na akiba yake itaishia kwenye chakula ... mtu huyu ni kilema wa akili kabisa, kamwe hawazii kingine zaidi ya kunyenyekea kwa mwajiri wake na kuleta majungu ili wenzake waachishwe kazi abaki yeye aibe vizuri. Mshahara pekee hufanyi lolote la maendeleo
 
Wakuu Mandella na Tutor B hakuna sababu ya kugombania fito wakati wote tunajenga nyumba moja.Wazo la kila mtu linafaa kwa kujenga msingi fulani wa kuanzia na kusonga mbele.
 
USIMTISHE MWENZIO
Wapo waliodhubutu na sasa hv wana maisha mazuri zaidi ya walioajiriwa miaka 30..........
Acha uoga



HEBU FIKIRIA KAMA SIO UTUMWA NI NINI WAZIRI NI PROFESA ANATUMIWA WATU WAENDE KUMREKODI AKILALAMIKA ALICHOPEWA HAKIKIZI MAHITAJI ILI AFUKUZWE KAZI JE HUO SIO UTUMWA NA AIBU? TATIZO ELIMU YETU TUMEANDALIWA KUWA WATUMWA SIO WAVUMBUZI NA KUJITEGEMEA.

HEBU TUJARIBUNI VIJANA SAIV TUNAENDA KIPIND CHA MAVUNO BAADHI YA MIKOA NA TUNASIKIA NCHI JIRANI TAYAR WANALALAMIKA NJAA JE HIYO SIO FURSA? TUJARIBUNI SERIKALI ITUPE KAMPANI.
 
Unaonekana unaogopa mtaani, kwamba kuna ukosefu wa ajira!
Sasa kabla hujaacha kazi, jiandae vizuri, andisha biashara iendeshe huku ukiwa bado umeajiriwa mpaka uhakikishe hiyo biashara inaweza kuendesha maisha yako hapo ndipo uache kazi, kitaa ni kigumu sana kama huna confidence
tatizo mkuu kuanzisha biashara wakati unafanya kazi kwa mhindi ni ngumu sana,huwezi kupata hata huo muda wa kufuata viazi mbatata huko Mbeya ulete Dar.
 
Mkuu,ushauri wangu usiache kazi ghafla kabla hujasuka mikakati ya shughuli utakayoifanya baada ya kuacha kazi,kujiajiri ni jambo la busara sana japo lina changamoto kubwa ya ubunifu na ili ufanikiwe katika hii sekta inabidi uishinde hii changamoto ya "ubunifu" kuepuka kufanya anachofanya mwingine kwa level ileile,kaa chini Fanya utafiti wa kutosha juu ya unachotaka kufanya kisha anza kuendesha huo mradi wako ukiwa kazini na utapoona mradi wako umekakamaa unaweza kusimama kwa miguu yote miwili hapo nakushauri acha kazi rasmi jikite kwenye miradi yako,ila kubwa kuliko yote mtangulize MUNGU katika kila unalotaka kulifanya uombe hekima na busara zake zikuongoze
Suala la pesa ya muhindi kuwa haifanyi jambo la msingi nafananisha na ule usemi wa pesa ya boom la chuo huwezi fanyia jambo la maana zaidi ya kununua nguo na subwoofer, mkuu hilo suala lipo kiimani sana na ukweli ni kwamba tunasahau kwamba 10% ya mapato yetu kila siku ni Mali ya MUNGU hivo yapasa tumrejeshee yeye mwenyewe,mkuu nakuhakikishia hakuna ulinzi mzuri wa mapato yako zaidi ya kumtolea BWANA fungu la kumi pesa zako utaziona utamu wake na utaztumia as ulivopanga bila ufujaji wa nia ovu ya shetani.
 
Mkuu,ushauri wangu usiache kazi ghafla kabla hujasuka mikakati ya shughuli utakayoifanya baada ya kuacha kazi,kujiajiri ni jambo la busara sana japo lina changamoto kubwa ya ubunifu na ili ufanikiwe katika hii sekta inabidi uishinde hii changamoto ya "ubunifu" kuepuka kufanya anachofanya mwingine kwa level ileile,kaa chini Fanya utafiti wa kutosha juu ya unachotaka kufanya kisha anza kuendesha huo mradi wako ukiwa kazini na utapoona mradi wako umekakamaa unaweza kusimama kwa miguu yote miwili hapo nakushauri acha kazi rasmi jikite kwenye miradi yako,ila kubwa kuliko yote mtangulize MUNGU katika kila unalotaka kulifanya uombe hekima na busara zake zikuongoze
Suala la pesa ya muhindi kuwa haifanyi jambo la msingi nafananisha na ule usemi wa pesa ya boom la chuo huwezi fanyia jambo la maana zaidi ya kununua nguo na subwoofer, mkuu hilo suala lipo kiimani sana na ukweli ni kwamba tunasahau kwamba 10% ya mapato yetu kila siku ni Mali ya MUNGU hivo yapasa tumrejeshee yeye mwenyewe,mkuu nakuhakikishia hakuna ulinzi mzuri wa mapato yako zaidi ya kumtolea BWANA fungu la kumi pesa zako utaziona utamu wake na utaztumia as ulivopanga bila ufujaji wa nia ovu ya shetani.
Ubarikiwe sana mkuu kwa kutoa muda wako na maarifa yako kwa manufaa yangu na wengine pia.
 
tatizo mkuu kuanzisha biashara wakati unafanya kazi kwa mhindi ni ngumu sana,huwezi kupata hata huo muda wa kufuata viazi mbatata huko Mbeya ulete Dar.
Anza ata ufugaji wa kuku, unaweza kukodi banda,ukatafuta kijana au mke awasimamie, kuku wa nyama au wa Mayai,
Siyo lazima viazi
 
HEBU FIKIRIA KAMA SIO UTUMWA NI NINI WAZIRI NI PROFESA ANATUMIWA WATU WAENDE KUMREKODI AKILALAMIKA ALICHOPEWA HAKIKIZI MAHITAJI ILI AFUKUZWE KAZI JE HUO SIO UTUMWA NA AIBU? TATIZO ELIMU YETU TUMEANDALIWA KUWA WATUMWA SIO WAVUMBUZI NA KUJITEGEMEA.

HEBU TUJARIBUNI VIJANA SAIV TUNAENDA KIPIND CHA MAVUNO BAADHI YA MIKOA NA TUNASIKIA NCHI JIRANI TAYAR WANALALAMIKA NJAA JE HIYO SIO FURSA? TUJARIBUNI SERIKALI ITUPE KAMPANI.
POINT MKUU
 
Kumbe tupo wengi wenye mawazo ya kujiajiri. Kiukweli tangu niajiliwa naona napata hela ya kula na kulipa kodi tu. Nadhani imefika wakati wa vijana kujiongeza na kuamua kuthubutu kutafuta ramani za kutokea kuliko kusubiria mshahara usiotosha mwisho wa mwezi. Japo mwanzo utakuwa mgumu ila **** una wazo na umeshafanya UPEMBUZI YAKINIFU nami nakushauri ACHA KUFANYIA WATU KAZI ILI UANZE KUJIFANYIA KAZI
 
Ndugu , kwanza kabisa pole sana na maswahibu ya unyonyaji wa hao maboss zako wahindi.
Pili, ninakushauri usithubutu kuacha hiyo kazi kwani huo mshahara unaoupata si haba sana. Unachotakiwa kufanya ni kuitatua hiyo changamoto inayokukabili ya kushindwa kufaidi matunda ya jasho lako. Changamoto hiyo ni ndogo tu ninakushauri ufanye ifuatavyo:

Kwakuwa Giza na Nuru havichangamani, wao wanatumia nguvu za giza kukunyonya basi wewe huna budi utumie nuru kujinasua katika unyonyaji huo . Nakushauri Kwa kila mshahara unaoupata tenga asilimia kumi yake na ukatoe pale unapoabudia, iwe ni kanisani au msikitini (kulingana na imani yako ) na kama hauna dini basi hiyo asilimia kumi peleka kwenye kituo cha kulea watoto yatima. Hakika ninakwambia ukifanya hivyo utafaidi matunda ya jasho lako na mambo yako yatakunyookea kuliko ulivyowahi kufikiria. Nakutakia Kila lakheri .
 
Kwanza pole sana!
Pili ..... (Kuna kalugha nakasikia mtaani kwamba pesa ya mhindi huwezi kuifanyia chochote) .. kuhusu hili binafsi niliwahi kulisikia ila inasemekana kwamba ili uifanyie kazi hiyo hela kuna namna unayopaswa kuifanyia .... kama uko tayari kujuzwa tuwasiliane ...

tatu, binafsi nilishahachana na mambo ya kuajiriwa zaidi ya miaka 5 iliyopita .. kuna msoto kidogo kama wa miezi sita hivi .. baada ya hapo hutapenda ajira tena, .... we piga kazi za mikataba beba kilicho chako, fanyia mambo mengine ya uzalishaji ... mdogo mdogo utasimama ndugu ...
Mkuu Tutor B nahitaji tuongee inaonekana wewe ni msaada sana nachotaka kufanya wewe tayari umefanya
 
naomba niamdike ushauri Wang kwa Herefi kubwa .


USITHUBUTU ,USITHUBUTU,USITHUBUTU ...KUACHA KAZI . TENA KAMA HAUNA KAZI NYINGINE ..

USITHUBUTU UTAJUTA MAISHA YAKO YOTE
Usimkatishe tamaa ndugu,kuajiliwa ni utumwa na kubeba hofu kubwa ktk maisha.unaweza ajiliwa kutafuta kianzio tu kama pesa ya kuendesha biashara zako na kilimo.ajira ni kelo,hofu,ufinyu wa mawazo,kupoteza network ktk jamii na kuilaza akili kwa kufikili jambo moja tu kila ukiamka,hapa mimi nimechukua likizo kazini na sirudi tena huko,nawaandikia notice ya mwezi m1 nachapa mwendo,ntaendesha hata taxi mtaani bola tu iwe yangu na nyingine nimpe mtu mwingine,naweza nunua hata gari tatu nikakaa kijiweni.mtoa mada songa mbele piga chini
 
Samahani kwa nitakaye mkwaza kwa hili.


Kuacha kazi kuna pande mbili,,
1. Kufanikiwa na kuishukuru akili iliyokutuma kufanya hivo na
2. Kushindwa na kujutia hasa kwa kuilaumu akili iliyokutuma kufanya hivo

Ikumbukwe hakuna asiye bisha kua ukiajiriwa ujue unafanya kazi kwa aliyejiajiri kataa ukubali na ukifuatulia chenye gharama hua ni bora

Kujiajiri ni bora na kuna gharama yake kwani unapoajoriwa na mtu inaonekana kabisa ujuzi ulio nao umeahindwa kuutumia na ukakubali akili ya mtu aliyejiajiri kuutumia,, hapo mi nasema ni mgando wa fikra na kutafuta unafuu wa maisha pasipo ku-u- weka uhalisia wa maisha

Naamini watanzania wengi hasa vijana tunaishi maisha ya maigizo sana na hicho hutufanya sisi kushindwa kufanya maamuzi kwani tumeshindwa kujitoa katika dimbwi la kutegemea akili zetu, yaani tumekua tegemezi kwa kila kitu,,
Kingene sisi ni wavivu sanaa na ndio tunapenda kutumikishwa na mtu aliyefanya juhudi akaukana uvivu wa kufikiri na kutenda, kwa mfano mpaka hapo yawezekana hauna katiba ya maisha yako ndio maana unashindwa kuamua.
Cha kukushauri sasa ni hiki,,


Kama unataka kuacha kazi jiandae katika kila nyanja
Kisaikolojia
Kiakili
Kiuchumi( matumizi)
Na vilevile unapaswa uandike project ya maisha yako inje ya kazi ili itumike kukuongoza utakapo kua inje ya kituo
Ukumbuke kabisa kua ukijiari usitegemee kukosolewa kwa utendaji m bovu utakao ufanya na hapo ndio itakua kifoa cha fikra kitakukumba,, ujuzi uliokua unaufanyia kazi kule uzidishe mara dufu ili kuongeza uzalishaji wako hapo jipe mda fuatilia jeee uko ndani ya chaki ya mipango yako??


Ongeza juhudi katika kazi utakayoichagua ipe muda zaidi ya ule wa kazi ya kuajiriwa tune your mind epuka mawazo finyu ya kuwaza kummilikisha ujuzi mtu mwingine. Jitume na amua kwa juhudi.

Yafuatayo yazingatie kwa manufaa yako
1. Andaa mchanganuo wa kazi unayotaka kujiajiri kisha ufanyie utafiti
2. Anza sasa baada ya kumaliza mchanganua lakini hakikisha umeuchambua vizuri kama unavofanya hapo offisini kwa muhindi
3. Muandae mkeo awe wa kukutia moyo na kukushika mkono kwani ikumbukwe unaingia katika mapambano
4. Punguza matumizi kwako kwa kila namna mpak mshahala wako unaojilipa baada ya kazi mf.starehe, burudani n.k
4. Acha wizi ndani mwako na hasa tabia ya udokozi, hapa namanisha unachukua kijisent hata kidogo halafu hata hukiandikii kinapotea tuu hivihivi bila ya kujua ukifanya hivo mwisho wa siku utashindwa kujua gharama halisi ya maisha yako kwa kipindi unachojifanyia kazi

Hayo ni baadhi tu ya ushauri wangu wa bure

IPE AKILI NAFASI YA KUPAMBANA KWA MANUFAAA YA NAFSI YAKE NA SI KWA MANUFAA YA MUHINDI
IKUMBUKWE KUA NAFSI YALO INAUMIA KUONA AKILI YAKO INATESEKA KWA AJIRI YA MUHINDI
 
[QUOTE="
Suala la pesa ya muhindi kuwa haifanyi jambo la msingi nafananisha na ule usemi wa pesa ya boom la chuo huwezi fanyia jambo la maana zaidi ya kununua nguo na subwoofer, mkuu hilo suala lipo kiimani sana na ukweli ni kwamba tunasahau kwamba 10% ya mapato yetu kila siku ni Mali ya MUNGU hivo yapasa tumrejeshee yeye mwenyewe,mkuu nakuhakikishia hakuna ulinzi mzuri wa mapato yako zaidi ya kumtolea BWANA fungu la kumi pesa zako utaziona utamu wake na utaztumia as ulivopanga bila ufujaji wa nia ovu ya shetani.[/QUOTE]
Kwenye fungu la kumi ndo anaponitia uvivu...watumishi wenyewe matajiri kuliko waumini..alafu bado wanataka tuwape fungu la kumi
 
Back
Top Bottom